Kura ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu ni kura dhidi ya Rais na Chama tawala!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995


Binafsi naweza kusema kwamba, nikiangalia kiufundi naweza kusema kuwa kama kuna sababu kubwa na ya msingi ya kuvunja baraza la mawaziri siyo shinikizo la wanasiasa, wananchi au watu wengine bali KUSHINDWA KUWAJIBIKA kwa pamoja. Kwenye serikali kuna nadharia ya "collective responsibility" kwamba mawaziri wote wanafanya kazi kwa pamoja kwa ridhaa ya Rais.

Ikumbukwe kuwa katika nchi yetu chombo kikuu cha kumshauri rais juu ya utendaji wa mambo mbalimbali ya serikali na majukumu yake siyo Bunge, au vyama vya siasa bali ni Baraza la Mawaziri. Katiba yetu inaliweka hili wazi kwa maneno yafuatayo Ibara ya 54:3 "Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara ya 37(1) ya Katiba hii, Baraza la Mawaziri litakuwa ndicho chombo kikuu cha kumshauri Rais juu ya mambo yote yanayohusika na utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, na litamsaidia na kumshauri Rais juu ya jambo lolote litakalowasilishwa kwenye Baraza hilo kwa mujibu wa maagizo maalum au maagizo ya jumla yatakayotolewa na Rais."

Na kutokana na uzito huu - kwamba ndicho chombo cha kuaminiwa na rais kumpa ushauri - katiba inaweka kinga kamili (absolute immunity) kwa baraza hilo linapotoa ushauri kwa Rais. Inasemwa "Suala kama ushauri wowote, na ni ushauri gani, ulitolewa na Baraza la Mawaziri kwa Rais, halitachunguzwa katika mahakama yoyote." Kwa maneno mengine mawaziri wanaweza kutoa ushauri pasi ya hofu kuwa mambo waliyoshauri yanaweza kutumiwa dhidi yao mahakamani au hata kuchunguzwa!

Sasa dhana hii ya kuwajibika kwa pamoja kwa baraza la mawaziri kimsingi inaenda sambamba na hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu (serikali). Kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu siyo kura dhidi ya mtu binafsi! Ni kura dhidi ya serikali na inapopigwa serikali nzima lazima ivunjwe na siyo tu kuvunjwa lakini serikali nzima inatakiwa kujiuzulu na kuitisha uchaguzi mpya. Wikipedia inaelezea hili hivi (kwa sisi tunaofuata mfumo wa Westminster) "if a
vote of no confidence is passed in parliament, the government is responsible collectively, and thus the entire government resigns. The consequence will be that a new government will be formed, or parliament will dissolve and a general election will be called" Huwezi kuwa na kura ya kutokuwa na imani na serikali na Rais akabakia! Huwezi kuwa na kura ya kutokuwa na imani na serikali na Bunge likabakia! If one falls, the other must follow!

Nadhani ni makosa kufikiria kuwa kura hii ni dhidi ya Pinda kama Waziri Mkuu; mtazamo huu siyo sahihi. Pinda ni Waziri Mkuu wa Serikali iliyoko madarakani. Yeye kama Waziri anafanya kazi kwa mujibu wa Katiba lakini akitekeleza majukumu yake chini ya Rais. Bahati mbaya sana Waziri Mkuu wetu siyo mtendaji (a non-executive Prime Minister) yaani siyo anayeunda serikali. Waziri Mkuu wetu japo anapitishwa na Bunge hawajibiki kwa Bunge moja kwa moja! Ibara ya 53:1 ya Katiba iko wazi katika hili "Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mkuu atawajibika kwa Rais kuhusu utekelezaji wa madaraka yake." Hii ina maana ya kwamba, Waziri Mkuu akiboronga kama yeye chombo cha kumwajibisha ni kilichomteua yaani Rais!

Na kifungu kinachofuatia kinaiweka dhana hii ya "kuwajibika kwa pamoja" kwenye Katiba yetu. Kifungu hicho kinasema "Serikali ya Jamhuri ya Muungano, chini ya mamlaka ya Rais, ndiyo itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya sera ya Serikali kwa jumla, na Mawaziri, chini ya uongozi wa Waziri Mkuu, watawajibika kwa pamoja Bungeni kuhusu utekelezaji wa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano." Ni muhimu kutambua kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano mkuu wake siyo Waziri Mkuu! Waziri Mkuu ndiye "kiongozi wa shughuli za serikali Bungeni". Hata hivyo, katiba pia inampa madaraka Waziri ya kusimamia shughuli za kila siku za serikali kwenye ibara ya 52:1 ya Katiba yetu. Hata hivyo madaraka hayo yanafungwa na kifungu hicho cha 53:1

Ibara ya 33:2 ya Katiba yetu inasema hivi kuhusu madaraka ya rais kuwa "Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu." Ni vizuri kuona tofauti ya "kiongozi" inavyotumiwa kwa Waziri Mkuu na kwa rais. Waziri Mkuu nimeonesha anaitwa "kiongozi wa shughuli za serikali Bungeni" yaani "leader of Government business in the National Assembly" lakini rais ni "Head of Government". Hii ina maana gani basi?

Hii ina maana ya kwamba, kama serikali inapwaya, kama serikali haitekelezi kazi zake vizuri na kama inaonekana kuwa serikali imechafuliwa sana basi mtu sahihi na wa kwanza kulaumiwa ni Rais! Waziri Mkuu anaweza kulaumiwa kama kule bungeni mawaziri walikuwa wanagongana au walikuwa hawawajibiki kwa pamoja. Lakini kama ni suala la serikali nzima kuwa na matatizo basi mtu sahihi wa kubebeshwa lawama ni Mkuu wa Serikali (head of government) yaani rais.

Sasa, kwa vile serikali ni moja ni vigumu kutenganisha kuwajibika kwa Waziri Mkuu na kuwajibika kwa rais. Ikumbukwe ni Rais ndiye anayemteua Waziri Mkuu akiwa na uhuru kamili (absolute freedom) na hulipendekeza jina hilo kwa Bunge. Waziri Mkuu mkuu anasimamia utekelezaji wa serikali kwa niaba ya Rais. Sasa Katiba yetu haijaweka utaratibu wa kumpigia rais kura ya kutokuwa na imani lakini imeweka utaratibu dhidi ya Waziri Mkuu. Kwa msingi wa kuoanisha uhusiano ulipo kati yaWaziri Mkuu na Rais ni wazi kuwa kumpigia kura Waziri Mkuu ni kupigia kura serikali; na kuipigia serikali ni kumpigia kura Rais ambaye ndiye MKUU WA SERIKALI. Huwezi - narudia tena - kujipanga kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu halafu ukasema una imani na Rais! Huwezi kumnyoshea mkono Waziri Mkuu kuhusu utendaji mbovu wa seriakli bila wakati huo huo kumnyoshea mkono Rais ambaye ndiye aliyemteua Waziri Mkuu huyo lakini vilevile ndiye mkuu wa serikali hiyo.

Mmoja akiondolewa na mwingine ni lazima afuate ndio maana rais anapokufa au kuacha urais kwa sababu zilizoanishwa Kikatiba Waziri mkuu naye anapoteza nafasi yake na baraza la mawaziri linavunjika! Ni sauti na mwangwi! Chini ya Ibara ya 36 Rais ndiye anauamuzi wa mwisho wa nani anatumikia serikali hii kwani ana uwezo wa kumfukuza mtu yeyote kwenye utumishi wa umma. Siyo Waziri Mkuu.

