Kupunguza ukali wa gharama za maisha- wawakilishi wetu wamelala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupunguza ukali wa gharama za maisha- wawakilishi wetu wamelala

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kabathe, May 13, 2011.

 1. K

  Kabathe Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuna tatizo kubwa la viongozi katika nchi hii, hawa tunao wa chagua kuwa wawakilishi wetu bungeni sidhani kama kweli wanatuwakilisha. Kwani yapo matatizo ambayo yako wazi kwa kila mtu lakini wawakilishi wetu wamekaa kimya ama kwa kutojisumbua kufikiria au uwezo wao wakufikiria umefikia hapo.

  Hakuna asiyejua hali ngumu ya kimaisha inayomkabili Mtanzania kwa sasa, kila kitu kimepanda. Mfano ni bei ya mafuta, kwa kua hii ni bidhaa muhimu ktk uzalishaji ikipanda kila kitu kitapanda. Serikali kupunguza bei ya sukari kwangu mimi ni uwezo mdogo wa kufikiria, kwa anae pata mlo mmoja kwa siku sidhani kama anaitaji sukari, kunywa chai ni anasa kwa Mtanzania.

  Kama kweli unadhamira ya kusaidia PUNGUZA kodi kwenye mafuta na hapo kila kitu kitashuka ikiwemo na sukari.


  Napenda kuwapongeza CDM kwa kufanya maandamano ya kupinga kupanda kwa garama za maisha, lakini ya CDM yanapuuzwa na chama tawala kwa kigezo tu kwamba wanatafuta umaarufu wa kisiasa.

  Ili swala ili lisionekane la kisiasa kama kuna mbunge wa kuweza kufikiria, I know wako wachache sana angeandaa hoja binafsi ya kumtaka waziri wa fedha kupunguza Kodi katika mafuta. Hili linawezekana kabisa.


  Kwa wezetu Kenya walifanya hivyo, swala likajadiliwa bungeni na hatimae baadhi ya vitu vikashuka.
  Lakini tukisubiri uruma za bwana mkubwa tutakufa.

  Nawasilisha hoja.:A S 103:
   
 2. B

  Bendera ya bati Senior Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu lazima uelewe kuwa,most of our legislators ni Makhilikhili!!!
   
 3. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2011
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 483
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Then hiyo hoja ipeleleke pale kwenye mjengo wa ndio....
  Unafikiri nn kitatokea kama sio ban, sorry kufukuzwa kwa kupotosha mjengo.
   
Loading...