Kupunguza kuzeeka na kuwa na ngozi laini na changa

Magnificient

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
1,162
705
JINSI YA KUIFANYA NGOZI YAKO KUWA CHANGA NA KUPUNGUZA KUZEEKA

KUZEEKA KWA NGOZI NA JINSI YA KUPUNGUZA KUZEEKA
Kuzeeka ni utaratibu wa kawaida kwa mwili wa binadamu. Na hutokea kila siku kwa yeyote ambaye ameshafika umri wa utu uzima. Hakuna shida yoyote kwa mtu kuwa mzee isipokuwa kama mtu anapenda au anahitaji muonekano wa ujana – ngozi laini, nywele nyeusi nk

JINSI KUZEEKA KWA NGOZI KUNAVYOTOKEA
Kuzeeka kunatokana na kuharibika na kupungua kwa protini za ngozi zinazofanya kazi ya kuifanya ngozi iweze kukua, kuvutika na kutunza maji ya kutosha. Protini hizi huitwa elastin na collagen.
Protini hizo zikiharibika na kupungua ngozi hushindwa kukua, hushindwa kuvutika na hupoteza maji na matokeo yake huanza kufubaa, kuwa ngumu na kuwa makunyanzi.
Pia kushindwa kuvutika kwa ngozi ndio sababu ya mtu kuwa na michirizi.

JINSI YA KUPUNGUZA AU KUONDOA KUZEEKA KWA NGOZI
Kuzeeka kwa ngozi kunaweza kupunguzwa au kuondolewa kwa kuongeza uzalishaji na kiasi cha protini aina za elastin na collagen
Hilo linaweza kufanikishwa kwa vipodozi vya aina mbalimbali katika mfumo wa lotion, cream, mafuta na kadhalika
Hizi zitasaidia kuifanya ngozi kuwa changa na ya kuvutia kwa kuisaidia kukua, kuvutika na kutunza maji ya kutosha.

VITU GANI UTUMIE KUFANIKISHA HILI
Kuna bidhaa za aina nyingi na za kampuni mbalimbali za kuweza kufanikisha zoezi hili. Mfano wa kwanza ni vipodozi vyenye Vitamin A au mazao yanayotokana na Vitamin A (Lazima upate ushauri wa kitaalam ndipo uanze kutumia na zikusaidie vizuri)
Pia kuna vipodozi vyenye Vitamin E. Hivi navyo husaidia sana kuifanya ngozi kuwa laini na ya kupendeza, na kupunguza kuzeeka kwa ngozi.
Kitu cha muhimu ni kusaidia kuondoa ngozi iliyozeeka, kuongeza uzalishaji wa elastin na collagen na kuongeza maji na utunzaji maji katika ngozi (Moisturizer husaidia kukamilisha zoezi la kuongeza maji katika ngozi. Chagua iliyo bora kabisa na utumie).
Pia kunaweza kuwa na tofauti ya mahitaji ya bidhaa kati ya mtu na mtu, kwa hiyo ni vyema kila mtu kushauriwa kutokana na ngozi yake na mahitaji yake.
EPUKA VIPODOZI VISIVYO SALAMA NA VILE VISIVYOFAA KWA NGOZI YAKO. VINAWEZA VIKAKUHARIBU ZAIDI.

PATA USHAURI WA KITAALAM, BIDHAA BORA NA SALAMA NA MAELEZO ZAIDI
Kwa kupata maelezo zaidi, ushauri wa kitaalam na bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na usalama unaweza kuwasiliana na Washauri wa afya na wataalam wa urembo na vipodozi - S&E BEAUTY SOLUTIONS

S&E BEAUTY SOLUTIONS
TEMEKE BUZA BLOCK T PLOT No. 601
MASHINE YA MAJI NAMBA 5
DAR ES SALAAM
Simu : 0 659 528 724 , 0 784 082 847
Pia unaweza ukatembelea ukurasa wetu wa Facebook : S&E BEAUTY SOLUTIONS
E-mail : tecetra@gmail.com
 
Em tutajie Anti-aging creams nzuri, uzee ukianza tu nihamie huko
 
BAADA YA KUTUMIA VIPODOZI (LOTION, CREAM, MAFUTA NK) PUMZISHA NGOZI YAKO
Unashauriwa kuosha ngozi yako na kuondoa vipodozi vyako vyote (lotion, mafuta, cream nk) na kuiacha ngozi yako ikiwa free ili iweze kupumzika na kupumua vizuri. Osha kabisa vipodozi na uchafu wote utoke usoni au sehemu nyingine ya ngozi kisha baki hivyo kwa angalau masaa 6 kwa siku, either masaa 6 mfululizo au masaa 3 kutwa mara 2.
Ngozi yako itapata muda wa kupumua vizuri, kupumzika na kujijenga vizuri zaidi.

washing face 1.jpg
washing face.jpg
 
BAADA YA KUTUMIA VIPODOZI (LOTION, CREAM, MAFUTA NK) PUMZISHA NGOZI YAKO
Unashauriwa kuosha ngozi yako na kuondoa vipodozi vyako vyote (lotion, mafuta, cream nk) na kuiacha ngozi yako ikiwa free ili iweze kupumzika na kupumua vizuri. Osha kabisa vipodozi na uchafu wote utoke usoni au sehemu nyingine ya ngozi kisha baki hivyo kwa angalau masaa 6 kwa siku, either masaa 6 mfululizo au masaa 3 kutwa mara 2.
Ngozi yako itapata muda wa kupumua vizuri, kupumzika na kujijenga vizuri zaidi.

washing face 1.jpg
washing face.jpg
 
VITU VINAVYOHARIBU NGOZI ZETU

Ngozi zetu zimeundwa kwa chembe ndogo ndogo zinazoitwa seli, ambazo ni viumbe hai; yaani huzaliwa, hukua na kufa. Seli za zamani zinakufa na seli mpya zinazaliwa kila siku. Huu ni utaratibu wa kawaida na hutokea kila siku katika maisha yetu, na ni mwili wenyewe ndio unaoendesha na kusimamia utaratibu huu.

Ukiacha huo utaratibu wa kawaida wa seli za ngozi kuzaliwa, kukua na kufa kuna vitu vingine kutoka kwenye mazingira ambavyo huathiri utaratibu huo na kupelekea kudhoofika au kufa kwa seli zetu. Vitu hivyo vikitokea kwa kiasi kidogo hudhoofisha seli zetu, lakini vikiondolewa seli zetu hujijenga upya na kurudia hali yao ya kawaida. Vikitokea kwa kiasi kikubwa au kuendelea kuwepo kwa muda mrefu huzidhoofisha zaidi seli zetu na kuziua kabisa.

Vitu hivyo ni;

i. Msongo wa mawazo
ii. Jua kali
iii. Ukosefu wa mlo mzuri
iv. Kutokunywa maji ya kutosha
v. Kujichubua
vi. Umri mkubwa
vii. Uchafu
viii. Vipodozi visivyo salama
ix. Magonjwa na maambukizi
x. Kujeruhiwa

Matokeo yake ni ngozi kuharibika, kuwahi kuzeeka au kupoteza uzuri wake.
Tunaweza kutunza ngozi zetu ili ziwe nzuri na zidumu na uzuri wake kwa Kupumzisha mwili na akili zetu kiasi cha kutosha, kuepuka jua kali, kupata mlo kamili, kunywa maji ya kutosha, kutojichubua, Kusafisha vizuri ngozi zetu na kuondoa uchafu wote, Kutumia vipodozi bora na salama, Kuwa makini ili tusipate majeraha na kujikinga vizuri dhidi ya magonjwa na maambukizi.

PICHA ZA CHINI ZINAONESHA BAADHI YA VIPODOZI VISIVYO SALAMA NA VILIVYOPIGWA MARUFUKU TANZANIA.

UTACHUKUA HATUA GANI SASA ILI KUEPUKA NGOZI YAKO KUHARIBIWA?

Vipodozi vilivyopigwa marufuku 1.jpg
vipodozi visisvyo salama 2.jpg
Vipodozi visivyo salama 4.jpg
 
Na. (vi) tiba yake ni nini?
Kwa umri mkubwa na ngozi kuzeeka yenyewe automatically unaweza kuondoa ngozi iliyozeeka au kupunguza kasi ya ngozi kuzeeka. Hii hufanywa kwa kutumia vipodozi au dawa zinazoondoa seli za ngozi zilizokufa au kuzeeka na kuacha seli changa za ngozi. Pili hufanywa kwa kuchochea kasi ya uzalishwaji wa seli mpya za ngozi. Si unaona baadhi ya watu wenye umri mkubwa lakini hawataki kuzeeka wanavyong'aa mpaka leo?
 
Mbona dodo siioni hapo?
Dodo nayo pia imepigwa marufuku na sio nzuri kutumia. Hapo nimeweka baadhi tu, kama nilivyosema. Kwa msaada wa kuhakiki kipodozi chochote kama ni salama au sio salama, kimeruhusiwa au kimepigwa marufuku nk unaweza kuniuliza, nikakujibu na kukushauri kulingana na mahitaji yako.
Karibuni sana!
 
Mafuta aina ya Rinju na clere ni salama?
Rinju haina tatizo, ni salama na ni nzuri. Clere ni nzuri pia ni salama kwa hizi za kawaida ambazo si za kuchubua au kung'arisha rangi ya ngozi, lakini CLERE LEMON CREAM na CLERE EXTRA CREAM ni mbaya na zimepigwa marufuku na mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA). Zenyewe zina HYDROQUINONE, ambayo ni kiambata kibaya na kinachoweza kuharibu ngozi yako na kukuletea madhara mengine baadae. Hizo tusizitumie.
 
Walio na umri wa miaka 35 na kuendelea na anautayar wa kugharamikia ngoz yake kwa 240,000 anitafte nimpe set ya ecollagen, ni uhakika.. Ila usiwe na chunusi.. Kma unachunusi inabid kushughulikia hizo kwanza
 
Ngozi yangu ni ya mafuta,ni mweupe ila usoni si mweupe kama mwilini,sielewi nitumie lotion au creme gani ili inisaidie niwe kawaida,sasa hivi natumia orangevate gel nachanganya na coco pulp,nikiacha naharibika uso, naomba ushauri Niko arusha
 
Back
Top Bottom