Lakini huwezi pia kunyoshea kidole Waziri Mkuu na rais bila kunyoshea kidole chama cha Waziri Mkuu na Rais. Ikumbukwe kuwa Rais wa Tanzania anachaguliwa na wananchi lakini sharti la msingi chini ya Ibara ya 39:1c. Ibara hiyo inasema mojawapo ya sifa za mtu kuwa Rais ni kuwa ni lazima awe "ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa". Kimsingi Rais ni lazima atoke kwenye chama. Katika suala letu rais wetu anatokana na Chama cha Mapinduzi - ndiyo mwanachama wake na ndicho kilichompendekeza. Kuinyoshea mkono serikali ni kunyoshea mkono chama kilichounda serikali hiyo.

Lakini pia tuangalie kwa namna nyingine kidogo; Bunge linapomnyoshea mkono Waziri Mkuu ina maana linaonesha halina imani na serikali - ndio maana inaitwa kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu - na hivyo halina imani na Rais. Bunge linapokosa imani na Rais ambaye anamteua Waziri Mkuu lenyewe pia linajikuta matatani kwani Rais ni sehemu ya Bunge! Ibara ya 62:1 iko wazi kuhusu hili "Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo
litakuwa na sehemu mbili, yaani Rais na Wabunge" Hivyo, Bunge linaponyoshea kidole sehemu yake mojawapo - yaani rais - Bunge linajinyoshea lenyewe kidole; kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni kutokuwa na imani na Rais na kutokuwa na imani na rais ni kutokuwa na imani na sehemu ya bunge; Waziri Mkuu akilazimishwa kujiuzulu Rais naye ni LAZIMA ajiuzulu! Na Rais akijiuzulu Bunge lazima livunjwe! Wote wanawajibika kwa pamoja per excellence!

Lakini pia tunaweza kuliona hili vizuri - Waziri Mkuu anapendekezwa na rais, na anapitishwa na Bunge. Sasa Bunge linapomgeuka Rais, Bunge linageuka uamuzi wake lenyewe. Ikumbukwe kuwa Pinda alipendekezwa na Rais, jina lake likaletwa Bungeni, Wabunge wakaulizwa na kuunga mkono uteuzi huo wa rais na sasa wanataka kuukataa. Sasa, hawawezi kuukataa na wao wakabakia! Naomba niweke tofauti kidogo ambayo ningependa ieleweke. Ni vizuri sana kuweka shinikizo Waziri Mkuu ajiuzulu au mawaziri wajiuzulu. Wabunge wanaweza kuweka shinikizo hilo kwa kutumia Bunge. Lakini wanapokaa na kuwa tayari kupiga kura ya kutokuwa na imani wamevuka kutoka kwenye shinikizo kwenda kwenye suala la kisheria ambalo lina matokeo; kupiga kura ya kutokuwa na imani ni Waziri Mkuu ni kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali (Rais) na kutokuwa imani na Rais (ambaye ni sehemu ya Bunge) ni kujishtaki lenyewe!

Ni sawa sawa na mtu kunyoshea kidole mtu kwenye kioo na kumtishia kumkata kichwa kwa panga. Well, ukitaka kumkata mtu wa kwenye kioo weka panga shingoni mwake, ukimkata yeye na wewe hubakii! hivyo, naunga mkono kabisa kura ya kutokuwa na imani na serikali lakini kama nilivyosema kwenye mada nyingine naamini watu wengi hawajui kuwa huwezi kuwa na kura ya kutokuwa na imani nusu - yaani ukaishia kwa Waziri Mkuu. Ni LAZIMA ili liende moja kwa moja kwa Rais, na kwa Bunge.

Ni matumaini yangu - na maombi yangu -kuwa Spika Makinda atakubali hoja hii na kuitisha kikao cha Bunge cha dharura chini ya kifungu cha 27:4 cha Kanuni za Bunge kuwa "Endapo manufaa ya Taifa yatahitaji kuwa Bunge lisikutane tarehe ile iliyowekwa kwa Mkutano utakaofuata, bali likutane tarehe ya mbele zaidi au ya nyuma zaidi, basi Spika anaweza, baada ya kushauriana na Kamati ya Uongozi, kuliita Bunge likutane tarehe hiyo ya mbele zaidi au nyuma zaidi." Ninaamini kama matakwa ya Katiba yametimizwa (taarifa ya asilimia 20 ya wabunge kutaka hoja hiyo iletwe) basi Spika NI LAZIMA aitishe kikao maalum cha Bunge mapema zaidi.

Ni matumaini yangu vile vile kuwa Rais Kikwete hatovunja baraza la mawaziri sasa hivi au kufanya mabadiliko yoyote kwa sababu ya hoja ya kina Zitto kwa sababu mabadiliko hayo sasa YAMECHELEWA MNO kiasi cha kupoteza umaana. Sasa hivi hoja iliyopo mbele ya taifa ni kuwa wananchi hawana imani na serikali yao na Rais Kikwete hawezi kupata imani hiyo kwa kufanya mabadiliko isipokuwa kwa Waziri Mkuu wake kupigiwa kura hiyo. Hivyo, ninaamini kabisa kuwa rais akubaliane na Spika ili Bunge liitishwe mapema kabisa iwezekanavyo ili Serikali yake ijaribiwe na wawakilishi wa wananchi na awe tayari kwa matokeo yoyote yale.

Hata hivyo, naamini pia kwa rais kukubali hili ni LAZIMA AWEKE WAZI kwa Wabunge wote kuwa Kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni kura ya kutokuwa na imani na serikali yake na ni kura ya kutokuwa imani na yeye na kuwa yuko tayari kabisa wabunge wawe uhuru kabisa katika kura ya SIRI kupiga kura hiyo na kuwa endapo wabunge hawana Imani na Waziri Mkuu na wakaonesha hivyo kwa kura basi Waziri Mkuu ataondolewa lakini siyo hapo tu na yeyemwenyewe atajiuzulu na kuvunja Bunge ili nchi ianze upya. Ikumbukwe huwezi kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu lakini ukataka kubakia ama na Rais au na Bunge.

Hakuna mabadiliko nusu! Tumeamua kuvua nguo, tuyaoge.


Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
 
na-waziri-mkuu1.jpg

Mbona kama wanagombana vile!
Pinda anamwambia Zitto usiniharibie kitumbua, Zitto anamwambia sina imani na wewe
 
Most of the beautiful things in life come with the element of suprise. Serikali kuamua kujipanga upya labda kwa nguvu ya umma
 
"Hata hivyo, naamini pia kwa rais kukubali hili ni LAZIMA AWEKE WAZI kwa Wabunge wote kuwa Kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni kura ya kutokuwa na imani na serikali yake na ni kura ya kutokuwa imani na yeye na kuwa yuko tayari kabisa wabunge wawe uhuru kabisa katika kura ya SIRI kupiga kura hiyo na kuwa endapo wabunge hawana Imani na Waziri Mkuu na wakaonesha hivyo kwa kura basi Waziri Mkuu ataondolewa lakini siyo hapo tu na yeyemwenyewe atajiuzulu na kuvunja Bunge ili nchi ianze upya. Ikumbukwe huwezi kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu lakini ukataka kubakia ama na Rais au na Bunge."

Mkuu Mwanakijiji,

nimekuelewa, na asante kwa makala yako yenye ufafanuzi murua. Lakini kuna haja gani ya rais kuwafafanulia wabunge au kuwa wazi kwa wabunge kama ulivyoelezea hapo juu? Ikiwa muongozo upo kwenye katiba, huoni kama kumshauri hivyo kunampa nafasi ya kuchakachua maamuzi yao (wabunge) ambayo wamakwishaamua kuyafanya siku kadhaa nyuma, na kwamba ni namna mpya ya kuomba huruma? Ninadhani asiwaambie chochote kama ambavyo hajasema chochote hadi sasa...Kura zipigwe na kila mtu akubali matokeo.

Labda makala yako itamsaidia yeye kuelewa mapana ya kura ya kutokuwa na imani na PM.
 
