Kupotea kwa boti ziwa Tanganyika: Nashauri Jeshi liingilie kati

Jan 15, 2017
50
64
Wasalaam,imeripotiwa na vyombo vyote vya habari hasa ITV kuhusu kupotea kwa boti iliokuwa ikielekea kongo. Humo kuna watanzania wenzetu;nawashauri serikali kutuma kikosi cha wanamaji(JWTZ) na KMKGM kutafuta mapaki ya boti au miili ya marehemu. Maana tusije Sema boti imezama kumbe imetekwa nyara na watu kuuwawa maana ukanda huu sio salama wote tunafahamu;namuomba waziri WA ulinzi alichukue hili na kulifanyia kazi.
 
Imezama upande gani maana ziwa tanganyika nikubwa kwa Tanzania ni Kigoma hadi Chipwa Mkoani Rukwa, wapi sasa, na Congo hiyo Moba, Nkorosha, Kiku, Uvira ama Kalemie, fafanua uzuri
 
Ndio usafiri tulio nao labda Azam atunusuru
Azam anaweza kuja kuwekeza kule anapita bandari kubwa kubwa zote ingawa najua kule kuna fitna kubwa sana toka kwa wenyeji waliowekeza kwenye maboti hayo miaka nenda rudi ushirikina umetamalaki pia.....hali usalama kwa upande wa pili congo na burundi sidhani kama atakuwa radhi kupeleka meli zake zikatekwe kule na kudaiwa mamilioni kuzikomboa......hata wale matajiri wa Mwanza waliowekeza kwenye kivuko mbona wanaogopa kuwekeza meli za mizigo kule? Kuna changamoto kubwa sana kule!!!!
 
Mkuu unaikumbuka mv bulombola ilivyo kuwa inapigwa juju na wenye maboti kina mzee aman ya mungu kina kiswaga mangi
 
Back
Top Bottom