Kura ya maoni kuhusu muundo wa muungano na katba mpya

Fredrick Sanga

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
3,153
697
Katika kufatilia hali halisi ya mchakato wa kupata katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, nimeona nami nitoe maangalizo na maoni yangu binafsi.

Zanzibari imeshatunga katiba yake mpya. Je hii katiba ya muungano itagusa mabo yaliyomo katika katiba ya Zanzibari? Kama jibu ni ndiyo, basi hapa kuna kazi ya ziada, maana katiba ya Zanzibari inaweza kuimeza katiba mpya

Je kama wananchi watapenda zaidi mfumo wa serikali tatu. Nani atatengeneza rasimu ya serikali ya Tanganyika? Maana kuna uwezekano wa kuwa na mapendekezo ya serikali tatu kushamiri sana katika mchakato wa hii katiba mpya. Hii itasababisha haja ya kurasimu katiba mbili, yaana ya Tanganyika na ya Muungano.

Je kama wananchi watataka muungano upumzike, watakubaliwa au watafungwa kama wahaini. Kama watafungwa je huu mchakoto utakuwa huru kweli. Mimi napenda muungano uendelee, lakini labda wasioupenda ni wengi? Sijui? Je tume inajua?

Mwaka 1964 nilikuwa bado mdogo sana, lakini sikumbuki kama wananchi waliulizwa kuhusu, haja ya muungano, muundo, na mambo yake. Na kama kweli kuna mkataba wa Muungano, uko wapi? unasemaje? Je kuna tofauti kati ya mkataba wa muungano na hati ya muungano?

Inasemekana kuna hati zimefichwa, kama ni kweli ni kwanini? Muungano ni haki ya umma au serikali? Kama zipo, huu sio wakati muafaka wa kuzichapisha katika magazeti ya serikali? ili nasi tujue yaliyomo ili kuondoa haya mambo ya uvumi uvumi. Yanawapa watu visingizio vya kuzungumza mengiiii.

Naona kama kuna haja ya kuangalia vizuri sana huu mchakato wa katiba. Bado naamini kabisa ukifanyika vizuri utamjengea Raisi na bunge letu heshima kubwa sana kihistoria, na nchi kutupatia amani na maendeleo ya kudumu.

Nengeshauri, kwa hali ilivyo sasa, bila kutumia vitisho, maoni ya awali yakakusanywe Zanzibar (Pilot study), ili tume iweze kuwa na roadmap nzuri. Sikubaliani na vitendo vya kihuni, na nategemea vyombo vya sheria vinashughulikia. Ila nahisi kuna kitu cha kuangaliwa kwa umakini sana Zanzibar.

Nayasema haya kwa nia nzuri, nikiamini kutoka moyoni kwamba naipenda nchi yangu, na vizazi vyake vijavyo. Na ningependa sana amani ya kweli katika mfumo wa demokrasia ijengeke na kukomaa kadri miaka inavyoendelea. Bila katiba muafaka, nahisi matatizo makubwa mbele ya safari. Kuna haja sana ya kujikana nafsi zetu, katika suala la kutengeneza katiba mpya, yaani tunatikiwa kuwa wayakinifu zaidi, kuliko kubebwa na ushabiki wa aina yeyote ile.

Mod hii sio habari mchanganyiko, be fair.

Samahani kwa nikaokuwa nimewakwaza.
 
EXCELLENT muandishi umebase kwenye ukweli zaidi, kuliko matashi yako binafsi. i like it.

inabidi kama itakuwa serikali tatu tanganyika iunde bunge lao la tanganyika na bunge lilikuwepo liwe la muungano au vp?
na bunge la tanganyika liwe responsible kwa kupitisha katiba ya tanganyika.

NGUMU SANAAAAA. Bora muungano uvunjike maana hiyo gharama ya kuendesha hayo mabungee ni nomaaa.
 