Kama ingekuwa ni dhidi ya Rais, Zitto hakuwa na haja kupitia kwa Waziri Mkuu. Bunge linaweza kikatiba kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais mojakwamoja. Kutokuwa na imani na chama tawala ni ngumu zaidi kwani Bunge hili lina zaidi ya theluthi mbili ya Wabunge wa CCM. Kwa ulafi wa wabunge hawa hili ni ndoto kuungwa mkono.
Ukichukulia "special relation" iliyopo kati ya Zitto na Jakaya kura hii kwa Pinda ina maigizo mengi ndani yake. Tusubiri tuone kinachokuja siku hizi mbili tatu.
 
"Hata hivyo, naamini pia kwa rais kukubali hili ni LAZIMA AWEKE WAZI kwa Wabunge wote kuwa Kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni kura ya kutokuwa na imani na serikali yake na ni kura ya kutokuwa imani na yeye na kuwa yuko tayari kabisa wabunge wawe uhuru kabisa katika kura ya SIRI kupiga kura hiyo na kuwa endapo wabunge hawana Imani na Waziri Mkuu na wakaonesha hivyo kwa kura basi Waziri Mkuu ataondolewa lakini siyo hapo tu na yeyemwenyewe atajiuzulu na kuvunja Bunge ili nchi ianze upya. Ikumbukwe huwezi kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu lakini ukataka kubakia ama na Rais au na Bunge."

Mkuu Mwanakijiji,

nimekuelewa, na asante kwa makala yako yenye ufafanuzi murua. Lakini kuna haja gani ya rais kuwafafanulia wabunge au kuwa wazi kwa wabunge kama ulivyoelezea hapo juu? Ikiwa muongozo upo kwenye katiba, huoni kama kumshauri hivyo kunampa nafasi ya kuchakachua maamuzi yao (wabunge) ambayo wamakwishaamua kuyafanya siku kadhaa nyuma, na kwamba ni namna mpya ya kuomba huruma? Ninadhani asiwaambie chochote kama ambavyo hajasema chochote hadi sasa...Kura zipigwe na kila mtu akubali matokeo.

Labda makala yako itamsaidia yeye kuelewa mapana ya kura ya kutokuwa na imani na PM.


Kama wabunge wanachukua msimako kwa sababu ya principle kweli sidhani kama Rais akiwaambia matokeo ya msimamo huo watabadilisha msimamo wao. Unless...
 
Kama ingekuwa ni dhidi ya Rais, Zitto hakuwa na haja kupitia kwa Waziri Mkuu. Bunge linaweza kikatiba kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais mojakwamoja. Kutokuwa na imani na chama tawala ni ngumu zaidi kwani Bunge hili lina zaidi ya theluthi mbili ya Wabunge wa CCM. Kwa ulafi wa wabunge hawa hili ni ndoto kuungwa mkono.
Ukichukulia "special relation" iliyopo kati ya Zitto na Jakaya kura hii kwa Pinda ina maigizo mengi ndani yake. Tusubiri tuone kinachokuja siku hizi mbili tatu.

Bunge haliwezi kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais; hakuna mfumo huo. Linaweza kumshtaki Rais kibunge (impeachment).
 
Ni muda wa vitendo sasa story ziishe. Nyie kina MMM ndio wa kushawishi watu watambue Urai wao sio kulalamika tu. Wengine wanakatwa SDL na Payee kubwa lakini hawaelewi na hawajui kufuatilia zinapokwenda. Ningependa kuona 3ds za mabadiliko sio malalamiko.
 
Ni muda wa vitendo sasa story ziishe. Nyie kina MMM ndio wa kushawishi watu watambue Urai wao sio kulalamika tu. Wengine wanakatwa SDL na Payee kubwa lakini hawaelewi na hawajui kufuatilia zinapokwenda. Ningependa kuona 3ds za mabadiliko sio malalamiko.
Vitendo bila serious political thought of what we would like to do, itakuwa ni hatari kwa usalama na uwepo wa Taifa letu. Angalia leo Libya au Egypt na hata Syria...hawakujipanga. Wanalazimisha mabadiliko bila kujua stake ya kila mtu kwenye hayo mabadiliko. Mwisho wake ni kugawana vipane vipande vya nchi.
Tuanze kuumiza vichwa ili tutakapokwenda kwenye next stage tutakuwa tujua nini tunakitaka
 
na-waziri-mkuu1.jpg

Mbona kama wanagombana vile!
Pinda anamwambia Zitto usiniharibie kitumbua, Zitto anamwambia sina imani na wewe

Maelezo ya Mzee Mwanakijiji wala hayajikanganyi, ni mawazo yake tu, anayeweza kujikanganya ni msomaji mwenyewe ambaye angependa kusikia maneno fulani kwa style aipendayo yeye kiasi ambacho mwandishi yeyote hawezi kumtimizia kila mtu mmojammoja ladha aitakayo. Mchezo wa siasa ndivyo ulivyo. Huenda nje jamaa hawa ni marafiki wakubwa sana na wanaheshimiana sana, na huenda pia waliambiana kwamba mambo hayo yatajitokeza na kila mtu achukue tahadhari kwa upande wake na labda na wanajua hatama ya mjadala huu. Lakini hawa watu si ni wapinzani kati yao na lazima kupashana majoto? Huenda Zitto anajua kabisa ugumu wa anayoyataka yafanyike lakini wanaocheza karata sio maadui ila ni washindani tu.

Anachokieleza Mzee Mwanakijiji ni tafakuri ya mambo anavyoyaona, sasa mwingine naye na atoe changamoto yake sio kwa sentensi moja kwamba "Yanajichanganya", bali apangue kila hoja iliyotolewa kwa ushahidi na tafakuri yake binafsi na hapo ndiko kukomaa kwa JF na member wake, ndiko kutalipatia jukwaa hili uaminifu na quality of supplied information. Vinginevyo ni kujaribu kuzodoana na au kukatishana tamaa isivyo hekima. Songa mbele Mzee Mwanakijiji, wapo ambao wanapenda wasiluelewe, lakini wengi sana wanapendaa kukuelewa. Ukiona wote wanakuelewa mara moja hoja yako pasipo upinzani ujue kuna kasoro katika hoja yako.
 
Mwanakijiji umenena, hata hali halisi INAONYESHA; ni nani sasa hivi ana imani na RAIS au hili BUNGE la CCM? Labda hao wachache wanaofaidika na vyombo hivyo viwili lakini siyo wananchi wa kawaida ambao matatizo yao hayapewi kipaumbele na yeyote.
 
Most of the beautiful things in life come with the element of suprise. Serikali kuamua kujipanga upya labda kwa nguvu ya umma
Sauti ikanijia na kuniuliza, "Entrepreneur Unaona nini?'' Nikajibu, "Ninaona vyungu vinne vinavyochemka vikiwa vimeinama midomo yake ikielekea upande wa kaskazini, Kusini, Mashariki na Magharibi.''. Yule Bwana akaniambia,

Kutoka
pande zote nne za nchi hii, maandamano makubwa yatatokea na maafa yatamwagwa kwa wale wote watendao maovu na kufisidi mali ya UMMA. Mwenyezi Mungu atatoa hukumu yake kwa serikali hii kwa sababu ya uovu wao wa kuwasahau wananchi na kutanguliza matumbo yao na ya familia zao. Polisi wao watakuja na silaha zao, kuzunguka pande zote za miji ili kuwalinda na Ghadhabu ya UMMA, lakini hawatawashinda, kwani Mungu wenu atakuwa pamoja Nanyi
 
du jamaa ana usongo na hii serikali sijui wamemfanyia nini, i assume wewe sio CCM then:A S shade:
 
Back
Top Bottom