Katika sensa ya marudio iliyofanyika kwa gharama kubwa na kutoa taarifa kuwa Tembo wamepungua kutoka idadi ya tembo 109,000 mwaka 2009 mpaka kufikia tembo 51,000 mwaka 2015. Hii ni AIBU kubwa kwa SERIKALI YA AWAMU YA NNE ambayo kila kona inalaumiwa. Hivi kulikuwa na nini katika awamu hii. Tuakuomba Mhe.Magufuli kwa imani yetu kwako wadhibiti hawa majangili ili wasipate nafasi tena wa kuwaangamiza tembo ambao ni urithi wetu tuliopewa na Mwenyezi Mungu. Ninaamini kwa usimamizi wa Mhe wa HAPA KAZI TU baada ya miaka mitatu idadi ya tembo waafikia 150,000. AIBU SANA KWA SERIKALI YA AWAMU YA NNE.