Kura nyingine za maoni hizi hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kura nyingine za maoni hizi hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kaa la Moto, Oct 9, 2010.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Jamani hali ya hewa ni mbaya sana kwa sisi m hata vijijini. Hivi sasa nipo Kagera kwenye msiba na nipo eneo linaitwa Izibya ni Bukoba vijijini. Hapa ni usiku na tupo watu wengi kulala hapa msibani na umetokea mjadala mkali sana kuhusu hali ya uchaguzi upande wa urais na sisi m wakasema wana hakika watashinda. Hawa ni vibosile wenye pesa yao mzuri na baada ya ubishi mkubwa mwisho ikalazimika kwamba zipigwe kura za siri ili kuthibitisha kama ni kweli sisi m itashinda. Mara ukaandaliwa uchaguzi kwa taratibu ambazo wote tumekubali ulikuwa huru na haki. Jamani kumbe hatuna haja ya REDET kabisa maana umefanyika uchaguzi wa siri kabisa na matokeo yametoka hivi:

  Kikwete kura 8;
  Dr Slaa kura 48;
  Lipumba kura 4;
  Wagombea wengine hawakupata kitu.

  Hii imenishitua kabisa maana hapa ni mbali sana na mji na wala hakuna mtandao wa internet kama wa JF, lakini watu wanafahamu watampigia nani kura. Kwa wale wakazi na watu waliowahi kutembelea wilaya ya Bukoba wanapafahamu. Jamani, Kikwete afanye packing ya mizigo yake maana after 31.10 hatakuwa rais wetu tena. Nimefurahishwa sana na misimamo ya wanavijiji na nimefuta ile dhana kuwa kura za sisi m zitatoka vijijini.

  Habari ndio hiyo. Kwa herini.
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Saa ya ukombozi imewadia,EE mola utuongoze tuweze pata Kiongozi anayekerwa na umaskini wetu
   
 3. P

  Paul S.S Verified User

  #3
  Oct 9, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Amahakika chadema mmepata kijiwe kizuri cha kujiliwaza, yaani mtu akifikiria chochote tu anaandika ilimradi kitawafurahisha wenzake, nawachangiaji wataunga mkono hata iwe upupu gani
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Tutafute njia ya kufichua njama za sisi m kuchakachua matokeo ya uchaguzi. Ndicho kilichobaki.
   
 5. G

  Genda Member

  #5
  Oct 9, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sikatai kuwa mlipiga kura na kusahau hayo ya mazishi!

  Lakini hiyo kura..external reliability yake ikoje? Je, tunaweza kuisambaza kwa Tanzania nzima na kutamati kuwa Slaa atashinda?
   
 6. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  vipi kama ile ya REDET? iko safi eee au ndiyo yale yale ya chenu keki na chetu kinyesi?
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Chukua polls zote unavyofikiri pamoja na hii ya REDET mnayoamini sisi m maana hao hamuwahoji maswali haya. Kisha amua mwenyewe. Subiri tarehe 31.10 uone ukweli. Mimi nakuletea live kutoka kwenye tukio kupitia LT yangu.
   
 8. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ndiyo ile misiba ambayo kila siku mnamalizaga gari zima la bia?

  Hatudanganyiki lakini kudanganya kama kawa! Teh teh teh!
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hapo sasa. Ubishi kama huu ndio umetufikisha kupiga kura zile.
  Hata kama utatofautiana na wa Moro, Singida au Dodoma. Lakini nikilinganisha na hizi polls zingine ambazo hata REDET wachakachuaji wamekili jamaa ana kasi isiyo ya kawaida, ninawiwa kukubali kuwa kuna mabadiliko mbele yetu.

  Tatizo lilianzia pale watu wengi waliponyamaza na kutoonyesha msimamo wao wale wa sisi m wakadhani silence means wako upande wao. Na wao ndio wameshinikiza ipigwe kura kwa wote waliokuwepo. Matokeo ndio hayo. Utajaza mwenyewe......
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Angalieni wakati wa kutangazwa matokeo msijeanguka kwa shock wote. Maana hivi tu mmeshaanza. Hivi karibuni na Masha pressure juu kaanguka sasa yuko uerope kutibiwa. Nawahurumia sana
   
 11. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu hukutakiwa kuwa na dhana hii kwa watu wa nje ya miji. ukweli watu wanataka mabadiliko zaidi ni wa vijijini. Sample angali wabunge wengi wa upinzani tanzania bara wanatoka majimbo gani Sio musoma bali tarime, Cheyo aliwai kushinda Magu nk.

  Binafsi mi nadhani sisi wa mjini huw ndo tunajidai wasomi na tunajua siasa lakini hatuendi kupiga kura na tunaona kupnga foleni ni usumbufu.
   
 12. N

  Njaare JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mchukia Fisadi Kwanza pole na msiba. Asante sana kwa kutuletea matokeo mazuri kabisa ya kura za maoni.

  Mimi tu ninalotaka kukujulisha ni kuwa sii kweli kuwa CCM wanapata kura nyingi vijijini ila vijijini ni rahisi kuiba kura. Watu wa vijijini walishaichoka CCM miaka mingi na kama bado uko hapo hebu uliza wanachama wa CCM ni wangapi halafu waulize kadi mara ya mwisho walilipia lini.

  Kama tukiwa na utaratibu mzuri wa kulinda kura CCM haipati hata asilimia ishirini.
   
