Kura ya HAPANA Katiba Mpya, itaenda sambamba na kuing'oa CCM Serikali za Mitaa, Uchaguzi Mkuu

CHADEMA

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
490
2,471
CHADEMA kimewaambia wananchi kuwa kura ya hapana kuikataa Rasimu ya Katiba Mpya ambayo itakuwa imechakachuliwa kwa kuweka kando maoni ya muhimu ya wananchi waliyowasilisha kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba, itakuwa ni maandalizi ya kupiga kura ya kuking'oa CCM madarakani kuanzia kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa mwaka kesho, ili wananchi waweke madarakani uongozi utakaoandika Katiba Mpya kwa kuheshimu maoni ya wananchi wenyewe.

Kimesema kuwa CCM kimejiandaa kwa mbinu za hila, kuondoa maoni yote ya muhimu ambayo yangeleta mabadiliko kwenye maisha ya wananchi, ikiwemo UWAJIBIKAJI, UWAZI NA UADILIFU, kisha kinapenyeza mambo ambayo kinataka yaendelee kama yalivyo leo ambayo yataendelea kulea ufisadi na mafisadi, ubadhirifu na usiri.

[video] CHADEMA 2, Kibaha, Kongowe - YouTube[/video]
 
hatuna vitambulisho vya kupigia kura,sasa tutapigaje kura,,,tutawatoaje,,,cdm kuna wakati makao makuu you let us down,,,,,vijana tumemaliza form four tangu 2010 had
2013,,,wapo wengine wengi wamepata Elim ya uraia wanataka kupoga kura,sasa wapigaje,,,,,,
kwa nini hili suala. mnalisahau kwenye baadhi ya mikutano kuongelea,,,,?????
 
ccm watafanya hila kwenye daftari la mpiga kura..hapo vijana wengi watanyimwa haki yao ya kupiga kura na ndipo moto kama wa misri utakapoanza kuwaka.
 
Sisi wengine huku chini tunaipigania cdm kweli..bila hata kutumwa wala kuambiwa na mtu..lakini kusema ukweli mkuu huko juu..mnatuangusha..hizo kura zinapigwa vipi nawakati hamna juhudi kuanzia juu za kuandaa base ya wapiga kura..inatakiwa cdm ishinikize daftari la wapigakura liboreshwe..alafu na chadema ni msingi..itumike kuandaa hiyo base ya wapigakura..kuna maeneo kama arusha, kilimanjaro, mwanza(sio maeneo yote), musoma , iringa mjini, mbeya mjini, kigoma( nccr n cdm), na baadhi ya maeneo ya singida .. Ndo cdm angalau ina uhakika wa kura 60% lakini maeneo mengine kura si za uhakika...mnaona tabia za watanzania wakienda ccm wnashangilia wakienda cdm wanashangilia..sasa mbona hamna effort ya viongozi wa juu..kutumia advantage ya vijana kuikubali cdm kutengeneza base ya wapiga kura...movement fo change..utapateje mabadiliko(change) bila kuwa na wapiga kura... Kama ni ubaya wa ccm, ufisadi, usanii watu sasa hivi wanajua hasa vijana...sasa hivi kinachotakiwa kuongelewa ni kura..kupiga kura.. Kulinda kura.. kura inadhamani gani..kwa nini kijana aache kuendesha boda boda yake akapige kura..kura inamaanisha nini kwa cdm na mustakabali wa taifa..
cc: tumainimakene
 
Kauli za CHADEMA na UKAWA zimeanza kutofautiana!.

UKAWA wanasema hawawezi kurudi kwenye bunge la Katiba na bila wao kuwepo kwenye bunge la Katiba, wabunge waliobaki hawawezi kufanikiwa katika zoezi la kuboresha, kurekebisha au kufuta kifungu chochote cha Rasimu ya Katiba.

CHADEMA wao wanasema zoezi la kuboresha, kurekebisha na kufuta kifungu chochote litafanikiwa hata bila kuwepo UKAWA lakini litakataliwa na wananchi katika hatua ya mwisho ambayo ni kura ya maoni.

Hoja ya CHADEMA ni kama ya kinajimu. CHADEMA inawapangia wananchi watakachokisema kwenye kura ya maoni kama vile wananchi hawajitambui. Watanzania wanajitambua vizuri ndiyo maana kwa mamilioni wameendelea kujitokeza kupiga kura na kuwachagua viongozi wanaowataka katika maisha yao nani wananchi hao hao waliwachagua wabunge wengi wa CCM kuwa wawakilishi wao kutokana na sera na Ilani ya Uchaguzi ya chama walichokuwa wanakiwakilisha katika uchaguzi.

Bunge la Katiba haliundwi pekee na Wabunge kupitia vyama vya siasa. Kuna kundi la wabunge 201 katika bunge la Katiba ambao hawana affiliation na vyama vya siasa, kwa maana kuwa siyo wote waliobaki kwenye bunge la Katiba ni wanasiasa.
 
ccm watafanya hila kwenye daftari la mpiga kura..hapo vijana wengi watanyimwa haki yao ya kupiga kura na ndipo moto kama wa misri utakapoanza kuwaka.
Watu wa cdm tuache siasa za ajabu..mambo ya misri bongo tunajua hayawezi tokea..ila tushinikize cdm nayo itengeneze base ya wapiga kura..cdm ianze kukomaa na elimu kuhusu kura.. Kuanzia imuhimu wake, kutake advantage ya vijana wanaoikubali cdm kuandaa wapigakura.. Kuhamasisha hao vijana wakajiandikishe..kuhamasisha uandikishwaji wa daftari jipya..mm najiuliza kwa nini cdm haiweki mkazo na shinikizo kwenye maswala ya kura..inabaki inalilia na ccm tu..cdm ina network inaitwa cdm ni msingi..kwa nini isitumie hiyo network
 
Kauli za CHADEMA na UKAWA zimeanza kutofautiana!.

UKAWA wanasema hawawezi kurudi kwenye bunge la Katiba na bila wao kuwepo kwenye bunge la Katiba, wabunge waliobaki hawawezi kufanikiwa katika zoezi la kuboresha, kurekebisha au kufuta kifungu chochote cha Rasimu ya Katiba.

CHADEMA wao wanasema zoezi la kuboresha, kurekebisha na kufuta kifungu chochote litafanikiwa hata bila kuwepo UKAWA lakini litakataliwa na wananchi katika hatua ya mwisho ambayo ni kura ya maoni.

Hoja ya CHADEMA ni kama ya kinajimu. CHADEMA inawapangia wananchi watakachokisema kwenye kura ya maoni kama vile wananchi hawajitambui. Watanzania wanajitambua vizuri ndiyo maana kwa mamilioni wameendelea kujitokeza kupiga kura na kuwachagua viongozi wanaowataka katika maisha yao nani wananchi hao hao waliwachagua wabunge wengi wa CCM kuwa wawakilishi wao kutokana na sera na Ilani ya Uchaguzi ya chama walichokuwa wanakiwakilisha katika uchaguzi.

Bunge la Katiba haliundwi pekee na Wabunge kupitia vyama vya siasa. Kuna kundi la wabunge 201 katika bunge la Katiba ambao hawana affiliation na vyama vya siasa, kwa maana kuwa siyo wote waliobaki kwenye bunge la Katiba ni wanasiasa.
Na wewe ni mtupu sana..katiba ni tendo la maridhiano katika nchi..hamwezi mkaandika katiba huku mko vipande
vipande..nchi itaparaganyika..wakati mwingine uccm na ucdm ukizidi sana inakuwa ni ujinga
 
hatuna vitambulisho vya kupigia kura,sasa tutapigaje kura,,,tutawatoaje,,,cdm kuna wakati makao makuu you let us down,,,,,vijana tumemaliza form four tangu 2010 had
2013,,,wapo wengine wengi wamepata Elim ya uraia wanataka kupoga kura,sasa wapigaje,,,,,,
kwa nini hili suala. mnalisahau kwenye baadhi ya mikutano kuongelea,,,,?????
Sio mikutano mkuu..hii inafaa sasa ndo kuwa ajenda sasa hivi..kama ni ubovu wa ccm wananchi hasa vijana washajua vzr..sasa hivi nguvu ni kuelekeza kwenye kura..kujua zikowapi na watazipataje..?!...kwani unafikiri chalinze na iringa nini kilitokea..cdm tumefanya kampeni nzuri..lakini siku ya kupiga kura vijana wanayoiunga mkono cdm hawakupiga kura...wengi hawana shahada au hawapo kwenye daftari..unategemea unashinda vipi hapo..cuf si wajinga znz wanajua kabisa wanakura ngapi..wanajua kabisa nyumba ile na ile na ile tuna kura ngapi..mm nasema kama cdm wataendelea kupuuza hili la wapiga kura (kuacha kuandaaazingira mapema)..watashidwa uchaguzi(chaguzi zijazo vibaya mno)..hata hiyo kura ya maoni...
 
Tujiulize kwanza Tume ya Warioba ilikosea wapi mpaka CCM wakaja na rasimu yao? Basi na vyama vingine viandae rasimu zao ndio mwezi wa nane zikajadiliwe! Hutana uongozi bora katika nchi hii. Hivi wale wazee waadilifu wote wameshatangulia mbele za haki?
 
Kwani UKAWA imekufa? Maana siku hizi kila chama kinatoa matamko ambayo hayajapata ridhaa ya UKAWA
 
Ili tushinde hila za ccm kwa sasa tuanze kuhimiza watu wajitokeze kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura,
 
Na wewe ni mtupu sana..katiba ni tendo la maridhiano katika nchi..hamwezi mkaandika katiba huku mko vipande
vipande..nchi itaparaganyika..wakati mwingine uccm na ucdm ukizidi sana inakuwa ni ujinga
Unachangia hoja na kumjibu mtu mtupu sana ukitegemea atakuelewa?. Huoni kuwa wewe ndiyo una tatizo katika fikra.

Wewe umeona tatizo la chama liko kwangu pekee wakati aliyeleta hoja ya Katika ni CHADEMA. Hivi Unadhani CHADEMA ni charity au non-governmental organization (NGO)!.

Bora angalau hoja ya Katiba ingeletwa kwa kutumia nembo ya UKAWA ambayo kuna watu ndani yake ambao siyo wanasiasa.
 
Wewe akili yako imezeeka Kama Avatar yako,kwani unashindwa kusoma na kuelewa nini kimeandikwa
 
Na wewe ni mtupu sana..katiba ni tendo la maridhiano katika nchi..hamwezi mkaandika katiba huku mko vipande
vipande..nchi itaparaganyika..wakati mwingine uccm na ucdm ukizidi sana inakuwa ni ujinga
Bora tu tuufute kabisa mchakato huu wa katiba mpya ili isiwe sababu ya Watanzania kufarakana
 
kila mwananchi yuko tayari kwenda kuandikishwa kwenye daftari la kupiga kura,tunasubiri kwa hamu na huo utakuwa mwisho wa ccm kwani vijana wengi wamenyimwa haki ya msingi ya kipiga kura muda mrefu sana,wakati umefika na hakuna pa kukwepea hili
 
Kauli za CHADEMA na UKAWA zimeanza kutofautiana!.

UKAWA wanasema hawawezi kurudi kwenye bunge la Katiba na bila wao kuwepo kwenye bunge la Katiba, wabunge waliobaki hawawezi kufanikiwa katika zoezi la kuboresha, kurekebisha au kufuta kifungu chochote cha Rasimu ya Katiba.

CHADEMA wao wanasema zoezi la kuboresha, kurekebisha na kufuta kifungu chochote litafanikiwa hata bila kuwepo UKAWA lakini litakataliwa na wananchi katika hatua ya mwisho ambayo ni kura ya maoni.

Hoja ya CHADEMA ni kama ya kinajimu. CHADEMA inawapangia wananchi watakachokisema kwenye kura ya maoni kama vile wananchi hawajitambui. Watanzania wanajitambua vizuri ndiyo maana kwa mamilioni wameendelea kujitokeza kupiga kura na kuwachagua viongozi wanaowataka katika maisha yao nani wananchi hao hao waliwachagua wabunge wengi wa CCM kuwa wawakilishi wao kutokana na sera na Ilani ya Uchaguzi ya chama walichokuwa wanakiwakilisha katika uchaguzi.

Bunge la Katiba haliundwi pekee na Wabunge kupitia vyama vya siasa. Kuna kundi la wabunge 201 katika bunge la Katiba ambao hawana affiliation na vyama vya siasa, kwa maana kuwa siyo wote waliobaki kwenye bunge la Katiba ni wanasiasa.
Haujui chochote katika maisha ya mtanzania hauna shule wala nini ndio mahana unapiga kelele ili upate buku 7
 
Bora tu tuufute kabisa mchakato huu wa katiba mpya ili isiwe sababu ya Watanzania kufarakana
Wewe dada yangu usijiangarie angaria jinsi familia yako inavyoshinda na njaa.lakini sawa kwasababu huna elimu yoyote na bora hufanye hivyo.buku 7
 
Back
Top Bottom