Kura ya maoni kwanza kabla ya mjadala wa katiba – Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kura ya maoni kwanza kabla ya mjadala wa katiba – Zanzibar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kakke, May 1, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Written by administrator // 01/05/2012 // Habari // No comments


  Salma Said,
  JUMUIYA ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar imetoa fomu maalumu ya kuorodheshwa idadi ya yatu wanaotaka kuitishwa kura ya maoni juu ya mustakabali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kabla ya katiba mpya. Jumuiya hiyo imeshirikiana na taasisi nyengine za dini ya kiislamu imeanza kusambaza fomu hizo hapo jana na kuzitawanya sehemu mbali mbali Unguja na Pemba na jijini Dar es Salaam.
  Lengo la kujaza fomu hizo ni kuchukua majina kamili, saini na namba ya vitambulisho vya wazanzibari au namba ya pasi ya kusafiria kwa wanaotaka kuitishwe kura ya maoni ya kuulizwa wazanzibari iwapo wanautaka au hawautaki Muungano uliopo wa Tanganyika na Zanzibar kabla ya tume iliyoteuliwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete kuanza kazi.
  “Tunataka kuulizwa kwanza iwapo tunautaka Muungano au hatuutaki halafu tena tume ya rais ianze kazi ya kukusanya maoni ya kuundwa kwa katiba mpya ya Tanzania lakini wakati huo tuwe tumeshaamua tunataka au hatutaki” alisema Kiongozi wa Jumuiya hiyo, Sheikh Azzan Khalid Hamdan.
  Hatua hiyo ni muendelezo wa harakati zinazofanyika hapa Zanzibar zinazofanywa na taasisi hizo ambapo kwa zaidi ya mwezi sasa kumekuwepo mikusanyiko na mikutano mbali mbali ya kuelezea faida na hasara za Muungano uliopo lakini pia matatizo na kero ambazo kwa takriban miaka 48 zimeshindwa kutatuliwa na viongozi waliopo madarakani.
  Kwa mujibu wa fomu hizo ambazo Mwananchi imepata nakala yake na kuthibitishwa na Sheikh Azzan kuwa taasisi yake ndio iliyoratibu zoezi hilo la kugawa fomu amesema tayari wameshazisambaza kila sehemu Unguja na Pemba na matarajio yao kufika hadi vijijini ili watu wapate fursa ya kujiorodhesha majina yao na kuweka saini zao kama ni ushahidi kabla ya fomu hizo kukabidhiwa Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein kwa hatua za zinazofuata.
  “Tumechapisha fomu 25,000, kila fomu watajaza watu 20 na tayari tunazisambaza kote, mjini na vijijni Unguja na Pemba, lengo ni kukusanya saini 400,000,” alisema Sheikh Azzan.
  Kuchapishwa kwa fomu hizo ni miongoni mwa harakati za wazanzibari mbali mbali kupitia vikundi na taasisi kadhaa zinazodai kuitishwa kwa kura ya maoni kwanza kabla ya tume ya Rais Kikwete kuanza kazi zake.
  Hivi karibuni Kiongozi mmoja wa kikundi cha wanaharakati wa taasisi ya kiraia iitwayo Umoja wa Wazanzibari (ZARFA), Rashid Salum Adiy na wenzake 12 kufikishwa mahakamani hapa Zanzibar wakituhumiwa kwa uhuni, uzururaji na kupinga Muungano baada ya kukusanyika katika viwanja vya baraza la wawakilishi.
  Watu hao 12 walikamatwa mwezi uliopita mwaka huu katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, ambako imedaiwa walikwenda kushinikiza baraza hilo kuitisha kura ya maoni ili kujua kama Wazanzibari wanataka au hawataki Muungano huu uliopo wa Tanganyika na Zanzibar ambao umetimiza miaka 48 hivi karibuni.
  Suala la kuitishwa kwa kura ya maoni juu ya Muungano limekuwa likizungumzwa na watu mbali mbali Zanzibar na hata Tanzania Bara ambapo hivi karibuni kupitia kipindi cha mazungumzo mbele ya meza ya duara kinachorushwa na idhaa ya kiswahili ya Ujerumani (DW) mwandishi wa Habari Maarufu Tanzania, Jenerali Ulimwengu alisema ipo haja ya kuitishwa mjadala wa wazi na kufanyika kwa kura ya maoni kwanza kabla ya tume kuanza kazi yake ya kukusanya maoni ya katiba mpya.
  “Kabla ya kuwa na Katiba mpya, kuwe na mdahalo wa wazi juu ya Muungano, waulizwe watanzania wanautaka Muungano au hawautaki, vinginevyo ni kupoteza fedha nyingi na muda wa watu,” alisema Jenerali Ulimwengu.
  Ulimwengu alisema suala la Muungano linapaswa kupewa nafasi muhimu katiba katiba na bila ya kujadiliwa Muungano hakuna katiba mpya kwani huwezi kuzungumzia katiba ya Tanzania bila ya kugusa Muungano wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar.
  “Zanzibar haina mwenza wake, Tanganyika …. katika hali hiyo hata uwepo wa Zanzibar katika Muungano hauonekani kikatiba,” alisema Ulimwengu.
  Ulimwengi ni miongoni mwa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliounda kundi lijulikanalo G 55 na kupeleka hoja Bungeni kutaka kufufuliwa kwa serikali ya Tanganyika lakini kwa wakati ule jambo hilo lilizimwa kimya kimya na Mwalimu Nyerere bila mafanikio yaliokusudiwa.
  Harakati za kutaka kura ya maoni na Zanzibar na kutolewa ndani ya mikono ya Muungano zimekuwa zikiendelea kila siku hapa Zanzibar licha ya kukemewa mara kadhaa na viongozi wa ngazi mbali mbali za serikali akiwemo makamu wa pili wa rais na mawaziri wanaohusika na masuala ya katiba.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi wakati akifunga kikao cha baraza la wawakilishi April 20, mwaka huu, alisema kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haitawavumilia tena wanaharakati wanachochea vurugu badala ya kutoa elimu juu ya masuala mbali mbali ya kijamii, likiwemo la upatikanaji wa Katiba mpya ya Tanzania .
  Lakini licha ya onyo hilo harakati hizo zimekuwa zikipamba moto kila kukicha kama kwamba hakuna tahadhari iliyotolewa kuhusiana na jambo hilo na taasisi hizo zimekuwa zikiongezeka zaidi na kuunga mkono jambo hilo ambapo sasa baadhi ya wanataaluma ya kisheria, wasomi, na wanasiasa mbali mbali wamekuwa wakiunga mkono harakati hizo wazi wazi na kusema mustakabali wa Muungano uamuliwe kwanza kabla ya Katiba mpya.

  www.mzalendo.net
   
 2. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #2
  May 2, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Tukubaliane.. Iko Haja ya kuongelea Dubwashika hili Muungano.. lazma.. Na Muafaka wa Muungano Na sintofahamu zote ziwekwe wazi tu.. Si Muda wa kuogopa tena..
   
Loading...