 13. T

  Time4change Member

  #13
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi kubwa iliyobaki ni kuelimisha watanzania walio wengi kuwa CCM ilfariki na Mwalimu. Kilichobaki ni usanii wa Vuvuzela. Kipindi cha kampeni ni kipindi cha kutoa hoja za msingi na kuruhu mijadala ya kuuza sera. Wapiga kura wanataka kufahamu, tena ni haki yao, kwa nini hata baada ya miaka takriban 50 ya uhuru kuna watu ambao bado hawana vyoo. Sisemi rais akachimbe choo, bali watendaji wake kuanzia ngazi za chini wawajibishwe. Tunahitaji mabadiliko. Bila shaka hata hawa ndugu zatu wa Bukoba vijijini wameona hilo.
   
 14. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2010
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kwanza nitakuomba utume salamu ,ukisha maliza kutuma salamu chaguwa wimbo.
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Naona ki LT changu kinaishiwa charge maana huku umeme ni hadithi ingawa nasikia Kikwete eti kawapa ahadi kuwa atawakumbuka katika miaka mitano ijayo. Ngoja nikapumzike. Kwa wale wasiojua hili ndilo lilikuwa jimbo la Karamagi bwahahahahahahaha
   
 16. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,461
  Likes Received: 789
  Trophy Points: 280
  CCM bila Mwalimu Julius Nyerere ni sawa sawa na kumtafuta paka mweusi kwenye giza totolo na hali hayupo.
   
 17. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Wakuu amini msiamini huku sukumaland vijijini watu wanasema Kikwete hajawafanyia kitu kwahiyo hawamchagui nasema kweli. Kwahiyo mwaka huu ni kweli Kikwete awe muungwana tu aache wananchi waamue nani wanataka awe rais wao naye aachie nganzi kwa amani na kwahilo ataheshimika na jamii ya watanzania na kuipatia sifa Tanzania katika duru za kimataifa. Maana anachopanga kufanya ni kama kile cha Zimbabwe cha Mugabe kutumia jeshi kutwaa madaraka kwa nguvu. Kikwete kuwa muungwana waache wananchi wachague rais wanayemtaka, wakikuchagua basi shauri yao wenyewe.
   
 18. R

  RMA JF-Expert Member

  #18
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr Slaa yes we can! :llama::decision::preggers:
  Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.


  Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupunguzwa kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili ajibu bila unafiki!


  Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendelee kuwa watumwa ni nini? :llama::smow: :blah:

  Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni sawa na tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo lukuki zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata moja haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini, wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado! Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na vikofia za njano. Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni sehemu ya maisha yao. Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..


  Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na Tanzanite. CCM wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na wameruhusu wizi huo. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shilingi 350.000 achana na longolongo za CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji yao.


  Ni Dr. Slaa ambaye amepanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba anapewa mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa sheria uko wapi?


  CCM hawawezi hayo? Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake. Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo! :llama::smow: :moony:


  Ni Dr Slaa anayeweza kufanya hayo. Nani anabisha! Si tumeona alivyowataja mafisadi wote! hapo akiwa ni mbunge tu! Je akiwa rais si watakimbia nchi? Jamani nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupushe muone moto utakavyowaka.. Tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata madawati. Jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekalia mawe? We must be serious!


  Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo botswana kwa sababu ya maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao? Nani asiejua asilimia 85 ya watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu?


  Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi? Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?:llama::smow::blah:


  Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa, anaweza kutuvusha tulipo. Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito, maziwa, national parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini kila leo rais kuwaabudu wazungu na bakuli la kuombaomba! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania. Ee Mungu utuhurumie!


  Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja utakuta bado wanatumika kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache woga inawezekana! Mbona Kenya wameweza? Mbona malawi wameweza?Mbona zimbabwe wameweza? Mbona Ghana wameweza? Kufanya mabadiliko sahihi, inawezakana na nafasi ni hii tuitumie. :tonguez::llama::decision:


  Tumtume Dr Slaa atukurupushie wezi wote na atuwekee katiba sawa. Huo ndio msingi wa yote. Ni Dr. Slaa asiyeogopa kuwepo na mgombea binafsi. CCM hili hawaliwezi. Wamelipinga hadi mahakamani. Wanataka wao tu ndio waendelee kututawala na kutunyonya.

  Jamani 2010 hakuna kudanganyika! enough is enough. Acheni kudanganyika. Wakati ndio huu. Watanzania msipoamua sasa, mtamlaumu nani tena? Nawatamani watu wa kule Mara -hakuna kura inaibiwa. Zote zinasimamiwa. Tukibadilika inawezekana, tena ni rahisi.


  Peleka ujumbe huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Waambie Nyerere alikwishakufa na nchi imeishatekwa nyara na vibaka. Peleka ujumbe huu haraka kwa simu kama ipo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani ni hela..

  :tonguez::llama::smow:
   
 19. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Mkuu nakukubali kwa mawazo yako,
  Wengi wanafikiri vijijini hawaelewi, wakati ukweli ni kwamba vijijini wako serious kuliko mijini.

  Juzi nilikuwa kijijini kwwetu mkoani Manyara, watu wako wazi kuhusu wanataka kumpigia kura nani. Wengi wanataka kumpigia Dr Slaa na chama chake. Mijini kuna unafiki mwingi ukilinganisha na vjijini.
   
 20. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #20
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Hii imekaa vizuri, nitaprint then ntatuma nilikozaliwa, kuna vijana wanapiga photocopi jarida lolote linalozungumzia mageuzi. ntawatumia
   
Loading...