Kura ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu ni kura dhidi ya Rais na Chama tawala!

Bunge haliwezi kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais; hakuna mfumo huo. Linaweza kumshtaki Rais kibunge (impeachment).
Ni lugha tu za kisheria Mwanakijiji. Hatma ya wote wawili ni kuondoka/ kuondolewa madarakani. Si unajua wanasheria wanavyopenda kupamba lugha yao ili angalau kuonyesha tofauti za watu hao wawili. Nafasi ya WAZIRI MKUU wetu imekuwa pambo kupita kiasi. WM wetu ni kama kiranja mkuu wa shule ambaye hawezi kumwadhibu kiranja mwingine halafu tunamtwisha zigo la hawa wateule wabovu wa Rais. Bunge liwe wazi.
 
mbona kama vile zitto anamrekodi waziri anaye talajiwa kujiuzulu?
Amrekodi nani? Pinda? Pinda si ndo baba wa kazi hiyo ya kutafuta na kusambaza habari hata zile mnazoona ni siri kabisa. Kikubwa ametuletea mkoa mpya unaitwa Katavi. Mwenye wivu ajinyonge.
 
Mzee Mwanakijiji, JK hana ubavu wa kuyafanya yote hayo. anajua watu hawana imani nae. na anajua watu hawana imani na CCM. na anajua ikipigwa kura huru bungeni serikali yake itaporomoshwa na wabunge wengi. na anajua wabunge wake wengi watahamia CDM kwenye uchaguzi ujao. na anajua CDM kitashinda uchaguzi huo kwa kishindo cha kweli. na anajua CDM wakiingia madarakani, protections walizonazo mafisadi na wezi wa mali za umma zitayeyuka. na anajua ataishia jela na kufilisiwa...na anajua hataki yote hayo yamtokee...na anajua hatokubali hayo yamtokee kwa hiari yake mwenyewe au kwa njia yoyote laini 'ya kidemokrasia'. kwa hiyo, ni mpambano tu, aidha wa kisanii au kinamna yoyote ile, ili mradi status quo kama ilivyo leo iendelee kubaki...labda, inshallah, kesho italeta ahueni...si unajua upepo wa leo ukipita umepita?
 
Mzee Mwanakijiji, JK hana ubavu wa kuyafanya yote hayo. anajua watu hawana imani nae. na anajua watu hawana imani na CCM. na anajua ikipigwa kura huru bungeni serikali yake itaporomoshwa na wabunge wengi. na anajua wabunge wake wengi watahamia CDM kwenye uchaguzi ujao. na anajua CDM kitashinda uchaguzi huo kwa kishindo cha kweli. na anajua CDM wakiingia madarakani, protections walizonazo mafisadi na wezi wa mali za umma zitayeyuka. na anajua ataishia jela na kufilisiwa...na anajua hataki yote hayo yamtokee...na anajua hatokubali hayo yamtokee kwa hiari yake mwenyewe au kwa njia yoyote laini 'ya kidemokrasia'. kwa hiyo, ni mpambano tu, aidha wa kisanii au kinamna yoyote ile, ili mradi status quo kama ilivyo leo iendelee kubaki...labda, inshallah, kesho italeta ahueni...si unajua upepo wa leo ukipita umepita?

Hoja ni kwamba kutaka kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kunapaswa kuwa na matokeo yake. Ni jambo moja kudai Waziri Mkuu au Waziri fulani ajiuzulu lakini ni jambo jingine kutaka kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ipigwe. Kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais na serikali yake. Hili lazima lieleweke.
 
Mwanakijiji hebu nisaidie, hivi sisi tunafuata kweli Westminster System? Hebu angalia sifa za hii system uone kama kweli tunaifuata au tuna mfumo mwingine.

Key characteristics of Westminster systemImportant features of the Westminster system include the following, although not all of the following aspects have been preserved in every Westminster-derived system:[SUP][citation needed][/SUP]


Source: Wikipedia
 
Mwanakijiji hebu nisaidie, hivi sisi tunafuata kweli Westminster System? Hebu angalia sifa za hii system uone kama kweli tunaifuata au tuna mfumo mwingine.

Technically, tunafuata westminister system lakini siyo yote kamili na sehemu ambayo hatuifuati vizuri ni Madaraka ya Waziri Mkuu. Binafsi naamini hata kesho tukitaka Waziri Mkuu anaweza kuwa ni mtendaji na "Head of Government" na hivyo kuunda hata baraza la mawaziri. Lakini tumejichanganya mno hadi haiingii akilini!
 
Mzee Mwanakijiji asante kwa hili darasa. Nimekusoma ila nakumbuka zamani niliwahi kusoma mahali bunge linaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais kwa ku initiate imperchment process. Nitafanya rejea na kurejea.
 
Mzee Mwanakijiji Maelezo yako mazuri mwanzoni lakini naona baadaye unajichanganya. Mfumo wa westminster Mkuu wa nchi ni Malkia. Kama David Cameroon akijiuzuru au kupigwa chini kwa kura ya kutokuwa na imani Malkia huwa hapotezi mamlaka yake. Ndyo maana kwenye katiba yetu tumeweka kipengere hicho ambacho bunge laweza kumpigia Waziri Mkuu kura ya kutokuwa na imani naye akaondoka bila kuathiri mamlaka ya mkuu wanchi. Nadhani ni balance nzuri ku-enforce uwajibikaji bila kuathiri mfumo mzima wa utawala. Hizo derivation unazozifanya ni more of a phylosophy than legal. Unatafsiri vibaya tu hivyo vipengere.
 
Mzee Mwanakijiji asante kwa hili darasa. Nimekusoma ila nakumbuka zamani niliwahi kusoma mahali bunge linaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais kwa ku initiate imperchment process. Nitafanya rejea na kurejea.


Inawezekana; angalia hasa mabadiliko ya Katiba ya 2005 yaliongeza nini; kwa sababu kwenye mabadiliko yale ofisi ya waziri mkuu ilipandishwa juu zaidi ya Spika na Jaji Mkuu sasa inawezekana mambo fulani yalikuwa yanafanyika kabla
 
Mzee Mwanakijiji Maelezo yako mazuri mwanzoni lakini naona baadaye unajichanganya. Mfumo wa westminster Mkuu wa nchi ni Malkia. Kama David Cameroon akijiuzuru au kupigwa chini kwa kura ya kutokuwa na imani Malkia huwa hapotezi mamlaka yake. Ndyo maana kwenye katiba yetu tumeweka kipengere hicho ambacho bunge laweza kumpigia Waziri Mkuu kura ya kutokuwa na imani naye akaondoka bila kuathiri mamlaka ya mkuu wanchi. Nadhani ni balance nzuri ku-enforce uwajibikaji bila kuathiri mfumo mzima wa utawala. Hizo derivation unazozifanya ni more of a phylosophy than legal. Unatafsiri vibaya tu hivyo vipengere.

Siyo mimi niliyechanganya ni magenius wetu; Waziri Mkuu wa Uingereza akipigiwa kura ya kutoukwa na imani anajiuzulu pamoja na baraza lake kwa sababu yeye ndiye aliyeliunda halikuundwa na Malkia ambaye ndiye mkuu wa nchi. Sasa Waziri Mkuu wa Tanzania anapojiuzulu na baraza linavunjika kwanini wakati siyo aliyeliunda limeundwa na mkuu wa nchi?
 
Siyo mimi niliyechanganya ni magenius wetu; Waziri Mkuu wa Uingereza akipigiwa kura ya kutoukwa na imani anajiuzulu pamoja na baraza lake kwa sababu yeye ndiye aliyeliunda halikuundwa na Malkia ambaye ndiye mkuu wa nchi. Sasa Waziri Mkuu wa Tanzania anapojiuzulu na baraza linavunjika kwanini wakati siyo aliyeliunda limeundwa na mkuu wa nchi?

UK waziri mkuu in theory anapochaguliwa huenda kwa Malkia kuomba kuunda baraza la mawaziri na serikali na lazima apate ridhaa ya Malkia, Malkia akigoma basi uchaguzi hurudiwa. Vilevile kama watu wa chama chake hawamkubali na kumg'oa inabidi ajiuzulu kama ilivyomtokea Margereth Thatcher au Mbeki Afrika Kusini, hawakushindwa kwenye popular vote bali ni vyama vyao viliwawekea ngumu.

Hapa kwetu obviously hatuna mfalme au malkia tuna Rais ambaye ndio head of state na amiri jeshi mkuu, kikatiba Tanzania Rais anateua baraza la mawaziri kutoka kwa wabunge waliochaguliwa na wananchi au aliowateua kwa kushauriana na waziri mkuu, ndio maana kama WM akijiuzulu ni lazima rais avunje baraza la mawaziri sababu lazima WM aafike hilo baraza.

Kutokuwa na imani na rais na procedure za impeachment hata kwetu zipo hila ni lazima zipitishwe na 2/3 ya bunge ambayo ni ndoto kwa sasa ndio maana Zitto akaamua kwenda kwenye njia ya kutokua na imani na WM maana kama akijiuzulu hiyo itatrigger rais ateue baraza jipya.

Vilevile sidhani kama Tz tunaweza kumtoa rais midterm kama South Africa au UK kwa kupitia chama tawala, hivo JK tunae tu mpaka 2015!!!

Cha msingi ni kitu rahisi tusiwapigie kura CCM come 2015!! Lakini kwa vile nchi yetu ni wengi wape kama watu wengi wakikubali laghai ya sera za CCM na kuwapa kura nyingi zaidi ya vyama vya upinzani, well then there is not much we can do....Yetu macho
 
UK waziri mkuu in theory anapochaguliwa huenda kwa Malkia kuomba kuunda baraza la mawaziri na serikali na lazima apate ridhaa ya Malkia, Malkia akigoma basi uchaguzi hurudiwa. Vilevile kama watu wa chama chake hawamkubali na kumg'oa inabidi ajiuzulu kama ilivyomtokea Margereth Thatcher au Mbeki Afrika Kusini, hawakushindwa kwenye popular vote bali ni vyama vyao viliwawekea ngumu.

Hapa kwetu obviously hatuna mfalme au malkia tuna Rais ambaye ndio head of state na amiri jeshi mkuu, kikatiba Tanzania Rais anateua baraza la mawaziri kutoka kwa wabunge waliochaguliwa na wananchi au aliowateua kwa kushauriana na waziri mkuu, ndio maana kama WM akijiuzulu ni lazima rais avunje baraza la mawaziri sababu lazima WM aafike hilo baraza.

Kutokuwa na imani na rais na procedure za impeachment hata kwetu zipo hila ni lazima zipitishwe na 2/3 ya bunge ambayo ni ndoto kwa sasa ndio maana Zitto akaamua kwenda kwenye njia ya kutokua na imani na WM maana kama akijiuzulu hiyo itatrigger rais ateue baraza jipya.

Vilevile sidhani kama Tz tunaweza kumtoa rais midterm kama South Africa au UK kwa kupitia chama tawala, hivo JK tunae tu mpaka 2015!!!

Cha msingi ni kitu rahisi tusiwapigie kura CCM come 2015!! Lakini kwa vile nchi yetu ni wengi wape kama watu wengi wakikubali laghai ya sera za CCM na kuwapa kura nyingi zaidi ya vyama vya upinzani, well then there is not much we can do....Yetu macho

Inawezeknaa technically, kuwa na mid-term election..
 
"Hata hivyo, naamini pia kwa rais kukubali hili ni LAZIMA AWEKE WAZI kwa Wabunge wote kuwa Kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni kura ya kutokuwa na imani na serikali yake na ni kura ya kutokuwa imani na yeye na kuwa yuko tayari kabisa wabunge wawe uhuru kabisa katika kura ya SIRI kupiga kura hiyo na kuwa endapo wabunge hawana Imani na Waziri Mkuu na wakaonesha hivyo kwa kura basi Waziri Mkuu ataondolewa lakini siyo hapo tu na yeyemwenyewe atajiuzulu na kuvunja Bunge ili nchi ianze upya. Ikumbukwe huwezi kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu lakini ukataka kubakia ama na Rais au na Bunge."

Mkuu Mwanakijiji,

nimekuelewa, na asante kwa makala yako yenye ufafanuzi murua. Lakini kuna haja gani ya rais kuwafafanulia wabunge au kuwa wazi kwa wabunge kama ulivyoelezea hapo juu? Ikiwa muongozo upo kwenye katiba, huoni kama kumshauri hivyo kunampa nafasi ya kuchakachua maamuzi yao (wabunge) ambayo wamakwishaamua kuyafanya siku kadhaa nyuma, na kwamba ni namna mpya ya kuomba huruma? Ninadhani asiwaambie chochote kama ambavyo hajasema chochote hadi sasa...Kura zipigwe na kila mtu akubali matokeo.

Labda makala yako itamsaidia yeye kuelewa mapana ya kura ya kutokuwa na imani na PM.

Kuna kitu kimoja tunatakiwa kuelewa. Mbali na mbunge kuwa na wajibu wa kukiunga mkono chama, lakini nawajibu zaidi wa kuwajibika kwa wapiga kura wake (hata kama ni kinyume na chama chake), na vilevile nawajibika kwa dhamira yake (hata kama uamuzi anaoona ni sahihi unakiumiza chama chake).

Utaratibu wa kupiga kura ya kutokuwa na imani dhi ya rais una tofauti na ule wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu. Tunatakiwa kujua kuwa pamoja na madudu yote ya Mh Pinda, yeye ni tofauti sana na JK. At least amejaribu hata kujiuzulu, naamini kuwa anajua anawajibika kutokana na utendaji wa mawaziri waliochini yake, pamoja na kuwa si yeye aliyewateua.

tatizo ni kuwa pamoja na kuwa tunafahamu serikali yote haiaminiki, mechanisim na repercussions za vote of no confidence dhidi ya Rais, na ile dhidi ya PM ni tofauti sana.Ni better kumuacha Lowassa aumane na Pinda kuliko kumuacha aumane na JK.
 
  • Thanks
Reactions: DSN


Binafsi naweza kusema kwamba, nikiangalia kiufundi naweza kusema kuwa kama kuna sababu kubwa na ya msingi ya kuvunja baraza la mawaziri siyo shinikizo la wanasiasa, wananchi au watu wengine bali KUSHINDWA KUWAJIBIKA kwa pamoja. Kwenye serikali kuna nadharia ya
"collective responsibility" kwamba mawaziri wote wanafanya kazi kwa pamoja kwa ridhaa ya Rais.....................

