Kupunguza kashfa ;mapadre wa kanisa la katoliki waruhusiwe kuoa; | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupunguza kashfa ;mapadre wa kanisa la katoliki waruhusiwe kuoa;

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Apr 22, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,521
  Likes Received: 5,752
  Trophy Points: 280
  Mapdre wakikatoliki wameombwa kupewa kibali cha kuoa baad ya matatizo yaliotokea
  huko nyumba kuhusu watoto.wakiongea kwa nyakati ttofauti wameomba uongozi wa kania katoliki kushirikiana na papa pope waokoe maisha ya watu hawa kwa kuwaruhusu kuoa
  Tatizo lililotokea si tamaa wale ni binadamu na unajua kuna wengine wameenda kwa sababu ya shidaso wabajua wakingia wanakula kuku na manyama ya bure na ukitoka zaidi maisha yanakuwa bomba sasa inafika wakati ana hamu kama mwanaume nini cha kufanya anaona wale vitoweo wa karibu ndio salale yao na hivyo kubeba dhambi wasizoziweza
  Askofu Pengo tunaomba wazo hili mliwakilishe kwa papa kabla ya mapdre awajavua nguo madhabahuni kukidhi hamu zao.......
  Naomba tusiwalaumu sana waseja wale hakuna sehemu kwenye biblia imeandikwa mtumishi wa mungu lazima uwe mwenyewe ndio utumikie vyema huu ni uharamia wa somalia auuna budi kupigwa vita..ndio maana kama mnajua vyema msiimbazi pata habari zake uone masister wanavyolambwa na wakuubwa mapadre zao huku wakiwapiga mikwara kutotoa mzigo nje

  Polen wakatoliki kwa kashfa hizi tuko nanyi pamoja
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Habari hii ni ya kipumbavu...i dont care anything about what mods may act on me!

  PDIDDY hauko sawa upstairs, na kazi yako ni COPY AND PASTE, ndio maana inapokuja kuandika kitu kwa akili zako unaandika MAJI-TAKA YA KWENYE SEPTIC TANK.

  HAYA mambo kuandika hapa unataka msaada gani...this is shiit!

  Usibuni mambo yasiyo na nucleus...use a head, not your genitals!
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,375
  Likes Received: 3,138
  Trophy Points: 280
  kuishi ni kuchagua...............inabidi wachague maisha wanayotaka kuishi........kama wanataka uchungaji na kuoa madhehebu yanayofanya hivyo yapo hivo waende.......la sivyo hiyo ni makusudi..............kumbuka hao ni watu 2 kati ya wale 100 sasa wasitupotezee muda ni bora kama umeshindwa ukaacha na kuwa muumini wa kawaida inawezekana walilazimisha kwa hiyo sio lazima wawe mapadre kwa hiyo waamue kuacha na kuwa waumini wazuri waoe wawaache walioitwa na mungu kikwelikweli...............
  tusipotezeane muda....
   
 4. B

  Baba Ubaya Senior Member

  #4
  Apr 22, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  PAKA Jimmy uko sawa Pdidy hakuna alichoandika hapo cha kuchangia haileweki kama ni ushauri au ombi by the way kanisa halilazimishi mtu kuwa padre ukiingia lazima ufate utaribu wao haijalishi kama uliingia kwa shida zako.
   
