OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 48,776
- 102,133
@dr_chriscyrilo daktari wa binadamu, baba wa mtoto mmoja, ndugu na rafiki wa wengi. Hospitali anayofanyia kazi inafahamika, nyumba anayoishi inafahamika. Kwanini hamkumpelekea arresting warranty kazini au nyumbani kwamba anahitajika polisi ili aende mwenyewe? Kwanini mnamvizia na kumkamata kama jambazi? Na media zetu zinaona ni sawa tu? Daktari anakamatwa kama jambazi kwenu sio story?
Na hii si mara ya kwanza kukalia kimya matukio ya watu kukamatwa, kutekwa au kupotezwa. Wakati wa #BenSaanane tulipiga kelele wenyewe huku mitandaoni. Hakuna media iliyojishughulisha kuripoti. Baadae sana baada ya matumaini ya kumpata kupotea ndio media zikaanza kuripoti, but was too late.
Waandishi walipoanza kutekwa na kupotezwa ndio main stream zikaanza kuzipa uzito habari za watu kutekwa.
Kwenye "awamu hii" waandishi mnaweza kujiona salama kwa sababu hamjaanza "kushughulikiwa". Kwahiyo mnaona ni mambo yanayowahusu wakosoaji wa mitandaoni tu. Lakini amin amin nawaanbia, ipo siku itatokea kwenu na hakutakua na mtu wa kuwatetea. No one is safe in the situation of injustice.
Mchungaji Martin Niemöller aliwahi kusema "Waliwaua wajamaa, sikuwatetea kwa sababu sikua mjamaa. Kisha wakaenda kwa wafanyakazi, sikuzungumza kwa sababu sikua mfanyakazi. Wakaenda kwa wayahudi, sikuwatetea kwa sababu sikuwa Myahudi. Mwishowe wakaja kwangu, na hapakuwepo na aliyesalia kunitetea"
Credit: Malisa
My Take
Akipotea mwandishi wenu au kudakwa na polisi makelele kama yote. Ila kwa wengine mnakuwa kimyaaaa. Vita ya dhidi ya udhalimu haipiganwi hivyo.