Nadhani ni makosa kufikiria kuwa kura hii ni dhidi ya Pinda kama Waziri Mkuu; mtazamo huu siyo sahihi. Pinda ni Waziri Mkuu wa Serikali iliyoko madarakani. Yeye kama Waziri anafanya kazi kwa mujibu wa Katiba lakini akitekeleza majukumu yake chini ya Rais. Bahati mbaya sana Waziri Mkuu wetu siyo mtendaji (a non-executive Prime Minister) yaani siyo anayeunda serikali. Waziri Mkuu wetu japo anapitishwa na Bunge hawajibiki kwa Bunge moja kwa moja! Ibara ya 53:1 ya Katiba iko wazi katika hili "Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mkuu atawajibika kwa Rais kuhusu utekelezaji wa madaraka yake." Hii ina maana ya kwamba, Waziri Mkuu akiboronga kama yeye chombo cha kumwajibisha ni kilichomteua yaani Rais!


Hakuna mabadiliko nusu! Tumeamua kuvua nguo, tuyaoge.


Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com

MMM kwa mujibu wa katiba yetu bila kuweka nadharia kitendo cha Zitto kinatosheleza kabisa kumhukumu waziri mkuu pasipo kumgusa Rais.Tufike sehemu tuitumikie katiba yetu hii kama ilivyo.Kwa hili "Nadhani ni makosa kufikiria kuwa kura hii ni dhidi ya Pinda kama Waziri Mkuu; mtazamo huu siyo sahihi." kwa kweli MMM mimi siko pamoja nawe kwa kuwa KATIBA ambayo ni sheria mama inasema nini kwa Bunge kupitisha azimio la kumuondoa Rais Madarakani...

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO ATAPIGIWA KURA YA AZIMIO LA KUTAKUWA NA IMANI NAE KWA SHERIA HIZI

Bunge laweza kumshtaki Rais Sheria ya 1992 Na.20 ib.8 Sheria ya 1995 Na.12 ib.4


46A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii,
Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.

(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama
inadaiwa kwamba Rais-Sheria ya ….
(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba, au
(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.

(3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tu kama-
(a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya
Wabunge wote itawasilishwa kwa Spika siku thelathini kabla ya kikao ambapo hoja hiyo inakusudiwa kutolewa Bungeni, ikifafanua makosa aliyoyatenda Rais, na ikipendekezwa kuwa Kamati Maalum ya Uchunguzi iundwe ili ichunguze
mashataka yaliyowasilishwa dhidi ya Rais;
(b) wakati wowote baada ya Spika kupokea taarifa iliyotiwa sahihi na Wabunge na kujiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja kuiwasilisha hoja hiyo, na kisha Spika atalitaka
Bunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu ya hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi na kama ikiungwa mkono na Wabunge waiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote atatangaza majina ya wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi.

(4) Kamati Maalum ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya ibara hii, itakuwa na wajumbe wafuatao, yaani-
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati;
(b) Jaji Mkuu wa Tanzania Zanzibar na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(c) Wajumbe saba walioteuliwa na Spika kwa mujibu wa Kanuni za Bunge na kwa kuzingatia uwiano wa uwakilishi baina ya vyama vya siasa vinavyowakilishwa Bungeni.

(5) Endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi, Rais atahesabiwa kuwa hayupo kazini, kisha kazi na madaraka ya Rais yatatekelezwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(3) ya Katiba hii hadi Spika atakapomfahamisha Rais juu ya azimio la Bunge kuhusiana na mashataka yaliyotolewa dhidi yake.

(6) Ndani ya siku saba baada ya Kamati Maalum ya Uchuguzi kuundwa, itakaa ichunguze na kuchambua mashataka dhidi ya Rais, pamoja na kumpatia Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.

(7) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika muda usiozidi siku tisini, Kamati Maalum ya Uchunguzi itatoa taarifa yake kwa Spika.

(8) Baada ya Spika kupokea taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi, taarifa hiyo itawasilishwa Bungeni kwa kufuata
utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.

(9) Baada ya taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi kuwasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (8), Bunge litaijadili
taarifa hiyo na litampa Rais fursa ya kujieleza, na kisha, kwa kura za Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote, Bunge litapitisha azimio ama kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika, na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, au kuwa mashtaka hayo hayakuthibitika.

(10) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bunge lilipopitisha azimio hilo.

(11) Endapo Rais ataacha kushika kiti cha Rais kutokana na mashataka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupata malipo yoyote ya pensheni wala kupata haki au nafuu nyinginezo alizo nazo kwa mujibu wa Katiba au Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge.

WAZIRI MKUU ATAAZIMIWA KWA KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NAE KUPITIA BUNGE KWA SHERIA HIZI:
Kura ya kutokuwa na imani. Sheria ya 1992 Na.20 ibara 10 Sheria ya 1995 Na.12 ibara 7

53A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 51 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu endapo itatolewa hoja kupendekeza hivyo na ikapitishwa kwa mujibuwa wa masharti ya ibara hii.

(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kutaka kupitisha kura ya kutokuwa na imani na Waziri
Mkuu haitatolewa Bungeni endapo-

(a) haina uhusiano na utekelezaji wa majukumu ya Waziri Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 52 ya Katiba hii, wala
hakuna madai kwamba Waziri Mkuu amevunja Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

(b) haijapita miezi sita tangu alipoteuliwa;
(c) haijapita miezi tisa tangu hoja ya namna hiyo ilipotolewa Bungeni na Bunge likakataa kuipitisha.

(3) Hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitapitishwa na Bunge isipokuwa tu kama-
(a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya Wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku angalau kumi na nne kabla ya siku inapokusudiwa kuwasilishwa Bungeni;
(b) Spika atajiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja yametimizwa.

(4) Hoja iliyotimiza masharti ya ibara hii itawasilishwa Bungeni mapema iwezekanavyo kwa mujibu wa Kanuni za Bunge.

(5) Hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu itapitishwa tu iwapo inaungwa mkono na Wabunge walio wengi.

(6) Endapo hoja ya kura ya kutokuwa na imani kwa Waziri Mkuu itaungwa mkono na Wabunge wengi, Spika atawasilisha
azimio hilo kwa Rais, na mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku mbili tangu Bunge lilipopitisha azimio la hoja ya kura ya kutokuwa na imani kwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuu atatakiwa ajiuzulu, na Rais atamteua Mbunge mwingine kuwa Waziri Mkuu.

Mkuu nakuaminia sana kwa mavitu ambayo uwa tunajifunza wengine kupitia kwako,lakini kwa hili ebu liache lifanyiwe kazi kama KATIBA inavyosema.Nakubaliana nawe na tulishwaikujadilina nawe humu walati wa sakata la mgomo wa Madaktari kuwa kisheria WAZIRI MKUU anaonekana anamamlaka na kuwajibika Bungeni lakini likija kiutekelezaji anaonekana KUPWAYA kiasi kuwa nakumbuka kusema kuwa kauri ya Waziri Mkuu Pinda na swala la Jairo bungeni,wakati anatoa taarifa ya Serikali juu ya sakata hilo kuwa "namsubilia Rais atue ili atoe majawabu ya swala la Jairo".Tofauti na kuwa alipaswa kuamua na kusubilia Rais akija Ikulu akutane na mafairi ya maaamuzi ya ofisi ya waziri mkuu akimfahamisha jinsi alivyoamua kwa niaba ya Serikali na sio Jinsi gani Rais ahamue kwa niaba ya Waziri Mkuu Pinda ambae tayari KATIBA ya Nchi na Rais wamesha mpaka mamlaka ya kuamua.

Kwa swala zima la mchezo huu ni kusema basi haina maana kwa KATIBA na RAIS kudelagate na kuvest Power kwake kama Waziri Mkuu kama hawezi kuamua kwa niaba ya Serikali!!!

Acha aumie ili kesho na keshokutwa wengine wajifunze kuitumikia Katiba hata kama ni kumkosea MKUBWA WAKO [RAIS] kama HAPENDEZWI na MAAMUZI YAKO lakini umeamua kwa kuzingatia SHERIA ZA NCHI na Sheria MAMA KATIBA YA NCHI.Na ukiona Mkuu wako hakubalina na maamuzi yako ambayo dhahili unajua kuwa huko sahihi na umezingatia katiba,jiuzuru [Resign=quit] ili walioko pembeni wapime uzito wa maamuzi yako dhidi ya mkuu wako.

Naomba kusaidiwa tafsiri ya maneno haya kwa kiswahili uenda kwa lugha ya wenzetu yana maana tofauti.
1: Deligate= Appoint =Representive
If you are delegated to do something, you are given the duty of acting on someone else's behalf by making decisions, voting, or doing some particular work.

A delegate is a person who is chosen to vote or make decisions on behalf of a group of other people, especially at a conference or a meeting.

2: Vest
If something is vested in you, or if you are vested with it, it is given to you as a right or responsibility.

Mkuu nakuheshimu sana lakini kwa hili nisamehe wakuu hawa wamekuwa na tabia mbaya sana sana ya kufanya kazi kwa mazoea HOFU,MASHAKA,Kama ujui Serikalini watu wazima wengi wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea ya kale katabia ka OBEY YOUR SUPERIOR.Yani mfumo huo umedumaza watendaji wengi sana kiasi kuwa ofisi unakuta mtu anamamlaka lakini hawezi kuamua kwa niaba ya mamlaka au madaraka aliyonayo mkononi kwa vigezo vya kusubilia bosi wake juu yake aje kuamua...

Nakumbuka katika thread ile ulisema kuwa Pinda itabidi abebe mzigo huo kwa kuwa wajibu na dhamana vinaenda pamoja.Lakini Ukweli watawala wetu wengi wanapenda madadraka =dhamana lakini hawapendi wajibu wa dhamana hiyo Yani Authority should go together with Responsibility!!

Japo najua Katiba yetu inamapungufu lakini kwa hili la Zitto na wabunge72 liko wazi sana!!Wakati mwingine hatujui labda JK nae yanamsibu haya haya kuwa watu hawataki Responsibility kwa kuwa watakuwa Responsible na matokeo ya maamuzi yao!!Wao waendelee kula na kunywa na kelele za vingola barabarani huku WANATEGA KUBEBA LAWAMA KWA MAAMUZI OVYO/MAZURI kwa kuwa yatategema majibu ya mwitikio wa UMMA JUU YA TUKIO HUSIKA.

Mkuu mfano huko wazi umeona issue ya Pinda na Kikwete na Madaktari!!!
 
MWANAKIJIJI makala yako iko kama umeme wa TANZANIA, iko on point, then off point, then on point, then off point. Tafsiri yako ya Katiba is more political than legal, more activism like than real: in a word 'contradicting', incapable of construction. WELL SASA naangalia baadhi tu ya mikanganyiko yako, unasema "...
Sasa dhana hii ya kuwajibika kwa pamoja kwa baraza la mawaziri kimsingi inaenda sambamba na hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu (serikali). Kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu siyo kura dhidi ya mtu binafsi! Ni kura dhidi ya serikali na inapopigwa serikali nzima lazima ivunjwe na siyo tu kuvunjwa lakini serikali nzima inatakiwa kujiuzulu na kuitisha uchaguzi mpya. Wikipedia inaelezea hili hivi (kwa sisi tunaofuata mfumo wa Westminster) "if a vote of no confidence is passed in parliament, the government is responsible collectively, and thus the entire government resigns. The consequence will be that a new government will be formed, or parliament will dissolve and a general election will be called" Huwezi kuwa na kura ya kutokuwa na imani na serikali na Rais akabakia! Huwezi kuwa na kura ya kutokuwa na imani na serikali na Bunge likabakia! If one falls, the other must follow!"

Na una UNAONGEZA ..."
Mmoja akiondolewa na mwingine ni lazima afuate ndio maana rais anapokufa au kuacha urais kwa sababu zilizoanishwa Kikatiba Waziri mkuu naye anapoteza nafasi yake na baraza la mawaziri linavunjika! Ni sauti na mwangwi! Chini ya Ibara ya 36 Rais ndiye ana uamuzi wa mwisho wa nani anatumikia serikali hii kwani ana uwezo wa kumfukuza mtu yeyote kwenye utumishi wa umma. Siyo Waziri Mkuu."

KUKOLEZA UNAKAZIA KUWA '...Lakini huwezi pia kunyoshea kidole Waziri Mkuu na rais bila kunyoshea kidole chama cha Waziri Mkuu na Rais. Ikumbukwe kuwa Rais wa Tanzania anachaguliwa na wananchi lakini sharti la msingi chini ya Ibara ya 39:1c. Ibara hiyo inasema mojawapo ya sifa za mtu kuwa Rais ni kuwa ni lazima awe "ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa".'


WITH DUE RESPECT, either (1) kwa kutokuja au (2) kwa makusudi umeenda kinyume kabisa na dhana ya Bunge (nikimaanisha NATIONAL ASSEMBLY, AS) kupiga kura ya kutokuwa na imani na PM na mamlaka ya RAIS. TAFSIRI YAKO ULIYOTOA ni ya uncodified constitution ya WAINGEREZA siyo ya TZ KATIBA ya 1977: LEGALLY a vote of no confidence in the PM DOES NOT touch the PRES, rather, it is for the PM and the Ministers. More the VOTE does NOT touch the THE CABINET, if, it were to result in the resignation of the CABINET the PRES too would be in trouble: but that is not the case. Kura ya kutokuwa na imani na PM haivunji SERIKALI NA KUITISHWA UCHAGUZI MPYA, kwa TZ. UCHAGUZI mpya MKUU unaitishwa baada ya BUNGE (hapa ni PARLIAMENT siyo NA) kwa mujibu wa IBARA YA 90 (2) [SOMA kwa wakati wako, na hapo hakuna suala la VOTE of NO confidence in the PM].

JINGINE siyo kweli kwamba "... Chini ya Ibara ya 36 Rais ndiye ana uamuzi wa mwisho wa nani anatumikia serikali hii kwani ana uwezo wa kumfukuza mtu yeyote kwenye utumishi wa umma..." . Kwa nini? WATUMISHI wa UMMA Tanzania DO NOT SERVE HIS EXCELLENCY THE PRESIDENT, tofautisha na WAINGIREZA ambao watumishi wa serikali ni ROYAL SERVANTS, they serve at the pleasure of HER MAJESTY THE QUEEN. TZ ni constitutional republic, where sovereignty lies in the constitution. Hii ina maana gani? RAIS anaweza kufuta vyeo (SIYO KUFUKUZA KAZI) vya watumishi aliowateua (yaani those whose duty posts are by PRESIDENTIAL APPOINTMENTS, they serve at HIS pleasure). LAKINI hao aliowafuta vyeo wataendelea kutumikia nafasi zao za ajira yaani SUBSTANTIVE POSTS: ninamaanisha kuwa kama mimi ni MWL na cheo changu ni PRINCIPAL EDUCATION OFFICER, MUNGU si ATHUMAN, RAIS akaniteua kuwa Katibu MKUU WIZARA YA ELIMU, alafu nikaboronga; MAMLAKA YA RAIS ni kuniondoa kwenye UKATIBU MKUU lakini hana mamlaka ya kufuta u PRINC EDUC OFFICER wangu, huo unafutwa na mamlaka yangu ya nidhamu ambayo si RAIS. KWA HIYO RAIS WA TZ HANA MAMLAKA ya kumfukuza mtu yeyote anayotaka kutoka kwenye utumishi wa umma.

