Uchaguzi 2020 Kura kwa mwananchi ni kuchagua Kiongozi mtenda haki na sio chama. CCM hawatendi haki

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,944
3,820
CCM haifai kupewa kura na wananchi,viongozi wa upinzani mujikite kuwaeleza wananchi kuwa CCM imekosa viongozi waadilifu,waambieni kuwa CCM imevamia polisi,majeshi na vyombo vyote vya ulinzai na usalama ikiwemo mahakama.

CCM inaingilia uhuru wa vyombo hivyo bila ya aibu mchana kweupe na kusababisha mwananchi kukosa haki yake kikatiba,tunasikia watu wanahojiwa uraia wao na vyombo visivyohusika hata kufungulia mashitaka.

CCM inawapora wananchi maeneo bila ya kuwatafutia maeneo mbadala kisa tu wanakuza miundo mbinu,unamhamisha mtu kwenye makazi nyumba, kinachotakiwa ni kujenga nyumba na kuwahamishia watu uliowahamisha katika makazi uliyojenga,mnabaki kukisia unampa mtu milioni x akajitafutie kiwanja na eneo na kujengea haya hayapo sehemu nyengine yeyote nje ya Afrika,tuikatae CCM.

ChADEMA wekeni ahadi hamtamhamisha mtu kwenye eneo kama hamjamjengea nyumba nyingine sehemu mnayoona au mtakayoitenga kwa ajili ya makazi mapya wakati sehemu zitakazoathirika kwa miundo mbinu,msimlipe mtu hela huo ni uonevu.

Haya mambo ya wizara ya ardhi kupatanisha serikali na wanavijiji ni uzandiki ambao matatizo yake hayaishi. CCM imekosa uongozi.

Kinachoonekana ni CCM kutaka kupigiwa kura ichaguliwe na mwananchi Mtanganyika asie na uelewa wa faida ya kura yake anaona mabazazi hawa ndio wa kuchaguliwa. Amkeni CCM mkiipa itawabakisha mifupa mitupu wakijua kila uchwao wananchi wanazidi kuamshwa.
 
Back
Top Bottom