Mkoba wa Mama
JF-Expert Member
- May 5, 2021
- 201
- 84
Utangulizi.
Kwa kuzingatia mazingira ya sasa, idadi ya watu inazidi kuongezeka kwa kasi kubwa na pia changamoto za kiafya zinazowakabili watu wengi hasa katika umri wa kuanzia miaka 50, kupunguza umri wa kustaafu kwa lazima kutaweka msingi imara kwa ustawi wa wastaafu, kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na kuongeza nafasi za ajira.
Sababu na faida za kuzingatia mabadiliko haya ni kama ifuatavyo:
Kuongeza nafasi za ajira kwa vijana na kuchochea mzunguko wa ajira:
Kutokana na changamoto iliyopo ya ukosefu wa ajira ambayo inatokana na ongezeko la wasomi nchini, kupunguza umri wa kustaafu kwa lazima kutawapa fursa zaidi vijana ambao wanatafuta ajira katika sekta mbalimbali. Vijana wanahitaji kuingia katika soko la ajira na kuchangia katika ukuaji wa uchumi, mabadiliko ya utendaji kazi kuwa wa kisasa zaidi hasa katika nyanja ya matumizi ya sayansi na teknolojia na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kutokana na kuwa na nguvu na uwezo wa kutosha wa kukamilisha majukumu ya kikazi pasipo kuchoka mapema wala kusumbuliwa na matatizo ya kiafya ya mara kwa mara. Kwa kuongeza nafasi za ajira kupitia kupunguza umri wa kustaafu, tutaziba pengo la ajira na kuwezesha kizazi kipya kuchukua usukani katika kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi.
Kuongeza ufanisi wa utendaji kazi:
Ni ukweli usiopingika kuwa ufanisi wa utendaji kazi wa mtu unapungua kadri umri unavyozidi kwenda, mtu mwenye umri zaidi ya miaka 55 utendaji kazi wake hauwezi kulinganisha na kijana. Hivyo, kumuacha kazini mtu mwenye umri zaidi ya miaka 55 ukizingatia pia mazingira ya kazi hasa ya nchi zetu zinazoendelea kuna hatari kubwa; kwanza, ni kuendelea kumchosha na kumchakaza yeye mwenyewe na pengine kuwa katika hatari ya kupata maradhi hasa yasiyo ya kuambukiza (shinikizo la damu, kupooza viungo vya mwili, msongo wa mawazo n.k), lakini pia kusababisha ufanisi wa utendaji kazi kuwa wa chini zaidi ukilinganisha na utendaji kazi wa mtu wa umri wa chini.
Kuwapa wastaafu muda mrefu zaidi wa kupumzika na kufaidi mafao yao:
Kulingana na takwimu za mwaka 2022, wastani wa umri wa kuishi kwa mtanzania ni miaka 65, kwa maana hiyo, kwa kuzingatia utaratibu uliopo sasa mstaafu ana wastani wa kuishi ili kufurahia matunda ya kazi yake na kufaidi mafao yake aliyochangia kwa zaidi ya miaka 30 kwa muda wa miaka mitano tu baada ya kustaafu.
Kwa kupunguza umri wa kustaafu, wastaafu watapata muda mrefu zaidi wa kupumzika na kufurahia matunda ya kazi yao na kufaidi mafao yao. Hii itawawezesha kujijengea maisha mapya baada ya kustaafu na kufurahia maisha ya kustaafu kwa amani na utulivu bila msongo wa mawazo na maradhi mbalimbali tofauti na mtu akistaafu umri ukiwa umeenda zaidi.
Kupunguza msongo wa kazi na mawazo kwa watumishi:
Kwa kustaafu mapema, mtumishi wa umma anaweza kupunguza msongo wa kazi na mawazo ambao mara nyingi huja na majukumu ya kazi. Hii inaweza kusaidia kuboresha afya yao ya akili na kimwili na kuwawezesha kufurahia maisha bila shinikizo la kazi.
Lakini pia kutokana na wasiwasi wa watumishi wengi kuhusu afya zao na ikiwa watastaafu na watapata mafao yao ya uzeeni umri ukiwa umeenda zaidi, husababisha watu wengi kusumbuliwa na tatizo la msongo wa mawazo kama wataweza kunufaika na mafao ya uzeeni wakiwa bado wapo hai au wakiwa bado na nguvu na afya njema au mafao yao watafaidi watu wengine wao wakiwa tayari wamechoka sana na uzee au pengine wamefariki.
Kulinda afya za watumishi na kuwezesha wastaafu kufurahia mafao yao wakiwa na afya njema:
Kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha uliopo sasa, watu wengi sana kuanzia umri wa miaka 50 wanakabiliwa na hatari ya kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza na wengine tayari wana magonjwa hayo.
Hivyo kuendelea na utaratibu wa umri wa lazima wa kustaafu kuwa miaka 60 ni kuendelea kuhatarisha maisha ya watumishi hasa wenye umri mkubwa na kupunguza ufanisi wa kazi kutokana na changamoto ya maradhi. Magonjwa kama vile kisukari, shinikizo la damu, kupooza viungo vya mwili na magonjwa ya moyo yamekuwa ni tatizo kubwa hasa kwa watu kuanzia umri wa miaka 50.
Kupunguza umri wa kustaafu kutatoa fursa kwa watumishi wenye magonjwa hayo kupata mda mwingi wa kupumzika na kufuatilia matibabu au kujiuguza kwa usahihi zaidi, kwa sababu magonjwa hayo yanahitaji ufuatiliaji wa karibu zaidi wa matibabu na huduma nyingine za afya. Lakini pia itasaidia ikiwa watastaafu mapema, kutumia mafao yao katika malengo yao waliyo nayo badala ya kutumia mafao yao kujiuguza na maradhi hasa ya uzeeni.
Kukuza ujuzi na ubunifu, kuongeza ufahamu wa teknolojia na mabadiliko ya kisasa:
Ni ukweli ulio wazi kuwa katika suala la ujuzi na ubunifu, vijana wana uwezo mkubwa zaidi ukilinganisha na wazee.
Wafanyakazi walio katika umri mdogo watakuwa na motisha ya kujifunza na kukuza ujuzi mpya ili kuboresha utendaji wao kazini tofauti na ilivyo kwa wazee. Hii itasaidia taasisi na mashirika kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuwa na ushindani katika soko.
Lakini pia, vijana ambao wanachukua nafasi za wastaafu wanaweza kuleta ufahamu mpya wa teknolojia na mabadiliko ya kisasa katika soko la ajira. Hii inaweza kusaidia kuboresha utendaji wa shirika au taasisi kwa kuzingatia mwenendo na mahitaji ya sasa ya kiteknolojia.
Kupunguza gharama zisizo za lazima kwa serikali:
Watu wenye umri zaidi ya miaka 55 wapo kwenye hatari ya kusumbuliwa na maradhi ya mara kwa mara, hii inapelekea kushuka kwa ufanisi kazini na kupunguza siku za utendaji kazi kutokana na maradhi, hivyo italazimu mtumishi apewe ruhusu na kujiuguza na kufuatilia matibabu.
Hivyo serikali kuingia hasara ya kuendelea kimlipa mshahara mtumishi ambaye haifanyi kazi kwa kiwango na mda unaotakiwa badala yake mtumishi huyu angestaafu na nafasi yake kuchukuliwa na vijana ambao bado Wana nguvu na afya njema ya kutekeleza majukumu kwa kiwango cha juu zaidi.
Fursa ya kujihusisha na shughuli mpya au biashara:
Kustaafu mapema inaweza kumwezesha mtumishi wa umma kujihusisha na shughuli mpya au hata kuanzisha biashara yao wenyewe. Wanaweza kutumia ujuzi na uzoefu wao kutengeneza njia mpya za kujipatia kipato au kuchangia katika jamii kwa njia mpya.