NINAKUBALIANA na wewe KATIKA hili, kwa mtu wa kuwajibisha ni RAIS. Kwa nini? KATIBA YETU inajichangana sana. RAIS anahusika na SERA (IBARA 53) na PM anahusika na utekelezaji wa sera hizo (IBARA 52). LAKINI PM hana mamlaka ya kusimamia utekelezaji, mamlaka yako mikononi mwa RAIS (IBARA 36, 37 NK). SASA SERIKALI ikishindwa, nani kashindwa ni PM au ni RAIS? DEFINATELY ni RAIS, HUYU ndiye wa kula nae sahani moja. TUTAENDELEA KUJADILIANA ...




Binafsi naweza kusema kwamba, nikiangalia kiufundi naweza kusema kuwa kama kuna sababu kubwa na ya msingi ya kuvunja baraza la mawaziri siyo shinikizo la wanasiasa, wananchi au watu wengine bali KUSHINDWA KUWAJIBIKA kwa pamoja. Kwenye serikali kuna nadharia ya "collective responsibility" kwamba mawaziri wote wanafanya kazi kwa pamoja kwa ridhaa ya Rais.

Ikumbukwe kuwa katika nchi yetu chombo kikuu cha kumshauri rais juu ya utendaji wa mambo mbalimbali ya serikali na majukumu yake siyo Bunge, au vyama vya siasa bali ni Baraza la Mawaziri. Katiba yetu inaliweka hili wazi kwa maneno yafuatayo Ibara ya 54:3 "Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara ya 37(1) ya Katiba hii, Baraza la Mawaziri litakuwa ndicho chombo kikuu cha kumshauri Rais juu ya mambo yote yanayohusika na utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, na litamsaidia na kumshauri Rais juu ya jambo lolote litakalowasilishwa kwenye Baraza hilo kwa mujibu wa maagizo maalum au maagizo ya jumla yatakayotolewa na Rais."

Na kutokana na uzito huu - kwamba ndicho chombo cha kuaminiwa na rais kumpa ushauri - katiba inaweka kinga kamili (absolute immunity) kwa baraza hilo linapotoa ushauri kwa Rais. Inasemwa "Suala kama ushauri wowote, na ni ushauri gani, ulitolewa na Baraza la Mawaziri kwa Rais, halitachunguzwa katika mahakama yoyote." Kwa maneno mengine mawaziri wanaweza kutoa ushauri pasi ya hofu kuwa mambo waliyoshauri yanaweza kutumiwa dhidi yao mahakamani au hata kuchunguzwa!

Sasa dhana hii ya kuwajibika kwa pamoja kwa baraza la mawaziri kimsingi inaenda sambamba na hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu (serikali). Kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu siyo kura dhidi ya mtu binafsi! Ni kura dhidi ya serikali na inapopigwa serikali nzima lazima ivunjwe na siyo tu kuvunjwa lakini serikali nzima inatakiwa kujiuzulu na kuitisha uchaguzi mpya. Wikipedia inaelezea hili hivi (kwa sisi tunaofuata mfumo wa Westminster) "if a
vote of no confidence is passed in parliament, the government is responsible collectively, and thus the entire government resigns. The consequence will be that a new government will be formed, or parliament will dissolve and a general election will be called" Huwezi kuwa na kura ya kutokuwa na imani na serikali na Rais akabakia! Huwezi kuwa na kura ya kutokuwa na imani na serikali na Bunge likabakia! If one falls, the other must follow!

Nadhani ni makosa kufikiria kuwa kura hii ni dhidi ya Pinda kama Waziri Mkuu; mtazamo huu siyo sahihi. Pinda ni Waziri Mkuu wa Serikali iliyoko madarakani. Yeye kama Waziri anafanya kazi kwa mujibu wa Katiba lakini akitekeleza majukumu yake chini ya Rais. Bahati mbaya sana Waziri Mkuu wetu siyo mtendaji (a non-executive Prime Minister) yaani siyo anayeunda serikali. Waziri Mkuu wetu japo anapitishwa na Bunge hawajibiki kwa Bunge moja kwa moja! Ibara ya 53:1 ya Katiba iko wazi katika hili "Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mkuu atawajibika kwa Rais kuhusu utekelezaji wa madaraka yake." Hii ina maana ya kwamba, Waziri Mkuu akiboronga kama yeye chombo cha kumwajibisha ni kilichomteua yaani Rais!

Na kifungu kinachofuatia kinaiweka dhana hii ya "kuwajibika kwa pamoja" kwenye Katiba yetu. Kifungu hicho kinasema "Serikali ya Jamhuri ya Muungano, chini ya mamlaka ya Rais, ndiyo itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya sera ya Serikali kwa jumla, na Mawaziri, chini ya uongozi wa Waziri Mkuu, watawajibika kwa pamoja Bungeni kuhusu utekelezaji wa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano." Ni muhimu kutambua kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano mkuu wake siyo Waziri Mkuu! Waziri Mkuu ndiye "kiongozi wa shughuli za serikali Bungeni". Hata hivyo, katiba pia inampa madaraka Waziri ya kusimamia shughuli za kila siku za serikali kwenye ibara ya 52:1 ya Katiba yetu. Hata hivyo madaraka hayo yanafungwa na kifungu hicho cha 53:1

Ibara ya 33:2 ya Katiba yetu inasema hivi kuhusu madaraka ya rais kuwa "Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu." Ni vizuri kuona tofauti ya "kiongozi" inavyotumiwa kwa Waziri Mkuu na kwa rais. Waziri Mkuu nimeonesha anaitwa "kiongozi wa shughuli za serikali Bungeni" yaani "leader of Government business in the National Assembly" lakini rais ni "Head of Government". Hii ina maana gani basi?

Hii ina maana ya kwamba, kama serikali inapwaya, kama serikali haitekelezi kazi zake vizuri na kama inaonekana kuwa serikali imechafuliwa sana basi mtu sahihi na wa kwanza kulaumiwa ni Rais! Waziri Mkuu anaweza kulaumiwa kama kule bungeni mawaziri walikuwa wanagongana au walikuwa hawawajibiki kwa pamoja. Lakini kama ni suala la serikali nzima kuwa na matatizo basi mtu sahihi wa kubebeshwa lawama ni Mkuu wa Serikali (head of government) yaani rais.