Naona tuwe na wabunge wa wilaya tu, watapungua sana. Mawaziri watabaki wale wale, ataongezeka raisi mmoja tu wa Jamhuri ya muungano. hatuhitaji makamo wa raisi, waziri mkuu anatosha. nakuahakikishia, upo uwezekano wa kupunguza gharama. Hata hili baraza la mawaziri 54 la nini? Wakuu wa wilaya, watakuwa wabunge. Ila kama mkikubali, kwa hiari yenu.
 
EXCELLENT muandishi umebase kwenye ukweli zaidi, kuliko matashi yako binafsi. i like it.

inabidi kama itakuwa serikali tatu tanganyika iunde bunge lao la tanganyika na bunge lilikuwepo liwe la muungano au vp?
na bunge la tanganyika liwe responsible kwa kupitisha katiba ya tanganyika.

NGUMU SANAAAAA. Bora muungano uvunjike maana hiyo gharama ya kuendesha hayo mabungee ni nomaaa.

Kuuvunja muungano ni sawa na kula sumu. Hii siikubali kabisa
 
Kuuvunja muungano ni sawa na kula sumu. Hii siikubali kabisa

Mimi nina ndugu kabisa huko zanzibari, na wadogo zangu wameoa huko. Sioni haja ya kuvunja muungano, ila kuujadili na kuuimarisha. Hii mambo ya Muamusho ni hovyo kabisa.
 
Sikubaliani kabisa kabisa na mjadala wowote wa kuuvunja
muungano wa Jamhuri ya Tanzania.
Huu ni uhaini mkubwa ambao haujapata kutokea
hapa Tanzania,mara ya mwisho ulizungumzwa
bungeni na baadhi ya mawaziri mkuu na wafuasi wake
walipigwa chini,.....pigwachini...G55.

EXCELLENT muandishi umebase kwenye ukweli zaidi, kuliko matashi yako binafsi. i like it.

inabidi kama itakuwa serikali tatu tanganyika iunde bunge lao la tanganyika na bunge lilikuwepo liwe la muungano au vp?
na bunge la tanganyika liwe responsible kwa kupitisha katiba ya tanganyika.

NGUMU SANAAAAA. Bora muungano uvunjike maana hiyo gharama ya kuendesha hayo mabungee ni nomaaa.

Hakuna ghalama acha propaganda za kimagamba mkuu,
Mpaka sasa kwa muundo huu ni ghalama zaidi kuliko serikali tatu,
Hebu fikilia watu wanaamua tuu kuweka wizara kibao na wakuu wa wilaya weeengi, ndo maana sometimes hata kama mimi ni mwanaccm nawakubali sana CDM, kuna watu wanafikiria sana kuliko sisi wa ccm wakuu lazima tukubali!
 
Hakuna gharama, mawaziri kama Ngeleja (Nishati na Madini) ni waziri wa Tanganyika, hatutaongeza mwingine, yule sio waziri wa Jamhuri ya Muungano NK. Usicheke lakini.:bange:
 
Hakuna gharama, mawaziri kama Ngeleja (Nishati na Madini) ni waziri wa Tanganyika, hatutaongeza mwingine, yule sio waziri wa Jamhuri ya Muungano NK. Usicheke lakini.:bange:

Mkuu ngereja???
kunawizara hazitakuwepo kabisa kwenye serikali ya tanganyika badala yake itakuwa wizara ya muungano, hapo ndo tunaweza tukapeana uraisi wa kubadilishana ila kwa sasa sikubali kabisaa!
 
Watu kama nyie mko wachache, mnaelewa mambo haya vizuri. Wengine wamekazania gharama tu. Je gharama za kukosa Tanganyika?
 
Hivi ukienda kwenye tume ya katiba, halafu ukawaambia unataka serikali ya Tanganyika irudi hawatakukamata? Nataka niende huko.
 
Zanzibar ni dola kamili na mihimili yake yote mitatu, Mahakama, Serikali na Bunge. Hivi wao sasa wanalalama nini, bara ndio waliokuwa hawana kitu. Nafikiri Zanzibar wangeshughulikia serikali ya Tanganyika, Badala ya kuzungumzia kuvunja muungano.
 
Back
Top Bottom