Kura ya hapana yaibua mjadala upitishaji bajeti ya Serikali

Hoja zingine bungeni zinatolewa na waheshimiwa utadhani ni kikao cha mtu na familiake tu. unawezaje sema waliosema hapana wasipewe mafungu ya maendeleo ilihari kodi unakwenda kuzikusanya huko?. waheshimiwa muwe makini na kauli zenu, mtapasua vipande hili taifa.
 
kwan hizo hela wanapelekewa wabunge kwa ajili ya bata na familia zao? hata wasipopeleka watakuwa wanawakomoa watanzania wenzao
 
Huyu kifimbo cheza anatafuta sifa aonekane mkali aliyewaweza wapinzani!! Mtu timamu huwezi ongea vitu vyanamna hii hâta kwautani...wao mbona wameipinga na kuiponda ile ya upinzani?? Sijasikia hâta ccm mmoja akiunga mkono hâta sentensi moja kwenye bajeti ya upinzani.
Tuache ubabe wa kitoto...tutalipasua Taifa na awamu hii wameanza kufanya hivyo taratibu
 
Nina wasiwasi kuna wabunge, mawaziri na wanasiasa wengi hawajui dhana halisi ya kuwa na Serikali lakini pia hawajui mantiki ya kuwa na wawakilishi (Wabunge).

Kimsingi Serikali tumeiweka sisi madarakani ili kusimamia rasilimali zetu na kuhakikisha kwamba kila mtu ambaye amekabidhi mamlaka yake kwa hiyo Serikali anapata fursa ya maendeleo yake kiuchumi na kijamii. Lakini pia tumewachagua wabunge kama wawakilishi wetu ili kwa niaba yetu, Pamoja na majukumu mengine ifanye yafuatayo;
1. Wawasilishe mahitaji yetu kwa Serikali ili Serikali kututimizia au kutuwekea miundombinu ya kutatua changamoto za eneo husika.
2. Kuisimamia Serikali ili itende mambo yake sawa sawa na makubaliano yetu (wananchi tulioiweka madarakani - Social contract). Kwenye ili jukumu la pili Bunge inatakiwa liwe makini na kali kabisa kuhakikisha Serikali haiendi kinyume na misingi tuliyojiwekea.

Kutokana na hayo niliyoyaeleza ni hatari sana, Bunge linaposahau jukumu lake dhidi ya Serikali, na kujigeuza sehemu ya Serikali kusifia na kukubali kila kinacholetwa na Serikali bila kuhoji na kujiridhisha uthabiti wa kilicholetwa na Serikali. Nikionacho kwa sasa hakuna tena Bunge (kwa maana ya chombo cha uwakilishi wa wananchi) la wananchi bali tuna Bunge la vyama lililopo kwa maslahi ya vyama vyao. Mbaya Zaidi ni kwa sisi wananchi tusio sehemu ya vyama vya siasa, ambao kwa mtazamo wangu tumeshakosa wawakilishi kwenye Bunge la sasa, kukaa kimya na kuchekelea tu yanayoendelea huko wanapopaita Bungeni
 
me uyu jamaa nilishamchokaga cku nyingi!!hivi hajui check & balance_!!!hajui kuwa bunge ni mhimili unaojitegemea na wenye nguvu wa kuiadabisha serikali!!!sasa yeye kama anafanya kazi na serikali kuu c aende uko!!!mbona mahakama tunaona inavojitambua na ndio maana tunashuhudia sa hivi majaji wengi wakijiudhuru maana wanalazimishwa kufanya maamuzi ambayo sio mbadala na taaluma yao!!!_sasa hili jinga na nafiki linashindwa kujiamini na halijui linasimamia nini na lina nguvu kiasi gani!!! yaani ni ovyo kabisa!!!
 
Unaona mnavyokurupuka na kuchangia kwa mihemko. Magdalena Sakaya alichelewa kuingia Bungeni. Baadae alipata nafasi ya kupiga kura, na alipiga KURA ya NDIO.
Sasa ulichosema wewe c ndio mimi nilichosema, wale wabunge wote wanaomsapoti lipumba wamesema ndio, ukianzia huyo wa mtwara mjini. Wakati anaingia Magdalena sakaya mimi sikumuona wala kumsikia lakini nimesema hapo juu kwamba na yeye angekuwepo angesema ndio. Na nashukuru umekuja kunithibitishia kwamba sakaya alivyokuja kasema ndio. Umepata majibu hapo
 
bora tu kujiweka kando na maswala ya kusikiliza bunge......sometime najikuta napata wasiwasi na baadhi ya wabunge kwene swala la uelewa.....bunge lipo kama mpira wa yanga na simba duh....very shameful
 
Kuna kitu ambacho sipika anapaswa kukielewa, kwanza pesa za maendeleo zinapelekwa kwa wananchi woote wenye vyama na wasio na vyama watoto na wakubwa, pili wabunge ni wawakilishi wa wanachi kwa makundi niliyoyataja hapo juu, tatu pesa za maendeleo siyo hisani ya serikali kwa wananchi bali ni wajibu, nne pesa za maendeleo ni kodi za wananchi wooote wa majimbo yoote, tano wabunge wa upinzani wanahaki ya kuamua kura yao waipige upande upi....... Mwisho nimkumbushe bajeti ya 16/17 ilikuwa 29 tr lkn pesa za maendeleo zilizotolewa ni chini ya 48% licha ya kupitishwa kwa mbwembwe na wabunge wa ccm......
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom