Kura ya kutokuwa na imani ya kumuondoa Rais J Zuma kusubiri uamuzi wa Mahakama:

helu

Member
Feb 28, 2015
86
124
Chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance (DA) cha Afrika ya Kusini kiliwasilisha bungeni maombi ya kuitishwa kwa bunge la dharura ili kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma.

DA waliwasilisha rasmi maombi yao mbele ya Spika Baleta Mbeke, ambapo ikapangwa kuitishwa bunge la dharura juzi Aprili 18 2017, ili kujadili hoja hiyo na kupigwa kura ya kutokuwa na imani na Rais Zuma.

Hata hivyo ilielezwa bungeni kuwa upigaji kura huo utafanywa kwa wazi kama ilivyotokea Tanzania wakati wa upitishwaji wa rasimu ya katiba mpya. Jinamizi hilo sasa limeingia katika Bunge la Afrika Kusini.

Wapinzani hawakubaliani na utaratibu wa kupiga kura za wazi kwani wanaamini kuwa hali hiyo itawafanya baadhi ya wabunge toka chama tawala (ANC) kushindwa kupiga kura ya kumuondoa Zuma kutokana na kuogopa kuadhibiwa na chama. Inaaminika kuwa wapo wabunge wengi wa ANC wangependa Zuma aondoke, lakini upigaji kura za wazi ni kikwazo kwao.

Chama cha United Democratic Movement (UDM) kwa niaba ya vyama vingine, kimeamua kufungua kesi mahakamani ya kikatiba kikiitaka mahakama kulilazimisha Bunge kukubali upigaji kura wa siri na sio wa wazi.


Kesi hiyo sasa imeifanya DA kumuomba Spika aahirishe kwa muda Bunge maalumu la ‘kumng’oa Zuma’ hadi mwezi Mei ili kusubiri uamuzi wa Mahakama ya Katiba. Spika ameridhia hilo na sasa kikao kilichokuwa kifanyike juzi kimesogezwa mbele hadi Mei katika tarehe itakayotajwa baadaye.

A. Kusini waaandamana kumtaka Zuma kuondoka Madarakani:

 
Back
Top Bottom