Zogwale
JF-Expert Member
- Jul 10, 2008
- 15,287
- 10,842
Alishasema ni hadithi ya kutunga. Hivyo, si kweli ndivyo alivyo.Nionavyo mimi:-
1. Ni kweli tunaochangia mada hapa kwenye JF hatujuani kwa sura, lakini ni rahisi kurealize tabia ya mtu kutokana na uandishi au uchangiaji wake. Hapa point yangu ni kwamba, kutokana na uchangiaji wako hapo juu, naweza ku-realize kwamba wewe u-mshari au mwenye kupenda ugomvi.
2. Kutokana na issue yako na mmeo, naona tatizo si umri kwani range uliyoitoa ya miaka 35 kwa 47 inaonyesha kwamba ni watu wenye mawazo sawa. Hivyo suala la umri sio tatizo katika ndoa yenu.
3. Kama utakuwa umeolewa ukiwa na umri mkubwa sana (takribani miaka 32), kwa umri huu wanawake walio wengi (si wote) wanakuwa tayari hawana mawazo ya kuolewa ila kuishi maisha ya kujipangia uhuru wao wenyewe. Wengi wao wanakuwa wamekatishwa tamaa au wamejeruhiwa roho zao na wanaume kimapanzi kipindi cha umri ambapo wanakuwa wanatamani sana kuolewa (Miaka 20 - 30). Kwa umri wa miaka 32 tayari wanakuwa wamezoea kuishi kwa uhuru wao. On the other words, wanakuwa tayari wamekuwa sugu au wamekubuhu....hawajali tena ndoa..ila kujifuhaisha nafsi zao kwa mapenzi tu...
4. Kwa kifupi, kuna wanawake waolewa (good wives) na wanawake wasio waolewa (bad wives). Good wives wanapenda sana ndoa zao, na wanafanya kila liwalo kuzilinda bila kujali magumu wanayokumbana nayo. Bad wives hawa ni wale wapenda good time, wanataka wawe na wanaume kwa ajili ya kujifurahisha na kwa kipindi fulani. Baada ya muda huboreka na hutaka kubadirisha. Wengi wao unakuta wana vijisenti au kazi nzuri na hivyo wanakuwa na kiburi, si wasikivu.
5. Conclusion: Wewe dada aidha ni mshari au uko kwenye kundi la bad wives. Siwezi kukulaumu na pia huwezi ujilaumu. That is the reality.
6. Ushauri: Mwombe Mwenyezi mungu akuzishie upendo kwa mmeo na pia jitahidi kuwaona washauri wa mambo ya ndoa, pengine waweza kupata msaada zaidi wa kuimarisha ndoa yako.
7. Nakutakia maisha mazuri ya ndoa.
Ila ifahamike kuwa kuna ndoa ngumu sana, yaani ni mateso either kwa mke au mume. Katika hizi ndoa lazima kuna ambaye yeye ndiye anayesababisha mgongano. Cha msingi tu huu ni mfano na kwa wale ambao wako humu au ndugu au marafiki wana suffer katika ndoa, suluhisho si kuachana hasa pale ambapo mna watoto. Mara zote tujifunze kusuluhisha matatizo ya ndoa kila siku ikiwezekana kama pametokea kutoelewana hata katika jambo ndogo. Fahamu kuwa madogo huzaa makubwa. Kama hujajijengea utamaduni wa kumaliza tofauti zenu kila wakati mara leo mnanuniana, mara kesho mnacheka then mtakuwa na maisha magumu baadaye hasa pale miaka ya ndoa inaposogea.
Ndoa nyingi ni ngumu sana from 0-5 years maana hapa ndo kila mtu anaanza kuonyesha true colours zake. Sasa 5-10 years kama kulikuwa na tatizo na hakuna uvumilkivu na kuelewana hapa talaka ni nyingi sana. Kuanzia 10 years wanandoa wanaanza kuwa wazoefu kwa kiasi fulani na kutojali sana na mwishowe wanachukulia mikwaruzo kuwa ni part of their marriage life hakuna kujali na mtu anaona after all wameshazalisha au kujenga pamoja na haina maana kuachana so utakuta wengi wanalala vyumba tofauti au hata kama wanalala chumba kimoja lakini hakuna sexual desire na kila mtu unaweza kuta ana mtu wake nje, hasa wanaume tulio wengi. Akina mama wanaweza kuachana na sexual desire na akawa busy na watoto wake, hasa mabinti maana atakuwa nao karibu kwa umri huu wa wasichana na ubisy huo unamtosha. Ni ndoa chache sana ambazo zinakuwa smooth thoroughtout.
Cha msingi ni jukumu la kila mwanandoa kuilinda na kuheshimu ndoa yake. Ndoa inapovunjika ni aibu. Si jambo jema. Wanandoa tupendane na kuwa waaminifu, tusiwe wachoyo katika kuonyesha upendo. Na ndoa itadumu.