Kupungua au kukosa hamu ya kufanya mapenzi (low sexual libido or loss of libido)

Ilikuwaje hadi ukaolewa nae pengine kutokana na mfumo katika jamii zetu kwamba wanawake hawana choice, unasubiri atakaye kutafuta.

Mwanaume wa kwanza anakutest akiona hufai anakuacha, wakikutest wawili watatu utaitwa malaya! Mwanaume hata akiwa nao kumi na sita, yeye ni kidume cha mbegu!

Ushauri: wala usimuudhi mwenzio, ondoka kama ifuatavyo ukachezewe na wanaume wengine. Hakuna mwanaume mzuri isipokuwa yule responsible na anayekujali kwa shida na raha; na hakuna mapenzi ila yaende compatibility, ila huyu mliye compatible kumpata ndio kasheshe.

Ushauri mzuri, asante sana mama.
 
Sasa mtatukisha ambao hatujaoa au mnataka tubaki ka mwanaFA 'bado nipo nipo'' maada yako inatatanisha kidogo kitendo cha kumchukia tu mumeo bila sababu labda wataalamu kama wanasa technical advive ila mimi kinanipa shida kidogo. kama mplipendana vizuri mwanzo na hakukuwa na material thing 'yaani hukumpendea kitu fulani ambacho sasa hakipo' si rahisi kumchukia bila sababu may be kama ameanza tabia furani ambayo huipendi ila kama jamaa hanatatizo then there is something wrong with you.

Nakushauri mrudie Mungu wako na muombe Mungu wako alejeshe furaha ndani ya ndoa yako.
 
Kwa kweli imekuwa na furaha zake pia ni vikwanzo vingi. Imefikia sasa mimi najishangaa sana kuwa nimeishiwa hamu kabisa na mme wangu na ninamuona mbaya sana. Nakaa na kujiuliza ilikuwaje mpaka nikaolewa nae.
Wewe ni dini gani?
 
Mrs Mtaba,

Inaelekea ulikuwa na mchecheto tu wa kuolewa na hukuwa na mapenzi ya kweli kwa huyo mwanaume. Haiwezekani uwe umemchoka mumeo baada ya miaka miwili tu ya ndoa. Je ulilazimishwa kuolewa naye labda na wazazi, ndugu au marafiki? Kabla ya kuoana mlikuwa marafiki kwa muda gani?

Humfanyii haki huyo baba kwa kumfanyia visa ili akuache, na wakati huo huo yeye si ajabu anakupenda kwa moyo wake wote. Mwambie ukweli badala ya kumpotezea muda wake ili atafute mke mwingine ambaye atakuwa na mapenzi ya kweli kwake.
 
Last edited by a moderator:
Mrs Mtaba,

Hamu ni tamu kuliko tamu yenyewe. Mbingu ulizotamani naona zimegeuka jehanamu ndani ya miaka 2. Hili si tatizo lako peke yako, linawapata wengi. Shida ni njia unazotaka kutumia kulimaliza. Yaani inaonekana humfikirii hata kidogo mume wako. Labda utwambie umepata mtaalamu zaidi yake.

Hata hivyo uzuri wa kitu uonekana unapokikosa. Nakushauri ujipe likizo kidogo mbali na mume wako (kama mieizi 1-2) ili ufanye tafakuri kama kweli mume wako ana kitu chocho kinachokufaa. Kwa lolote utakalofanya (kubaki au kuondoka), naamini utajutia uamuzi wako tu! La muhimu ni kuchukua tahadhari ili kiwango cha majuto kisiwe kikubwa sana ambacho kinaweza kukusababishia madhara makuwa kiafya au kisaikolojia.

Nakutakia kila la heri dadangu; ila ujue dunia ni duara, ukizunguka utarudi ulikoanzia (kama utafanikiwa kuimaliza safari)!!
 
Last edited by a moderator:
Ninachoona hapa ni kukosa hamu basi nitumie message(PM) ili tuende faragha nikupatie hamu kwasababu kila mtu mwenye akili timamu anahitaji kufurahi.Kama kweli unachosema ndiyo unachokimaanisha nitakuwa tayari kukusaidia.
Nafikiri utakuwa umenisoma.
 
Mrs Mtaba,

Pole sana kwa hali uliyonayo, ila nashindwa kuelewa Unaomba JF wakupe mbinu za Kuachana na Mume wako au Unaomba JF wakupe ushauri na Experince ili uweze kurudisha hali ya Utulivu katika ndoa yako? Unajua Ndoa ni Ndoani, kama ni Mkristo hicho ni Kifungu cha Maisha kwa hiyo ushauri wangu badala ya Kuzunguka na Kutafuta Mbinu za Kumuacha Mumeo ni bora kujiuliza nini tatizo na utafute suluhisho la Ndoa yenu! Sidhani kama kuna Member atakayekuambia Fanya hivi au vile ili Mumeo akuache, Don't be selfish ni lazima umfikrie na mwenzako the way atakavyoumia.

Kama kuna kidume kinachokuzingua elewa kinafanya hivyo jaust because uko na mume wako na hakiataki responsibilities, siku mume wako akikumwaga na Hicho kidume chako nacho kitakumwaga na hapo ndipo kutakapokuwa na kilio cha Kusga na Meno!
Elewa kwamba suala la Ndoa ni responsibility yenu wote na si mume tu

Asante
 
Last edited by a moderator:
Mrs Mtaba,

inatokeaga sana hiyo, mie wakati nina mikwaruzano na mr nilikuwa sina hamu nae hata kidogoo, tulipoweka mambo sawa still nikawa bado sana, nilikuwa nafanya kama wajibu tu sio kimapenzi, si feel lolote najisemea amalize niendelee na mambo yangu mengine.....!hapo sasa yeye ndio ana mapenzi na wewe haswaa, huku wewe ndio walaaa akikugusa unatamani umzabe vibao...

haaa kazi kweli!, mie nakushauri usivunje ndoa yako, jitahidi sana kurudi kama awali japo ni ngumu but ma dia usivunje ndoa yako.
 
Last edited by a moderator:
Hiki kizazi cha karne hii sijui kina matatizo gani!
Ni kitu gani kilikusukuma hadi ukaingia kwenye hiyo ndoa? Kwa mana inawezekena kuna kitu ulikuwa unapata ama ulitaraji kupata kwa bahati mbaya sana hakipo,then ukajikuta unajenga chuki.

Vinginevyo ningekuwa wewe ningesafiri hata kwa mwezi then nikirudi niangalie kama kutakuwa na mabadiliko yeyote kuliko kumfanyanyia maudhi mwenzako.

Haumtendei haki kabisa.

kuna rafiki yangu 1 aliolewa coz jamaa yake alikuwa na gari /nyumba/na pesa nyingi, walifahamiana kwa miezi 3 tu wakafunga ndoa, kumbe mkaka ana mke na watoto kwao musoma, mwanaume ni kumpiga mpaka mdada analazwa, akajiondokea ndoa ikiwa na miezi 5 tu.
 
naona hajatumia misingi ya ndoa iapsavyo kama inavyoelekeza na dini zetu pia na mila zetu.

tafuta sababu kwanini unajisikia hivyo wakati ulikuwa na hamu na mume wako mwanzoni mwa ndoa yetu,inawezekana unamatatizo kibioligia.

jaribu kuwaona watalaamu wa psycholojia na maradha ya kina mama.

Pole sana
 
...it's obvious hata wachangiaji wa JF wamegawanyika makundi mawili. Kundi la mwanzo Wanawake, wana empathy na mwenzao, na wengi wao wanakubaliana naye lipo hilo tatizo, na linapaswa kushughulikiwa hatua kwa hatua...

Kundi la pili ambalo linajumuisha wachangiaji wanaume, wengi wao wamekuwa (pessimistic) negative na mawazo ya huyu bibie. Mmegundua tatizo ni nini?

UKWELI!... kwenye maisha ya ndoa/mahusiano hakuna jambo la busara kama kuukubali ukweli. Ukweli hauna Imani ya dini, umri, wala kabila... Ukweli unabakia Ukweli...

Wanaume tuukubali ukweli, hasa inapofikia suala la kujiuliza kwenye mahusiano ya ndoa, sie wanaume tunachangia kwa kiasi gani kupunguza hamu ya Mapenzi yalokuwepo awali na better halves wetu, sio kutoa kashfa, ukali na vitisho as if mwanamke hana haki ya Kulalamikia haki yake.
 
Na vipi wanawake nao, maana kuna wengi tu ambao hutoka nje ya ndoa zao kwa visingizio kibao visivyo vya msingi. Wanaume na wenyewe wana haki ya kulalamika?

Haya ya kusema sijui wanaume tuko hivi au vile na tukubali ukweli si kuwatendea haki wale wanaume wanaoheshimu marriage vows zao. Itakuwa busara kuchukulia kila mtu au kila tatizo la ndoa on a case by case basis na kuacha broad generalization.
 
Hayo ndo mambo ya kulazimisha mapenzi kwa sababu ya fedha au sifa au umaarufu, na mwisho wake nature inakuja kuchukua mkondo,
lakini tatizo kubwa hapo ni kupotezeana muda na usumbufu wa kisaikolijia utakao mpa mwwenzio kutokana na alivyokupenda wewe, pia kutakuwa na mtazamo ambao sidhani kama utakuwa wa heshima kama mlizokuwa nazo wakati mpo wawili, watu watajaji wanavyofiria na heshima kwa kiasi fulani itapungua, wengine watasema mama alikuwa kicheche mara mzee jogoo awiki ili mradi mtakuwa sio sio tu
 
...true man!...na point ya ukicheche..teh teh teh
 
Huwa nafurahia sana mabo ya kijinga ya wanwake. Wewe umchoke mwenzako halafu ili usipate aibu unachokoza ili uachwe? Hongereni
 
Huwa nafurahia sana mabo ya kijinga ya wanwake. Wewe umchoke mwenzako halafu ili usipate aibu unachokoza ili uachwe? Hongereni
Hivi ngoja nikuulize, unaweza kumwambia mkeo aende nje akatafute wanaume kwa sababu amedai unyumba ambao unampaga kama dawa ya surua na pale wewe utakapo!

Ok mke ulipomwambia hivyo akajinyamazia kimya bila ungomvi wowote, akawa anasubiria mpaka hamu yako itakapokupanda uende kuomba mambo. Then ukifika unaanza kumshikashika kama vile hutaki, na yeye anakuambia hana hamu. Kwa uselfish wako unajiinukia nakuondoka zako. Hivi kwa maneno hayo au matendo yaho utaendelea kumpenda huyu mtu wala kumtamani.

Tuwe wakweli jamaa tuache unafiki, maana mpaka kufikia hapa ujue maji yamefika shingoni.
 
Mrs Mtaba,

Please think positive, ndoa ni lulu. Ni bora mara elfu ushukuru upo ndni ya ndoa, kuna wengine wanatamani waolewe but Mungu mwingi wa Rehma hajawawezesha. Nakupa ushauri wa bure tuuu; tafuta nafasi tulivu kabisa ikiwezekana fanya mtoko rasmi wa kuwa mbali na hapo kwenu then fikiria yafuatayo: -

1. Ni kitu gani hasa huyo mheshimiwa wako alikuvutia nacho hadi mkakokotana ktk ndoa?
2. Ni kweli mnapendana kwa dhati au mnadanganyana?
3. Fikiria ni mambo gani mlikuwa mnayafanya kwa pamoja wkt uleee b4 hamjakula kiapo cha kuwa pmj daima milele, je kwasasa yapo au yameisha?
4. Pia nakushauri muwe wapya kila mara ktk ndoa yenu, jaribu japo kubadilisha mpangilio wa fenicha ktk nyumba yenu, nunulianeni kadi, mtoke pmj japo knd kanisani n.k

Yapo mambo mengi ya kufikiria b4 kuuamua kuachwa, ukishaachwa nini kitafuata? Nahisi unajidanganya utakuwa mtu huru but 2 me that is negative attitude!!!!

Mkumbuke Mungu wako na mtangulize kwa kila jambo then think b4 u act!!!!

Tchao
 
Last edited by a moderator:
Mrs Mtaba,

nakushauri usichukue hatua ya kumuacha mumeo kwanza. Acha visa, tena unapomchokoza ndio mambo yanakuwa mabaya sana. Kuna ushauri umepewa nauunga mkono wa kuwa na muda peke yako na kutafakari yaliyojiri, hasa sababu ambazo zimepekea kufikia hapo. Ila nakuuliza:-

Je una uhakika kabisa kabisa kuwa hauna mahusiano au haujavutiwa na mwanaume mwingine? Sema kweli kabisa.
Mtoto wenu ana umri gani, na mabadiliko kwa mumeo umeyaona tangu lini?

Ni siri iliyo wazi kuwa kama unaishi na mwanaume anakugusa gusa tu, hakufukuzii hata kama ni kwenye ndoa, hainogi kabisa, wanaume jifunzeni kwa KUKU na JOGOO.

Don't go against nature. Marriage is not automatic.
 
Last edited by a moderator:
Hivi ngoja nikuulize, unaweza kumwambia mkeo aende nje akatafute wanaume kwa sababu amedai unyumba ambao unampaga kama dawa ya surua na pale wewe utakapo!

Ok mke ulipomwambia hivyo akajinyamazia kimya bila ungomvi wowote, akawa anasubiria mpaka hamu yako itakapokupanda uende kuomba mambo. Then ukifika unaanza kumshikashika kama vile hutaki, na yeye anakuambia hana hamu. Kwa uselfish wako unajiinukia nakuondoka zako. Hivi kwa maneno hayo au matendo yaho utaendelea kumpenda huyu mtu wala kumtamani.

Tuwe wakweli jamaa tuache unafiki, maana mpaka kufikia hapa ujue maji yamefika shingoni.

Hilo ni kosa lako Anti, hukuwa wazi tangu ulipoanza luelezea mkasa wako. yaani hukusema yale yanayokufanya usiitamani tena ndoa yako. Je ushawahi kumuweka chini mkajadili tatizo nini why hapendi ku-sex nawe? je wewe ni tatizo au yeye? mumeo ni mlevi?

Plaese fikiria sana hili: UPENDO WA KWELI UPO KATI YENU?
 
Mrs Mtaba,

Kwanza inaonesha mmeoana umri ukiwa umeshasogea kidogo na inavyoonesha we ushapata mtu mwingine
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom