Leo asubuhi nimesoma kwa masikitiko makubwa kupungua kwa kasi kwa sarafu ya Tanzania dhidi ya dollar ya Kimarekani. Leo thamani ya dollar kwa fedha ya Kitanzania ni 1$ = 2194.50 kwa taarifa ya Benki ya Tanzania. Mwaka mmoja uliopita 1$ = 1640. Mimi ninawauliza Benki Kuu ya Tanzania ni sababu gani sarafu yetu imeporomoka kwa kasi hivyo?.