Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
Muundo wa MUUNGANO ni wa serikali mbili tuuuu tatu za nini??? Vijana wenzangu tujisomee tusifuate mkumbo.. Tuielewe historia ya nchi yetu... Mfano mdogo nautoa ni hivi Tanganyika ni Jina lililotumiwa na Wajerumani nami siku za usoni naona Wajerumani wanakujakuja hawahawa ndio wanaowashawishi baadhi ya vijana wapmbane ili wapate Tanganyika Yao.. Tukumbuke Kusini mwa jangwa la Sahara nchi pekee ambayo haijaathiriwa na vita ni Tanzania pekee.. Vijana tuwe na jicho pevu
 
Shida si muungano.

Nionavyo mimi ni kutokuwepo kwa uwazi kuhusu muungano unaosababisha kuonekana kwamba kuna unyonyaji fulani.

Ndoa zinatengana itakuwa muungano usio na tija?????

Kwani USSR iko wapi?????
 
wanajf kwa mda mrefu sasa kuelekea utungaji wa katiba mpya kumekuwa na mjadala mkali kuhusu muungano wetu uwe wa muundo upi sasa ningependekeza tuwe na kura ya maoni hapa jf kuhusu muundo wa muungano, upi ni muundo sahihi?

1.serikali moja.
2. Serikali mbili.
3.serikali tatu.

N:b ukiweza kutoa sababu za muundo wa muungano unaoutaka itakuwa vizuri zaidi

===============

Kumbe unajielewa ukakasi kibao humo ndani porojo nyingi ili kutushawishi, usiifanye tanzania uwanja wa majaribio katiba inayopendekezwa ndiyo fainali ya yote we subiri watanzania waamue wenyewe afu hizo serikali 3 zako utaenda kuzianzisha chini ya bahari.
 
shida si muungano.

Nionavyo mimi ni kutokuwepo kwa uwazi kuhusu muungano unaosababisha kuonekana kwamba kuna unyonyaji fulani.

Ndoa zinatengana itakuwa muungano usio na tija?????

Kwani ussr iko wapi?????

acha kukariri historia ya walioshindwa nani kakuambia sisi ni ussr, acha dharau kama ndoa yako imekushinda pole sana, hii ya katiba pendekezwa huiwezi waachie wenye akili au kama vipi hamia somalia ukaanzishe 3.
 
ASANTE KWA USHAURI WAKO NA MUHIMU WASOME HAPA

Uhusiano na Uratibu wa Mambo ya Muungano (Ibara za 127 – 128)

Katiba Inayopendekezwa inaimarisha Muungano wetu kwa kuanzisha Tume ya Usimamizi na Uratibu wa Mambo ya Muungano. Chombo hiki, pamoja na mambo mengine, kitakuwa na jukumu la kukuza na kuratibu ushirikiano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Mojawapo ya malengo ya uratibu huu ni kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya Serikali hizi mbili na kukuza kiwango cha utoaji huduma kwa wananchi wote.

Kwa utaratibu wa sasa ipo Kamati inayoshughulikia masuala ya Muungano ambayo inaongozwana Makamu wa Rais. Kwa Katiba Inayopendekezwa chombo hiki sasa kitakuwa na nguvu ya kisheria na hivyo kuweka mfumo madhubuti zaidi wa kushughulikia changamoto za Muungano na pia kuratibu masuala mengine yanayohusiana na ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar kwa ujumla wake.
 
Ally saleh huna hoja umejaza tu saver ya jf kwa kushabikia siasa na kutaja vyama utafikiri huo muungano ni wa vyama!!,
 
Serikali tatu sababu zangu ni sawa na zile za Jaji warioba za kitaalamu zaidi.

Wewe na huyo mzee wote ni wachumia tumbo hakuna taaluma hapo mbili zatosha 3 za nini au mnataka Jamhuri ya Pemba na Unguja? Hamjielewi nyie na mawazo yenu ya kielshabab!!!
 
Huoni kwa sasa kuna watu hawaridhiki...anyway ulisoma hesabu za seti?

Zote hesabu kwani vipi mbili zatosha hao wasioridhika mbona bado wanaishi TZ na wana biashara zao kubwa, wamejenga, wameoa na kuolewa, wamesoma na wanaenjoy maisha bara na visiwani acheni hizo kutuletea mambo ya CECAFA kwenye uhai wa taifa.Kutokuridhika ndio tabia ya wanadamu mpaka siku ya kiama!!!
 
3. Serikali 3
Achana na mambo ya Muundo wa Muungano katika kipindi hiki. Nenda kwanza kajiandikishe kupiga kura kuhusu Katiba Inayopendekezwa. Masuala ya Muundo wa Muungano yalijadiliwa sana katika Bunge Maalum la Katiba ambalo nina hakika hukulisikiliza na hukujua kama lilikuwepo kwa maana kipengele hiki kilijadiliwa na maamuzi yake kufikiwa. Labda kwa kukusaidia muundo ni wa Muungano unaoundwa na serikali mbili. Soma Katiba Inayopendekezwa na usichanganye madawa kwenye forum. Kwa heri.

ASANTE KWA USHAURI WAKO NA MUHIMU WASOME HAPA

Uhusiano na Uratibu wa Mambo ya Muungano (Ibara za 127 – 128)

Katiba Inayopendekezwa inaimarisha Muungano wetu kwa kuanzisha Tume ya Usimamizi na Uratibu wa Mambo ya Muungano. Chombo hiki, pamoja na mambo mengine, kitakuwa na jukumu la kukuza na kuratibu ushirikiano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Mojawapo ya malengo ya uratibu huu ni kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya Serikali hizi mbili na kukuza kiwango cha utoaji huduma kwa wananchi wote.

Kwa utaratibu wa sasa ipo Kamati inayoshughulikia masuala ya Muungano ambayo inaongozwana Makamu wa Rais. Kwa Katiba Inayopendekezwa chombo hiki sasa kitakuwa na nguvu ya kisheria na hivyo kuweka mfumo madhubuti zaidi wa kushughulikia changamoto za Muungano na pia kuratibu masuala mengine yanayohusiana na ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar kwa ujumla wake.
Wewe si ulifungiwa au kifungo umemaliza. Pole karibu kwenye forum lakini zamu hii uwe makini usije ukarudi gerezani.
 
Achana na mambo ya Muundo wa Muungano katika kipindi hiki. Nenda kwanza kajiandikishe kupiga kura kuhusu Katiba Inayopendekezwa. Masuala ya Muundo wa Muungano yalijadiliwa sana katika Bunge Maalum la Katiba ambalo nina hakika hukulisikiliza na hukujua kama lilikuwepo kwa maana kipengele hiki kilijadiliwa na maamuzi yake kufikiwa. Labda kwa kukusaidia muundo ni wa Muungano unaoundwa na serikali mbili. Soma Katiba Inayopendekezwa na usichanganye madawa kwenye forum. Kwa heri.

Ha ha ha ha...nikijiangikisha nipige kura gani?
 
Back
Top Bottom