Kupunguza faini kwa makosa ya bodaboda kuna faida au hasara?

SUTAGI-

JF-Expert Member
Nov 9, 2018
254
489
Siku moja niliwahi kushuhudia dereva boda akigongwa na gari wakati akiwakimbia Askari waliokuwa wanamkimbiza kutokana na makosa ya barabarani. Jamaa yule alipasuka kichwa palepale na ikawa mwisho wa maisha yake. Alikimbia faini ya shilingi 30,000 au zaidi akaambulia kifo..

Je, Kwa kuwa faini hiyo imepunguzwa na kuwa 10,000. Bodaboda wataepuka makosa ya barabarani ili wasipigwe faini? Ajali za bodaboda kuwakimbia Polisi zitapungua? Hawatoogopa kufanya makosa kwa kuwa adhabu imepunguzwa?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom