Kura ya hapana yaibua mjadala upitishaji bajeti ya Serikali

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,289
2,000
Kauli ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kwamba waliopiga kura ya hapana wakati wa kupitisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18 wasipatiwe fedha na mawaziri kwa ajili ya miradi imeibua mjadala bungeni.

Aliyeanza kuhoji kuhusu kauli hiyo leo (Jumanne) ni Joseph Mbilinyi maarufu Sugu aliyetaka mwongozo wa spika kuhusu kauli yake.

James Mbatia, amesema ni bora kufanyike mabadiliko ya Katiba ili kuwe na chama kimoja kama Bunge haliruhusu mawazo tofauti.

David Silinde amesema kauli zinazotolewa zinaweza kulipasua Taifa, hivyo kuwataka wabunge kutojenga Taifa ambalo wanaweza kulipasua wenyewe.

Mchungaji Peter Msigwa amesema wapinzani hawako bungeni kwa bahati mbaya na kwamba waliowachagua wanajua misimamo yao, hivyo wanapopiga kura ya hapana si kwamba Serikali ipeleke fedha kama hisani kwa kuwa ni fedha za walipa kodi.

Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amesema dunia imebadilika na kwamba zamani bajeti haikuwa shirikishi lakini sasa wabunge wanashirikishwa tangu mipango na maoni ya pande zote huchukuliwa kwa hiyo inashangaza kukataa.

Spika amesema upinzani si wa kusema hapana kwa kila jambo hata pale unaposhiriki na kwamba, unaposema sitaki halafu ukamfuata waziri kwa ajili ya fedha za miradi ataangalia akusaidie vipi. Amesema hapo baadaye itabidi kuangalia namna ya kufanya
 

Mshuza2

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
7,782
2,000
Nilikua naangalia bunge kipindi wanapiga kura za wazi kuna mbunge mmoja akawa anasifiwa na kina mama kwamba yeye ndio mwanaume kwa vile tu kasema ndio...
 

chinembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
5,559
2,000
Wabunge wa ccm wanasahau kwamba kuna watu katika majimbo ya upinzani walimpigia Magufuli kura hivyo anawajibika kuwaletea maendeleo

Pia katika uchaguzi mkuu,anayeulizwa maswali kitaifa ni rais kwa kuwa huwajibika kutembelea maeneo yote ya ccm na upinzani kuomba kura

Na pia ndani ya majimbo ya upinzani kuna baadhi ni madiwani wa ccm na baadhi wa upinzani

Na katika mgawanyo wa kura katika majimbo,tofauti ilikuwa mdogo kati ya upinzani na ccm,sasa sijui watawatenganisha vipi

Na pia hayo majimbo ya upinzani kuna mtawanyiko kimakabila,ukiwatenga watatuma taarifa mikoani kwao na kueneza chuki dhidi ya ccm
 

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,486
2,000
Ndugai amekuwa wa hovyo hovyo sana...


Kama walikuwa hawataki kura ya "HAPANA" kwanii waliitisha kupiga kura... Si wangepitisha tu kwakuwa uwezo huo wanao.CCM wanaongoza na ni mabingwa wa Unafiki.Ndugai na maCCM wenzake wanapaswa kujua kuwa hizo fedha hawatuletei kama fadhila bali ni haki zetu....
 

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,486
2,000
Nilikua naangalia bunge kipindi wanapiga kura za wazi kuna mbunge mmoja akawa anasifiwa na kina mama kwamba yeye ndio mwanaume kwa vile tu kasema ndio...
Mwanaume wa kweli anapinga panapofaa kupinga na kuunga mkono panapofaa kuunga mkono.......


Mwanaume wa kweli hana maisha ya Kinafiki nafiki...........
 

mluguru002

Member
Jun 11, 2017
25
45
Nilikua naangalia bunge kipindi wanapiga kura za wazi kuna mbunge mmoja akawa anasifiwa na kina mama kwamba yeye ndio mwanaume kwa vile tu kasema ndio...
Yule ni mbunge wa mtwara mjini ambaye anamspoti lipumba kwahiyo alifanya kwa maana. Nilitegemea hata kwa mama wa jimbo la kaliua Magdalena sakaya angesema ndio kwa bahati mbaya hakuwepo.
Miaka 50 ya Uhuru lakn bado bunge linaendeshwa utafikiri kikao cha dhalura cha chingaaz pale kariakoo!
 

Panda II

Senior Member
May 25, 2017
167
500
Hata kwenye madini walisema ndioooo alafu leo wanawabebesha mzigo wapinzani ndio maana huwa nikivaa nguo ya kijani watu wananishangaa kama nimevaa chupi kichwani kwa sababu kuwa CCM lazima uwe chizi kwanza
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom