Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
OLE WAKO TANZANIA...

Taifa lenye vijana walio tayari kuua,
Kuua kwa ajili ya Ukuwadi na Utumwa,
Kuua kwa ajili ya kutumwa na wakubwa,
Matajiri waliogeuza nchi hii Ubwabwa.

Ole wako Tanzania unayechezea amani,
Amani iliyodumu barabarani hadi nyumbani,
Amani imekuwa ghari sasa jaribu vitani,
Kwa kutumia vijana waso maadili ukubwani.

Ole wako chama kubwa kulewa madarakani,
Hakika pakichafuka utakuwa mashakani,
Afrika italia wakubwa mbio ulayani,
Unaanza twamaliza tumechoka asilani.

Ole wenu vyombo dola kwa kushindwa majukumu,
Kwa hakika wananchi watabeba gurudumu,
Gari letu litasonga bila nyinyi kwa ugumu,
Tutalinda Tanzania kwa ushindi wa machungu.
 
serikali tatu ndio maoni yetu wananchi, sababu ziko nyingi sana ila naomba nikupe moja tu, kunaumuhim gani kutumi pesa za walipa kodi wa tanganyika kuwalipa posho na mishahara wanasiasa wa zanzibar ambao hatukuwachagua ss na hawana mchango wa maendeleo ya watanganyika? Tunataka 3 kodi zetu zinunue madawa hospital, madawati shuleni nk
 
Hehe madawa na mikopo ya wanafunzi ambao mpaka sasa hawajui la kufanya huko vyuo vikuu ni tungepata kwa zile vijisenti billion 200 wakubwa wengine wameropoka asubuhi kua ni zaidi ya hizo ni mia nne basi tu ililimradi maisha ya songe wakubwa wale nchi
 
Bara na visiwani wote ni watoto wa baba na mama mmoja,so kusema waishi sehemu moja ni ngumu,amani itatoweka baina ya ndugu coz wazazi hawakuwajengea misingi imara ya upendo na ni kwasababu ya udhaifu na uzembe wa kutokukamilisha sera. Mf. Ujamaa,udini na ukabila.(Unaccomplish mission in tripple wars) Kwa hiyo ni vigumu sana kuwa na mfumo wa serekali moja.
 
Sijaipokea vizuri kwa haina Hoja za kuwashitaki wanaohujumu uchumi wa nchi na ndio maaana wanatetewa kwa kupigwa chini vyeo baada ya kuwahukum,,, Tanzania iliyochafu pazuri ninapo kaa mm tu.
 
Mimi naona serikali tatu ingefaa kwa sababu Tanganyika hatujui inaongozwa na nani, zanzibar wana rais wao na serikali yao, kwa nini Tanganyika isiwe na utawala wake? afu iwepo serikal inayounganisha Tanganyika na Zanzibar. kama vp muungano haina haja
 
Back
Top Bottom