 5. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Madhehebu yanayoruhusu mtu kuhubiri neno la Bwana na akawa ameoa yapo mengi; anayetaka kuwa hivyo aende huko:
  Orthodox: ukioa utaweza tu kuwa mchungaji, ngazi zinazofuatia huwezi kuzipata hadi uwe hujaoa na usioe
  Madhehebu yaliyobaki waweza kuwa umeoa na ukapanda hadi cheo cha juu kabisa
  Hivyo wanaotaka kuoa wana wide choice. Wawaache wakatoliki na ukatoliki wao.
  Kuhusu maandiko kutozuia mapadre kuoa, soma biblia vizuri:
  Mtume Paulo anaeleza vizuri sana suala hili katika waraka1 kwa Wakorintho 7:1-9. Amechanganua wale wanaoweza kukaa bila kuoa wala kuolewa, na wale wasioweza kuwa hivyo kwa sababu ya tamaa zao, basi waoe au waolewe. Sasa ukichagua upadre maana yake umechagua kutooa -basi fuata masharti yake. Pia katika sura hiyohiyo ya 7:32-34 anaeleza uzuri wa mtu asiyeoa au kuolewa anavyoweza kumtumikia Bwana na namna yule aliyeoa anavyogawanya mapenzi yake! Padre anatakiwa asigawanye mapenzi yake kwa Bwana; amtumikie kikamilifu- siyo nusu kwa Bwana na nusu kwa mke, na pengine hata hiyo nusu nayo aigawanye pia kwa nyumba ndogo nk.
  kumbuka pia wale mitume aliowachagua Yesu, wale waliokuwa wameoa waliwaacha wake zao na mali zao zote wakamfuata - hivyo kanisa linachukua hali hii kwa kuwaambia wale wanaotaka upadre waachane na mambo yote ya dunia (mali, wanawake nk.)
  Msichanganyikiwe wasomaji: Ukisoma injili ya Mathayo sura 16:13-20 utaona Yesu alivyomkabidhi Petro kanisa na namna alivyo ahidi kumpatia funguo za ufalme wa mbingu; alivyompatia mamlaka ya kufunga chochote duniani na kikawa kimefungwa pia mbinguni na kufungua chochote duniani kikafunguliwa pia mbinguni. Kumbuka huyu ndiye Petro, papa wa kwanza; naye alikabidhi mamlaka hayo kwa papa aliyefuatia hadi sasa. Hivyo Papa akisema wanaotaka kuwa mapadre wasitake tena kuoa - basi, anayo mamlaka ya kufanya hivyo na mbinguni inakubalika.
  Nihitimishe kwa kuwaelekeza katika injili ya Yohana sura 21:15-17 alipomuagiza Petro kutunza kondoo wa Bwana. Hapa ndipo alimkabidhi rasmi yale mamlaka na majukumu aliyoahidi; period.
  Tunayo mifano mizuri tu, wengi mtakuwa mnamfahamu Privatus Karugendo - si ameoa na ana mtoto sasa! mapadre wanaotaka hivyo, wafanye kama huyo - si dhambi.
  Makosa kubwa yanayofanyika katika kanisa katoliki hivi sasa ni:
  1) Kuwapa upadre vijana wadogo, na
  2) Kuwaacha mapadre katika eneo moja kwa muda mrefu sana na hivyo kujijengea himaya fulani, na
  3) Kuwaruhusu kumiliki mali.
  Ni mali hizi zinazowazidishia tamaa kwani wanajikuta hawana namna ya kutumia mali hizi kwani mahitaji yote ya msingi wanapewa na kanisa!
   
 6. Fab

  Fab JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2010
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 763
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mnh pananoga
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Unashangaza sana wewe......una akili kweli mpaka ukaandika haya?
   
 8. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  tuna uelewa/upeo tofauti...hapa jamvini kama hujapenda sredi...ipotezee tu..usijibu jamani he! :confused3::rolleyez:
   
 9. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,653
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  "kania katoliki kushirikiana na Papaa Msofe" perhaps? Ulevi mtupu!
   
 10. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Sasa ndugu yangu tuseme mara ngapi kuhusu hili? Hivi unadhani KURUHUSIWA KUOA NDO KUWA MWAMINIFU? Mnawaombea waoe as if wamekuelezeni kuwa wanataka hayo na ndo dawa madthubuti. Nilishasema kwa kulinganisha kwamba je waliooa nao mbona siyo waaminifu walio wengi au nao waruhuriwe kuoa kama kumi na kuolewa na kumi? Suala kubwa ni kujenga conviction tu. Mlishafanya suala la mapadre kuoa kama breaking news kila anayekuja hayo hayo hadi hata hamu ya kuchangia imeniishia. Msiwachagulie maisha bwana. hebu jiulize, sijui kama mwenzangu umeoa au la na km umeoa jiulize mara ngapi umekwenda nyumba ndogo sijui kubwa. Na kama hujaoa jiulize umezivunja amri za Mungu wako mara ngapi kama una imani kwa Mungu. Sisemi haya kujastfy makosa bali nasema haya ili tujaribu kupendekeza njia thabiti ya kuleta amani lakini umeshupalia waoe as if mshagongana nao sehemu wakakuzidi kete!
   
 11. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hii sredi imekaa kichuki-chuki kabisa. Kaiandika kishabiki zaidi kuliko uzito wa hoja. Waache na maisha yao. Ujue kwamba wale wachungaji walio na wake zao hawako bora kuliko hao mapadre kwani wengi wao licha ya kuwa na wake zao lakini pia wana nyumba ndogo, nk. Ingekuwa shida ni kutokuwa na mke/mume basi hao wenye wake wasingekuwa na hizo nyumba ndogo. Lakini unakuta na wenyewe wamo tu. Utaelezaje hilo? Dawa si kuoa bali ni kutawala matamanio (concupiscence) na kuridhika na aina ya maisha mtu aliyoyachagua. Hili ni la lazima kwa wenye ndoa na wasio na ndoa (waseja).
   
 12. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Mimi nafananisha kisa hiki cha mapadre na harakati za wanawake za kudai usawa. Sababu swali kwao linakuja ni nani kawazuia fursa za ushiriki? Halikadhalika kwa mapadre ni nani kawazuia kuoa? Na je ana mamlaka hayo? Wanamtumikia Mungu au mtu? Na kama ni Mungu ni wapi Mungu alishawahi kuweka sharti la utumishi hasa kuhani kutooa? Ama katika kitabu cha mwanzo sura ya kwanza ni Mungu mwenyewe aliyeona ya kwamba sii vema mtu huyu yaani Adamu kuwa peke yake na hivyo akamfanyia msaidizi wa kufanana nae. Wala sii Adamu aliyeomba mke bali Mungu mwenyewe aliyemwumba ndie aliyeona ana haja hiyo. Sasa anapotokea mtu anasema ni sharti kutokuoa ili uwe kuhani ni mzushi. Paulo nae akitoa sifa za mtu anaepaswa kuwa askofu(kuhani) kuna sharti kuu kwamba mtu huyo lazima awe mwanamume wa mke mmoja tena mwenye uwezo wa kusimamia nyumba yake mwenyewe. Sasa unnapofanya kinyume chake unakumbana na uharibifu. Kuhusu maoni ya paulo kushauri mwamini kutooa au kuolewa hili lipo kwa yeyote mwenye uwezo wa kufanya hivyo kwa ajili ya Bwana na kamwe halikuwa na kusudio la sharti la mtu kuwa padre(mchungaji). Petro alikuwa na mke na wakati mmoja Bwana yesu alimponya mkwewe petro ugonjwa wa kuhara. Na hoja kwamba kuna walioacha wake kwa ajili ya Bwana haikumaanisha divorce kama baadhi ya watu wanavyoshawishi tuelewe bali ni mfano tu uliotolewa wa kumpenda Mungu kwanza kuliko vyote mtu anavyomiliki. Haiwezekani hata kidogo neno la Mungu lijipinge lenyewe, mahali pamoja paseme mke haachwi(divorcing) kwa sababu yeyote ila kwa uasherati na pengine paseme ni ruksa ku-divorce kwa ajili ya kumtumikia Bwana. Petro kukabiziwa mamlaka ya kufunga duniani na hivyo mbinguni likawa limefungwa maana yake hapo Petro alikabidhiwa neno la Kristo ambalo ni kristo mwenyewe na wala sii greeds na dogma maana zisinge-aply na angeitwa kahaba. Alichofanya petro kwa mara ya kwanza na funguo hizo ambazo ni neno kipo katika kitabu cha mitume 2:38 siku ile ya pentekoste 'Petro akawaambia,tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi, nanyi mtapokea kipawa cha Roho mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie' hivyo tu ndio neno linavyoweza kukufungulia mlango wa ufalme na kinyume chake ni neno hilo hilo linakufungia. Kuhusu kudhaniwa kwamba utume wa Petro unarisishwa kwa kura ni upotoshaji kwani mitume na manabii wa Mungu hawachaguliwi wala kuteuliwa na mtu
   
 13. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mmh me narudia tena.....hoja ya kuoa na kutokuoa haipo. walipokuwa ma padre wa kikatoliki walijua kuwa hawaruhusiwi kujamiiana na yoyote na walikbali hilo.
  sasa kwenda kulawiti watoto ni suala binafsi ambalo halihusiani na ukatoliki kwa kuwa sharti liliwekwa wazi mapema.
  hapa mie kwangu nalikosoa kanisa katoliki kwa kuwafichia madhambi yao hao waliolawiti watoto.....they should have known better kuwa hakuna siri ya milele.....sasa hii imekula kwao
   
 14. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  "Naomba tusiwalaumu sana waseja wale hakuna sehemu kwenye biblia imeandikwa mtumishi wa mungu lazima uwe mwenyewe ndio utumikie vyema huu ni uharamia wa somalia auuna budi kupigwa vita.."-PDiddy.

  Sa waungwana ni maoni gani ya chuki na shari haya!


  Kinachotakiwa ni kutoa ushauri na njia zozote zinazoweza kusaidia tatizo...na si kutanguliza maneno ya maudhi, ya kukandia....hii inaboa!
  We Pdiddy unaujua uharamia wa Somalia kweli?...au unauza sura kwa members?..Lete COPY &PASTE zako salama usiingilie mambo ambayo uko extremely-shallow nayo, na huwezi kuyasemea hata "A" yake.
  Kumbuka kanisa katoliki lina waumini wengi ambao ni innocent, sasa kujiongelea off-points kienyeji ni kuwapa wakati mgumu...Hii ishu iko katika ngazi za kushughulikiwa, na waliodhurika wame'lodge malalamiko yao kwenye ngazi-stahiki, sasa shida yako kubwa nini?..

  Tulia kaka, andika yanayokuhusu..pilipili usizozila hizo!
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  kuna nini hapa jamani?

  1. This message has been deleted by Brutus.


  2. Reason lugha mbofu mbofu
  <
  1. JF Senior Expert Member
  2. This message has been deleted by Brutus.

   Reason lugha mbofu mbofu
  <LI This message has been deleted by Fab.


   
 16. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu Pdidy
  koua sio suluisho kuna makanisa yaliruhusiwa koua watu wa jinsia tofauti lakini sasa hivi wanadai haki tena ya kuoana watu wa jinsia moja binadami haridhiki mkuu ukimpa kimoja atataka kingine
   
 17. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Brutus ni Super Moderator.....anajua vyema kazi yake bana...
  Big up Mods!
   
 18. bona

  bona JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  who is this prick! unatakiwa ujue kuwa padre hawaruhusiwi kuoa kanisa katoliki na pia kwa anayetaka kuoa nafasi ipo kulitumikia kanisa ktk vyeo vingine kama mashemasi, makatekista etc kwa iyo kanisa limekua fair kwa wote, upadre ni kwa wale waliofikia steji ya juu kabisa kumtumikia mungu kwa maisha yao yote ndio mana sheria ya kutokuoa ikawepo ili uyo mtu asiwe anasumbuliwa na familia nk yeye maisha yake yawe ni kwa mungu tu, kwa wale wenye imani haba na wanataka kuenjoy raha za tendo la ndoa na kumtumikia mungu pia chance zipo kama nilivyozitaja apo juu jamani.

  muandishi wa thread ii anaonekana ameiokota ii aidia sijui wapi, hata mapadre wanaujua ukweli uu kwa iyo wasingeweza omba kitu kama icho, hatuwezi fanya reform kwa wachache wanaofanya dhambi, basi si wanafunzi kule maboarding wanapenda kufanya mapenzi kwa kuiba, kwa nadharia yako ni kwamba waruhusiwe kukaa mabweni pamoja walale vitanda pamoja wapike na kupakua pamoja ili wasing'atwe na nyoka uko vichakani!
   
 19. Bright

  Bright Member

  #19
  Apr 23, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  PakaJimmy utakuwa haujavunja kweli taratibu za JF forum kwa lugha hiyo? You have attacked Pdidy's personality. I could not expect this from a premium member!
   
 20. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna double standards za hali ya juu hapa. Aliyoyaandika Pdidy yalionekana ni lugha mbovu na kufutwa lakini aliyoyaandika Paka ambayo ni matusi yameonekana hayana utata!
   
Loading...