Kura ya kutokuwa na imani na rais kikwete huu ndiyo wakati wake

Napendekeza Mkono, Filikunjombe na Lugola waanzishe harakati hizi, ili kama liwalo na liwe!
Mkono huyuhuyu aliyesema patachimbika, akachimbwa yeye na akawa kimya, hakuna Mbunge hata mmoja magambani aliye kwa maslahi ya wananchi.

Naunga mkono hoja, kama si kikatiba, tumtoe kinguvu, abaki huko huko Oman asirudi huku huyo mzururaji
 
Siku hizi hata wanajeshi shupavu kama mayunga hawapo.

Si wachukue inchi ili sisi na vizazi vyetu tubakie salama kwa eshima na taazima ya watazania!
 
jamaa anaonyesha jinsi alivyo dhaifu. nchi inateketea huku ye anakula bata uarabuni
 
Kwanza dalili zote zinaonyesha huo urais hautaki tena, kachokaaa! Tatizo ni mafisadi wanaomlazimisha ili waendelee kukomba!
 
Rais na Pindo wake wanakula tu bata ughaibuni wananchi wao wanahangaika kama watu wasiokua na makwao.Mwenye nchi hebu linda heshima kwa kung'atuka kabla ya kupigiwa kura.Nyepesi tunaomba lianzishe hili huko mjengoni
 
Dhaifu anatia hasira sana,lakini ataondolewaje wakati hata bunge ni dhaifu.kweli tunaongozwa na kilaza bora tungeweka jiwe lituongoze kuliko huyu vasco da gama.aondolewe tu kama vp.
 
Chaguo la mungu! subira yavuta kheri bado miaka mitatu tuu!

ni kweli ulilo sema, lakini kwa mwenendo huu yafaa tumuoneshe kuwa watanzania tumechoka na utawala wake usio na malengo.hata kama tutaitisha kura ya maoni ya kwenye mtandao itatosha kufikisha ujumbe wetu. sijapata kuona kiongozi wa ngazi yoyote aliye shindwa kama yeye.
 
Siku hizi hata wanajeshi shupavu kama mayunga hawapo.

Si wachukue inchi ili sisi na vizazi vyetu tubakie salama kwa eshima na taazima ya watazania!
Nimewaza hivyohivyo! kwanini wanajeshi wasichukue Nchi japo kwa mwaka mmoja waone nchi itakavyo lipuka kwa shangwe na vigelegele. kweli dhaifu kaiangamiza nchi yetu.MUNGU MUWEZA WA YOTE ATATENDA MAAJABU.
 
kweli hili janga kwa taifa ila wabunge sidhani kama wanaweza kufanya hivyo cauze wanamuogopa tumpe LOWASSA Tanzania ndicho kilichobakia watu​ wangu
 
"Tumefika hapa kutoka a na udhaifu wa rais Kikwete" by Mnyika (mbunge) sometimes in June 2012 bungeni Dodoma
 
Huyu jamaa ni tatizo sijua kwa nini alitokea hapa nchini jamani tujiulize sana kuhusu huyu Jk nadhani kuna shida juu ya mtu huyu, lakini kuna kitu nimeambiwa leo na rafiki yangu kuwa tumeweka nchi kwa mtu anayetegemea nguvu za giza ndiyo maana mambo haya tunayaona maana hana hofu ya Mungu kila jambo anategemea ni NGUVU ZA GIZA hivyo ameiweka nchi katika laana kubwa. Tumuombe Mungu atuondolee hili janga maana kuendelea kuwepo hadi 2015 itakuwa hatari sana, mtu ambaye hawezi hata kuoga hadi mganga amwambie sasa nenda kaoge, hata kutoka ndani hadi mganga aseme. Kwa hiyo tunaongozwa na waganga wa kienyeji hatuna rais jamani tufikirie sana juu ya hili
 
Sina imani na rais, rais gani huyu hana uwezo wakutoa tamko, anakaatu kazi kuzurura wakati nchi ni tete
 
mkono alitia sahii kuto kuwa na imani na waziri mkuu kilichomkuta kakosa nafasi nek ya sisim mimi sina imani na rais na mawaziri wake

ngoja nipate 2 mbege
 
Mod, naomba usibanie uzi huu kwa sababu si uchochezi, bali ni uhalisia unaotokana na Katiba yetu.Nadhani huu ndiyo wakati kwa wabunge kuajiandaa KUPIGA KURA ya kutokuwa na imani na Rais Jakaya Kikwete kwa sababu ameshindwa kuongoza. Haiwezekani vurugu zote hizi nchini ziendelee, si yeye, Makamu wa Rais, wala Waziri Mkuu anayeshituka kuchukua hatua za kukemea kwa nguvu zote.

Katiba ya sasa imeainisha vizuri namna ya kumwondoa Rais madarakani kwa kutumia Katiba hiyo hiyo. Ndiyo maana napendekeza wabunge wajiandae ili Oktoba 30 watakapokutana mjini Dodoma, ajenda kuu ya Mkutano huo iwe kumwondoa Rais madarakani kutokana na kushindwa kwake kuilinda Katiba na Watanzania wote. JK asiponaswa kwenye udhaifu huu wa sasa, hatanaswa tena hadi 2015.

Nawasilisha.

Bila hata ya aibu unawanga mchana!!!!!!!!!!!!!!
 
Huyu jamaa ni tatizo sijua kwa nini alitokea hapa nchini jamani tujiulize sana kuhusu huyu Jk nadhani kuna shida juu ya mtu huyu, lakini kuna kitu nimeambiwa leo na rafiki yangu kuwa tumeweka nchi kwa mtu anayetegemea nguvu za giza ndiyo maana mambo haya tunayaona maana hana hofu ya Mungu kila jambo anategemea ni NGUVU ZA GIZA hivyo ameiweka nchi katika laana kubwa. Tumuombe Mungu atuondolee hili janga maana kuendelea kuwepo hadi 2015 itakuwa hatari sana, mtu ambaye hawezi hata kuoga hadi mganga amwambie sasa nenda kaoge, hata kutoka ndani hadi mganga aseme. Kwa hiyo tunaongozwa na waganga wa kienyeji hatuna rais jamani tufikirie sana juu ya hili

We mganga wako nani?????????? Acha Uzushi usio na ushahidi nao!!!
Bila shaka we ni mdini wa kutosha!!!! Na ule waraka uliorushwa humu huenda una chembe ya ukweli!!!!
 
Hii kali yaani mtu usipoenda choo unadai Rais ajiuzulu Hivi ni nani akipewa Nchi atawatuliza Uamsho, madaktari au Waalimu Shida hasa ni nini kwanini asiyetaka hali hii ya machafuko Duniani na hapa Tanzania asiende Duka la Mzinga akanunue Rifle 758 akaingia porini? ukipiga kelele humu JF au kuitisha kura sio njia sahihi ni kujifurahisha. Angalieni pale Kariakoo wanaotaka kuipima nguvu ya Dola wanavyobebwa na virungu tu hapo SMG, LMG au AK47 haijakohoa Ushauri wangu kajiandikishe 2015 sio mbali omba hata ubalozi kama utashindwa kuomba kugombea Urais Mwitongo hizo ni ndoto, miaka ya 1975 Vijiji vya Ujamaa tulishindwa kumtoa Kambarage aliyetunyanganya Mashamba, ikaja 1979 - 1981 mpaka mwenyewe alipokubali yaishe hakugombea tena Urais Nchi ndio ilikuwa taabani mpaka tukatumia sabuni za magwanji na viatu vya katambuga TV hatukuziona leo Computer na Internet unazithibiti na kuruhusiwa kutoa maoni yako huoni tofauti Basi weka hilo sanduku / hata Ballot Box mm ni NO BIG NO ww subiri 2015
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom