citizensindevelopment18
JF-Expert Member
- Apr 1, 2020
- 1,548
- 755
Anayesimamia, kuhesabu na kutoa matokeo ni yule yule na mpenda madaraka oh tumeliwa. Matokeo .watakuwa 80%Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama cha ACT-Wazalendo Zanzibar, Salum Bimani, amesema viongozi wa chama hicho wanafanya vikao na Wanachama wake katika majimbo ya Unguja na Pemba kufikia uamuzi wa endapo kishiriki kwenye Serikali ya Umoja.
“Chama bado kinaendelea na vikao vyake kuhusu msimamo wake wa kuingia katika serikali au laa.” alisema.
Bimani aliyasema hayo, huku taarifa za zisizo rasmi zikieleza kwamba mchakato huo umekamilika na kazi kubwa inayofanyika hivi sasa ni kufanya uchambuzi wa maoni ya wanachama na kuangalia faida za kuingia katika serikali hiyo na hasara zake.