Kura ya kumsaka mbunge bora kijana; Nani anashangilia matokeo ya uchaguzi wa aina hii? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kura ya kumsaka mbunge bora kijana; Nani anashangilia matokeo ya uchaguzi wa aina hii?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jumakidogo, Dec 16, 2011.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Dec 16, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kwa kujifurahisha wewe pamoja na wenzako unaweza kuanzisha kura ya maoni kwa ajili ya kupambanisha watu maarufu ili upate maarufu bora kuliko wengine, mfano; kura zilizopigwa katika blog ya Mjengwa kumsaka mbunge kijana ambaye ni bora kuliko wengine. Wapo wanaochukulia kuwa matokeo ya kura hizi ndiyo kipimo rasmi cha kukubalika kwa mtu na kuanza kuangua shangwe furaha na mbinja wakitembeza mabango ya ushindi. Upigaji kura wa aina hii hauaminiki hata kidogo. Kwanza hakuna namna yoyote ya kuzuia mtu kupiga kura kwa kurudia rudia kwa sababu mtu anaweza kuwa na acc zaidi ya moja. Pili hata mgombea mwenyewe anaweza kujipigia kura mara nyingi atakavyo kwa kutumia IDs tofauti . Tatu; hapa umri haujazingatiwa kwa wapiga kura, siku hizi hata watoto wa miaka 8 hutumia mitandao usiku na mchana. Aina hii ya uchaguzi haitofautiani na ile ya kumsaka kinara wa BBA au BSS. Zaidi hizi ni kura za kujifurahisha na kupoteza muda tu, wala hakuna sababu ya kutembeza mabango kwa kushangilia ushindi wa kishindo cha unyayo wa sisimizi...Itafutwe namna ya kuwafikia watu wenye sifa hasa za kupiga kura popote waliopo ili tupate matokeo rasmi na yenye uhakika.
   
Loading...