Jamani hali ya hewa ni mbaya sana kwa sisi m hata vijijini. Hivi sasa nipo Kagera kwenye msiba na nipo eneo linaitwa Izibya ni Bukoba vijijini. Hapa ni usiku na tupo watu wengi kulala hapa msibani na umetokea mjadala mkali sana kuhusu hali ya uchaguzi upande wa urais na sisi m wakasema wana hakika watashinda. Hawa ni vibosile wenye pesa yao mzuri na baada ya ubishi mkubwa mwisho ikalazimika kwamba zipigwe kura za siri ili kuthibitisha kama ni kweli sisi m itashinda. Mara ukaandaliwa uchaguzi kwa taratibu ambazo wote tumekubali ulikuwa huru na haki. Jamani kumbe hatuna haja ya REDET kabisa maana umefanyika uchaguzi wa siri kabisa na matokeo yametoka hivi:
Kikwete kura 8;
Dr Slaa kura 48;
Lipumba kura 4;
Wagombea wengine hawakupata kitu.
Hii imenishitua kabisa maana hapa ni mbali sana na mji na wala hakuna mtandao wa internet kama wa JF, lakini watu wanafahamu watampigia nani kura. Kwa wale wakazi na watu waliowahi kutembelea wilaya ya Bukoba wanapafahamu. Jamani, Kikwete afanye packing ya mizigo yake maana after 31.10 hatakuwa rais wetu tena. Nimefurahishwa sana na misimamo ya wanavijiji na nimefuta ile dhana kuwa kura za sisi m zitatoka vijijini.
Habari ndio hiyo. Kwa herini.
Rafiki yangu ww naona sasa unatupeleka dunia nyingine kabisa unalinganisha Utafiti wa kitaasisi na kura zinazopatikana katika mabishano kwenye msiba!!!?????.
My take
Chadema could take any reporting not in their favour by various institutions as a challenge regardless of whether it is objective or not. That way they can build a stronger party to be depended as an alternative party in the country. Otherwise wasipoteze muda kusikiliza maelezo ya mtu mmoja mmoja humu JF wakadhani tayari wameshinda. I think they need to do more homework than that, winning is not that simple, this country is geographically big, The country has wider varieties of people with different ways of perceiving things and thinking. YES we have to build a democratic country but that needs people to work even harder