Sasa, kwa vile serikali ni moja ni vigumu kutenganisha kuwajibika kwa Waziri Mkuu na kuwajibika kwa rais. Ikumbukwe ni Rais ndiye anayemteua Waziri Mkuu akiwa na uhuru kamili (absolute freedom) na hulipendekeza jina hilo kwa Bunge. Waziri Mkuu mkuu anasimamia utekelezaji wa serikali kwa niaba ya Rais. Sasa Katiba yetu haijaweka utaratibu wa kumpigia rais kura ya kutokuwa na imani lakini imeweka utaratibu dhidi ya Waziri Mkuu. Kwa msingi wa kuoanisha uhusiano ulipo kati yaWaziri Mkuu na Rais ni wazi kuwa kumpigia kura Waziri Mkuu ni kupigia kura serikali; na kuipigia serikali ni kumpigia kura Rais ambaye ndiye MKUU WA SERIKALI. Huwezi - narudia tena - kujipanga kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu halafu ukasema una imani na Rais! Huwezi kumnyoshea mkono Waziri Mkuu kuhusu utendaji mbovu wa seriakli bila wakati huo huo kumnyoshea mkono Rais ambaye ndiye aliyemteua Waziri Mkuu huyo lakini vilevile ndiye mkuu wa serikali hiyo.

Mmoja akiondolewa na mwingine ni lazima afuate ndio maana rais anapokufa au kuacha urais kwa sababu zilizoanishwa Kikatiba Waziri mkuu naye anapoteza nafasi yake na baraza la mawaziri linavunjika! Ni sauti na mwangwi! Chini ya Ibara ya 36 Rais ndiye anauamuzi wa mwisho wa nani anatumikia serikali hii kwani ana uwezo wa kumfukuza mtu yeyote kwenye utumishi wa umma. Siyo Waziri Mkuu.

Lakini huwezi pia kunyoshea kidole Waziri Mkuu na rais bila kunyoshea kidole chama cha Waziri Mkuu na Rais. Ikumbukwe kuwa Rais wa Tanzania anachaguliwa na wananchi lakini sharti la msingi chini ya Ibara ya 39:1c. Ibara hiyo inasema mojawapo ya sifa za mtu kuwa Rais ni kuwa ni lazima awe "ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa". Kimsingi Rais ni lazima atoke kwenye chama. Katika suala letu rais wetu anatokana na Chama cha Mapinduzi - ndiyo mwanachama wake na ndicho kilichompendekeza. Kuinyoshea mkono serikali ni kunyoshea mkono chama kilichounda serikali hiyo.

Lakini pia tuangalie kwa namna nyingine kidogo; Bunge linapomnyoshea mkono Waziri Mkuu ina maana linaonesha halina imani na serikali - ndio maana inaitwa kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu - na hivyo halina imani na Rais. Bunge linapokosa imani na Rais ambaye anamteua Waziri Mkuu lenyewe pia linajikuta matatani kwani Rais ni sehemu ya Bunge! Ibara ya 62:1 iko wazi kuhusu hili "Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo
litakuwa na sehemu mbili, yaani Rais na Wabunge" Hivyo, Bunge linaponyoshea kidole sehemu yake mojawapo - yaani rais - Bunge linajinyoshea lenyewe kidole; kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni kutokuwa na imani na Rais na kutokuwa na imani na rais ni kutokuwa na imani na sehemu ya bunge; Waziri Mkuu akilazimishwa kujiuzulu Rais naye ni LAZIMA ajiuzulu! Na Rais akijiuzulu Bunge lazima livunjwe! Wote wanawajibika kwa pamoja per excellence!

Lakini pia tunaweza kuliona hili vizuri - Waziri Mkuu anapendekezwa na rais, na anapitishwa na Bunge. Sasa Bunge linapomgeuka Rais, Bunge linageuka uamuzi wake lenyewe. Ikumbukwe kuwa Pinda alipendekezwa na Rais, jina lake likaletwa Bungeni, Wabunge wakaulizwa na kuunga mkono uteuzi huo wa rais na sasa wanataka kuukataa. Sasa, hawawezi kuukataa na wao wakabakia! Naomba niweke tofauti kidogo ambayo ningependa ieleweke. Ni vizuri sana kuweka shinikizo Waziri Mkuu ajiuzulu au mawaziri wajiuzulu. Wabunge wanaweza kuweka shinikizo hilo kwa kutumia Bunge. Lakini wanapokaa na kuwa tayari kupiga kura ya kutokuwa na imani wamevuka kutoka kwenye shinikizo kwenda kwenye suala la kisheria ambalo lina matokeo; kupiga kura ya kutokuwa na imani ni Waziri Mkuu ni kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali (Rais) na kutokuwa imani na Rais (ambaye ni sehemu ya Bunge) ni kujishtaki lenyewe!

Ni sawa sawa na mtu kunyoshea kidole mtu kwenye kioo na kumtishia kumkata kichwa kwa panga. Well, ukitaka kumkata mtu wa kwenye kioo weka panga shingoni mwake, ukimkata yeye na wewe hubakii! hivyo, naunga mkono kabisa kura ya kutokuwa na imani na serikali lakini kama nilivyosema kwenye mada nyingine naamini watu wengi hawajui kuwa huwezi kuwa na kura ya kutokuwa na imani nusu - yaani ukaishia kwa Waziri Mkuu. Ni LAZIMA ili liende moja kwa moja kwa Rais, na kwa Bunge.

Ni matumaini yangu - na maombi yangu -kuwa Spika Makinda atakubali hoja hii na kuitisha kikao cha Bunge cha dharura chini ya kifungu cha 27:4 cha Kanuni za Bunge kuwa "Endapo manufaa ya Taifa yatahitaji kuwa Bunge lisikutane tarehe ile iliyowekwa kwa Mkutano utakaofuata, bali likutane tarehe ya mbele zaidi au ya nyuma zaidi, basi Spika anaweza, baada ya kushauriana na Kamati ya Uongozi, kuliita Bunge likutane tarehe hiyo ya mbele zaidi au nyuma zaidi." Ninaamini kama matakwa ya Katiba yametimizwa (taarifa ya asilimia 20 ya wabunge kutaka hoja hiyo iletwe) basi Spika NI LAZIMA aitishe kikao maalum cha Bunge mapema zaidi.

Ni matumaini yangu vile vile kuwa Rais Kikwete hatovunja baraza la mawaziri sasa hivi au kufanya mabadiliko yoyote kwa sababu ya hoja ya kina Zitto kwa sababu mabadiliko hayo sasa YAMECHELEWA MNO kiasi cha kupoteza umaana. Sasa hivi hoja iliyopo mbele ya taifa ni kuwa wananchi hawana imani na serikali yao na Rais Kikwete hawezi kupata imani hiyo kwa kufanya mabadiliko isipokuwa kwa Waziri Mkuu wake kupigiwa kura hiyo. Hivyo, ninaamini kabisa kuwa rais akubaliane na Spika ili Bunge liitishwe mapema kabisa iwezekanavyo ili Serikali yake ijaribiwe na wawakilishi wa wananchi na awe tayari kwa matokeo yoyote yale.

Hata hivyo, naamini pia kwa rais kukubali hili ni LAZIMA AWEKE WAZI kwa Wabunge wote kuwa Kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni kura ya kutokuwa na imani na serikali yake na ni kura ya kutokuwa imani na yeye na kuwa yuko tayari kabisa wabunge wawe uhuru kabisa katika kura ya SIRI kupiga kura hiyo na kuwa endapo wabunge hawana Imani na Waziri Mkuu na wakaonesha hivyo kwa kura basi Waziri Mkuu ataondolewa lakini siyo hapo tu na yeyemwenyewe atajiuzulu na kuvunja Bunge ili nchi ianze upya. Ikumbukwe huwezi kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu lakini ukataka kubakia ama na Rais au na Bunge.

Hakuna mabadiliko nusu! Tumeamua kuvua nguo, tuyaoge.


Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
 
Inawezekana bunge likaitishwa, Kura ya siri ikapigwa, kura zinazounga mkono zikawa chache kuliko hata wale waliosaini petition. Mambo ya sayansi
 
MWANAKIJIJI makala yako iko kama umeme wa TANZANIA, iko on point, then off point, then on point, then off point. Tafsiri yako ya Katiba is more political than legal, more activism like than real: in a word 'contradicting', incapable of construction.

NINAKUBALIANA na wewe KATIKA hili, kwa mtu wa kuwajibisha ni RAIS. Kwa nini? KATIBA YETU inajichangana sana. RAIS anahusika na SERA (IBARA 53) na PM anahusika na utekelezaji wa sera hizo (IBARA 52). LAKINI PM hana mamlaka ya kusimamia utekelezaji, mamlaka yako mikononi mwa RAIS (IBARA 36, 37 NK). SASA SERIKALI ikishindwa, nani kashindwa ni PM au ni RAIS? DEFINATELY ni RAIS, HUYU ndiye wa kula nae sahani moja. TUTAENDELEA KUJADILIANA ...

Mkuu Nyamka naona na wewe pia umekuja na mchanganyiko usio na miguu wala kichwa kwa kuwa umeeenza vizuri umefika mwisho umevurunda kuliko hata dhana ambayo mwanakijiji alitaka kuijenga kwa kuwa najua kiu ya Mwanakijiji ni hicho kiti cha juu kihukumiwe kwa kuwa ndicho chenye jicho la mwisho la kuona yote haya,lakini nae pia anasahau kuwa kwa kiti hicho hicho cha uwziri mkuu wa Hayati Edward Sokoine kilitenda mambo mazito kwa mujibu wa nguvu/dhamana/wajibu husika ya Kisheria na Kikatiba aliyokuwa amepewa na Rais kwa mujibu ya katiba husika miaka hiyo. [Delegated and Vested to him].Leo hii watu wako kwenye sehemu ile ile ya Marehemu hawatendei ipasavyo mbona jamani katiba nakili inamapungufu ndio lakini ndio hii tunayoendeshea mambo yetu,leo mimi ni kijana chini ya miaka 35 nasoma kuna baadhi ya mambo yako sawa kama hili la madaraka ya Rais na Waziri Mkuu.

Nikiludi kwenye point ya msingi unasema Rais anahusika na SERA [Ibara 53] sikuelewi naomba ufafanuzi KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977 [CHAPISHO 2005] ibara ya 53 inazungumizia

Uwajibikaji wa Serikali Sheria ya 1984 Na.15 ibara 9
53.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mkuu atawajibika kwa Rais kuhusu utekelezaji wa madaraka yake.
(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano, chini ya mamlaka ya Rais, ndiyo itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya sera ya Serikali kwa jumla, na Mawaziri, chini ya uongozi wa Waziri Mkuu, watawajibika kwa pamoja Bungeni kuhusu utekelezaji wa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano

Hivi sentensi hii "Waziri Mkuu atawajibika kwa Rais kuhusu utekelezaji wa madaraka yake."maana yake nini?
Kuwajibika kwa tafsiri yangu sio kunyang'anya nguvu /mamlaka/madaraka [Power or authority vested into the person].

Kwa Tafsi ya Baraza la Kiswahili Tanzania [TUKI] neno wajibika ni
Wajibik.a* kt [sie] be responsible for, act responsibly. (tde) wajibikia; (tdk) wajibikika; (tds) wajibisha. (Kar)
.wajibu* nm [u-] responsibility, obligation, duty: Ni ~ wa kila mzazi kumlea mtoto wake it is each parent's resposibility to bring up his/her child. (Kar).

Hivi kuwa wajibika [Responsible for act] ndio kuondolewa dhamana/mamlaka/nguvu ambayo tafsiri unayotaka kujenga wakati katiba yenyewe inamwambia Rais rejea ibara ya 34 (5) a na b. na bado msumalia unazidi kumaliza nguvu ya Rais kwa kumpa Waziri Mkuu kujitetea kwa kipengele hiki 35-(1) na kuendelea.


Serikali ya Jamhuri ya Muungano na mamlaka yake Sheria ya 1984 Na.15 ib
.
34-(5) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika ibara hii hayatahesabiwa kwamba-
(a) yanahamishia kwa Rais madaraka yoyote ya kisheria yaliyowekwa na sheria mikononi mwa mtu au mamlaka yoyote ambayo si Rais; au
(b) yanalizuia Bunge kukabidhi madaraka yoyote ya kisheria mikononi mwa mtu au watu au mamlaka yoyote ambayo si Rais


Utekelezaji wa shughuli za Serikali Sheria ya 1984 Na.15 ib.9
35.-(1) Shughuli zote za utendaji za Serikali ya Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na watumishi wa Serikali kwa niaba ya Rais.
(2)
Amri na maagizo mengine yanayotolewa kwa madhumuni ya ibara hii yatathibitishwa kwa namna itakavyoelezwa katika kanuni zilizowekwa na Rais, kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii.

Sasa watanzania wenzangu hivi woga wa Waziri Mkuu kuitumikia Sheria Mama [KATIBA] unatokana na nini wakati katiba hiko wazi kwake kuitumikia Wakuu.

Nikinukuuu kipengele cha 34-(5) na zile code of Conducts & Ethics the Serikalini hakika na Rejea Sheria MAMA yani KATIBA inasema nini kuhusu waziri Mkuu.Katiba Mama wa sheria inasema wajibu wa Waziri Mkuu ni

Kazi na mamlaka ya Waziri Mkuu Sheria ya 1984 Na.15 ib.9
52.-(1)
Waziri Mkuu atakuwa na madaraka juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Waziri Mkuu atakuwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni.
(3) Katika utekelezaji wa madaraka yake, Waziri Mkuu atatekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote au mambo yoyote ambayo Rais ataagiza kwamba yatekelezwe.

Uwajibikaji wa Serikali Sheria ya 1984 Na.15 ibara 9
53.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mkuu atawajibika kwa Rais kuhusu utekelezaji wa madaraka yake.
(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano, chini ya mamlaka ya
Rais, ndiyo itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya sera ya Serikali kwa jumla, na Mawaziri, chini ya uongozi wa Waziri Mkuu, watawajibika kwa pamoja Bungeni kuhusu utekelezaji wa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Hapa ningependa kusema kama wengi wetu tunaona ibara hii inamzuia Waziri Mkuu kutenda kwa misingi ya kuwa kipengele 52-(1) kinampa nguvu/madaraka kisha anashindwa kuyatumia kwa msingi ya kipengele cha 52-(3) basi hakika WAZIRI MKUU huyo atakuwa ni MWOGA/na ASIYEJIAMINI kwa kuwa endapo atatofautina kwa misingi ya kutokutofautina na Rais ambae ndiye kiongozi wake na ile dhana ya OBEY YOUR SUPERIOR hata katika mambo ya msingi ambayo dhahili yana madhara kwa Taifa.

Hakika kwa Waziri Mkuu mwenye busara ili kuweka kumbukumbu sahihi ni vyema akakaa pembeni na kutwambia nilitenda A na kuamua B lakini kwa dhamana ile ya Katiba Ibara ya 52 -(1) na (2) lakini nimeamua A na Kutenda B lakini Kiongozi Mkuu tumetofautina kwa mujibu wa ibara ya 52-(3) na 53 -(1) na (2) ya Katiba. Hivyo binafsi kama Waziri Mkuu naachia ngazi kwa kuwa natofautina nae kwa hoja A,Be na Che na kwa swala hilo tulioko nje tunapima kauri zake na matendo yake na yale ya bosi wake ambae ni Rais wa Nchi kisha tunaludi kwenye katiba na kuona inasemaje basi tunahukumu kwa mujibu wa matendo ya kuwajibika.

Kwa zoezi zima la sakata la Zitto na Kujiuzuru kwa mawaziri kwa mujibu wa katiba hii Waziri Mkuu hana wa kumlaumu kuwa anaonewa kwa kuwa Katiba inamnyima nguvu eti kuegemea kuwa anategemea kipengere 52.-(1) na Uwajibikaji w Serikali (Collectivelly Responsibility) 53.(1) na (2) basi awajibike hivyo hivyo kwa kukubali dhamana ya Ibara 52.-(1) na (2).

Kama alivyoapta kusema M/Kijiji hakuna madaraka yasiyokuwa na wajibu!!!Japo katiba yetu ni mbovu lakin sio kiasi cha kutunyima nafasi ya kujua wapi pa kutokea na kusimamia,mengineyo yote ni woga,kutokuwa na uthubutu [dare] wa kusema hapana kisa wakubwa watakasilika,huku kuwafurahisha wakubwa huku ,basi wakianza kulia wao lia nao,usitake kuwafurahisha ukifika wakati wa kulia utake kuluka kulia nao,noooo thats big noo.

Na kama sheria ilivyo kabla bosi mafua hayajamshika basi nyie wadogo muanze kupiga chafya,na ndio maana waliotengeneza katiba hiyo waliitengeneza wakijua wanampa kila mmoja huku kile wakimnyanganya hiki.Rais kapewa nguvu yeye binafsi nae akanyaganywa 34.-(5) a na b. na vivyo hivyo waziri mkuu
52-(3) na 53 -(1) na (2).

Kilichotakiwa ni KUWAJIBIKA KWA TAFSIRI NA MATENDO NA SIO BRA BRA KATIBA IKO WAZI NI VYEMA BASI MSEMO WA KUNGURU MWOGA UKIMBIZA MBAWA YAKE [RESIGN=QUIT] ILI TULIOKO NJE TUPIME TOFAUTI TUTAJUAJE TOFAUTI WAKATI HUMO NDANI YA JAHAZI.!!!
 
DO! Inaonekana kweli hujanielewa, kama ambavyo na mimi sijakuelewa. Mimi nina maanisha kuwa kilichotamukwa katika ibara ya 52 ni kazi za kufanywa na PM siyo madaraka ya kuzitekeleza. Nikaongeza kusema kuwa ktk kutekeleza kazi zake PM anategemea huruma ya RAIS, kwani RAIS ndiye mwenye mamlaka juu ya watu ambao PM anapaswa kuwasimamia ili kutekeleza kazi za serikali: WATU HAO (1) wanateuliwa na RAIS, na (2) kama ni swala la kuwajibika, wanawajibika kwa RAIS siyo kwa PM. Sasa kama hakuna kitu cha maana kinafanywa na serikali mimi ninaami kuwa wakushughulikia, muundo huu wa kwetu ambapo RAIS ndiye mwenye mamlaka, ni RAIS siyo PM.


UNASEMA SOKOINE alifanya makubwa, ni kwa sababu moja, RAIS mwenye mamlaka alikubali SOKOINE atumie mamlaka yake. KAMA NYERERE angekatalia mamlaka yake basi, SOKOINE naye angekuwa mtu wa kucheza MAKIDAMAKIDA. PM wetu anafanya kazi kwa mtindo wa kushitaki, that is a fact, yaani kama kuna mtu anamuona anatenda visivyo anachoweza kufanya ni kumshtaki kwa RAIS. SASA Rais kama atakuwa mtu wa kuchukua hatua, PM ataonekana anafanya kazi, vinginevyo, ndo mambo yanakuwa kama tunavyoyaona sasa...

Mkuu Nyamka naona na wewe pia umekuja na mchanganyiko usio na miguu wala kichwa kwa kuwa umeeenza vizuri umefika mwisho umevurunda kuliko hata dhana ambayo mwanakijiji alitaka kuijenga kwa kuwa najua kiu ya Mwanakijiji ni hicho kiti cha juu kihukumiwe kwa kuwa ndicho chenye jicho la mwisho la kuona yote haya,lakini nae pia anasahau kuwa kwa kiti hicho hicho cha uwziri mkuu wa Hayati Edward Sokoine kilitenda mambo mazito kwa mujibu wa nguvu/dhamana/wajibu husika ya Kisheria na Kikatiba aliyokuwa amepewa na Rais kwa mujibu ya katiba husika miaka hiyo. [Delegated and Vested to him].Leo hii watu wako kwenye sehemu ile ile ya Marehemu hawatendei ipasavyo mbona jamani katiba nakili inamapungufu ndio lakini ndio hii tunayoendeshea mambo yetu,leo mimi ni kijana chini ya miaka 35 nasoma kuna baadhi ya mambo yako sawa kama hili la madaraka ya Rais na Waziri Mkuu.
 
Ni matumaini yangu - na maombi yangu -kuwa Spika Makinda atakubali hoja hii na kuitisha kikao cha Bunge cha dharura chini ya kifungu cha 27:4 cha Kanuni za Bunge kuwa "Endapo manufaa ya Taifa yatahitaji kuwa Bunge lisikutane tarehe ile iliyowekwa kwa Mkutano utakaofuata, bali likutane tarehe ya mbele zaidi au ya nyuma zaidi, basi Spika anaweza, baada ya kushauriana na Kamati ya Uongozi, kuliita Bunge likutane tarehe hiyo ya mbele zaidi au nyuma zaidi." Ninaamini kama matakwa ya Katiba yametimizwa (taarifa ya asilimia 20 ya wabunge kutaka hoja hiyo iletwe) basi Spika NI LAZIMA aitishe kikao maalum cha Bunge mapema zaidi


Contradictory article!!!

Ni yeye huyu mwanakijiji alimtaka zitto asiwasilishe hoja jumatatu kwa spika
 
MMM nimefarijika na elimu uyoitoa. Ila uwajibikaji kwenye katiba hii napata mashaka kidogo hususani kutokana na katiba hii kumpa madaraka makubwa raisi kuteua Waziri Mkuu,Jaji Mkuu,Mwanasheria Mkuu,Mkuu wa Jeshi la polisi,Mkuu wa Jeshi la wananchi,Mkuu wa usalama wa taifa,Mkuu wa TAKUKURU,Wakuu wa mikoa,Mawaziri,Katibu mkuu kiongozi,Makatibu wakuu wa wizara,Makatibu tawala wa Mikoa,Wenyeviti wa bodi za wakurugenzi za mashirika ya uma...list ni ndefu.

Nani wa CCM ana ubavu wa kurusha maneno dhidi ya viongozi wa juu wa nchi ili hali anajua kesho yake TAKUKURU/USALAMA/JESHI LA POLISI watabisha hodi mlangoni mwake na kumuuliza ujasiri wa kumsema mkuu anautoa wapi!

Mungu ibariki Tanzania dhidi ya huu utawala mbovu wa CCM.
 
Back
Top Bottom