Kupotea kwa Ben Saanane: Hoja za wananchi, kinachoendelea na maoni ya Waziri Mwigulu

Bwana mkubwa sana Mwigulu Nchemba

Vijana kama ninyi mlio na madaraka makubwa sana mlitakiwa kubadilisha hali ya kisiasa iliyopo kwa sasa kwa kumshawishi na kumshauri yule Bwana Mkubwa Zaidi abadilike. Hakuna kitu kama
negócios, como sempre na hata fait accompli. Ili jamii isonge mbele watawala wanatakiwa kuangaliwa na kusimamiwa na wanao waowaongoza na sio kinyume chake. Siku za mbeleni jamii itakuja kuwahukumu hata kama in post humus . Kwa sasa kuna hawa millenials wanajengewa mazingira mabaya sana kiakili na kifikra. Kusimama hadharani na kutetea kuwa mambo yako sawa wakati hayako sawa na hata katika nafsi zenu mkijua hilo ni jambo la hatari sana.

Deus salve o meu povo!!!
 
technically toa hiyo pctr ya Nyerere, huitendei haki
Kwanza majibu yake tu ni ushaidi tosha kwamba hana uhakika na anachokielezea......

Soma between the line kwenye maelezo yake utapata majibu kuwa anachokiongea sio anachomaanisha.....

Atoi time flame ni lini hizo mifupa zitamalizika kufanyiwa test....

Waziri Mwenye dhamana ya kumpata mtu aliyepotea yeye analalamikia kupotea kwake?.....

Alafu anakwambia anaweza kukukamata ujibu uku ameshindwa kuwakamata waliofanya Ben Saanane apotee na kujua haliko ?

Kazi yao kuangaika na wanao wakosoa kuliko Ku deals na matatizo ya wananchi?........

Akili ndogo haiwezi kutawala akili kubwa .
 
WanaJF,

Nimeamua (kama member wa JF) kuandika kwa masikitiko makubwa sana kufuatia uzi wa technically:

Mwigulu Nchemba ndiye suspect namba moja kupotea kwa Ben Saanane?

Vijana wenzangu, tuwe tunatafakari kwanza kabla ya kuaondika mambo makubwa yasiyo na utani bila kujiridhisha na tunachokiandika. Sio kitu kizuri kuandika jambo kubwa hivi kwa taarifa za kuungaunga na ufahamu wa kuungaunga.

1) Moja anasema watu wamezikwa bila kutambuliwa: Ni kweli watu hao miili ilishaharibika na hatua iliyokuwa inasitahili ilikuwa kuzikwa. Hata hivyo tumechukua sampuli kwa kila mwili nawe ukitaka kuitambua unaruhusiwa. Mpaka sasa haijulikani sana uhakika kuwa hao ni nani, lakini sisi tulisema kuna uhusiano mkubwa wa watu hao na wahamiaji haramu ambao waliokotwa 81 wakiwa mahututi eneo hilohilo na wiki hiyo hiyo.

Hatujasema kuwa ni kwa asilimia 100 ni wahamiaji haramu, tunasema huenda wakawa ni wao maana kama hao 81walikuwa hoi wiki hiyo hiyo huenda kati yao kukawa na baadhi yao ambao walishapoteza maisha na tukasema tuendelee na kutafuta undani zaidi, lakini wewe unasema tumezika bila kutambuliwa, hivi ni nani angewatambua? This is not fair.

Wapo wakadiriki hata kusema watu hao waliuwawa na Polisi, la hasha hata wakiwa wahamiaji haramu hawaruhusi kuuawa ndio maana Polisi ilipowaokota wale mahututi wakiwa hwawezi kuongea wala kusema iliwapikia uji na wengine kuwapeleka hosipitali.

Tunaongelea miili iliyookotwa, kumekuwa na kawaida ya wasafirisha watu kutupa miili hovyo, sishangai huenda hata wakawa walikuwa zaidi ya 81 wameokotwa saba, huenda wengine wakawa wamepelekwa baharini, ndio maana tunaendelea kutafuta undani.

2) Pili unasema kifo cha Mbagala kahusika Mwigulu, Eti alifika wa kwanza.

Si kweli, sikufika wa Kwanza. Angalia, kwanza tukio lilifanyika saa moja kwenda saa mbili hivi, akaenda OCD saa moja hivi, saa tatu akaenda RPC, saa nne akaenda Siro na IGP. Mimi nilienda Saa sita usiku na nimemkuta RPC na Kamanda Siro na video zipo. Niliwakuta na ndio walikuwa wananielekeza tukio lilipo. Unasema niliwatangulia polisi? Jitafakari. Yaani yote hayo ni kutaka kuhalalisha fikra potofu na kuchafua taswira ya mtu, kwanini unaandika kwa uhakika wakati ni vitu vya kusikia?

3) Tatu unasema swala la Lwakatare. Kwa sasa Lwakatare ni mbunge na ni rafiki yangu na anajua ukweli wa yote yale yaliotokea na tunaongea mara kwa mara. Nitakupa namba yangu, hebu tafuta siku tukakae na Lwakatare mimi nawe akisema nilimsingizia nitaacha ubunge na uwaziri.

Jana tu, tar 20/12/2016 ilikuwa kesi hiyo hiyo wewe unasema kesi ilienda mpaka ikaisha! Uwe unapata ukweli kabla ya kuandika. Jambo hili halijaisha jana ilikuwa kesi, lakini Lwakatare anajua hili jambo, tunaongea mara kwa mara nadhani ungeacha tu jambo hili liishe liliko kwenye mkono wa sheria, usilichokonoe hata Lwaka hangependa ulichokonoe kama unavyofanya kwani yeye anajua ukweli, namba yangu ni 0714008888

4) Unasema nilisema nitatoa ushahidi wa mauaji ya SOWETO. Ndugu, kapitie upya kumbukumbu zako. Nenda kaongee na Lema hata sasa kulekule alipo, muulizie maana naye mwanzo alikuwa na mtazamo kama wa kwako.

Ushauri wangu: Kuandika hapa jamvini suala serious kama hili ni vyema ukafanya fact finding kidogo

Sasa kuhusu suala la Ben Saanane:

Kwanza tumwombee kwa Mungu awe salama mpaka sasa. Tafadhali usiandike kwa hisia zako.

Ben is my personal friend (Sio katika Siasa) tunakutana na kushirikiana mambo kila mara mpaka ya familia, namfahamu na anaifahamu familia yangu mpaka watoto wangu wanamfahamu. Nilimsaidia kura za maoni ndani ya chama chake, nimewasiliana naye mfululizo mpaka wiki hiyo hiyo. Unamwongelea rafiki yangu na ndugu yangu wa ndani, na sasa nafuatilia kama serikali na kama rafiki.

Tafadhali, tuna mambo ya kisera tunaweza kupigana madongo, lakini hapa tunaongelea maisha ya mtu, an innocent young brother. Usikusanye vitu vya kuungaunga na kuleta katika jambo kubwa ambalo bado lina giza na wengine ni ndugu yao wa damu na wengine ni close friend.

Naamini mimi Ben ni rafiki wa karibu kwangu kuliko kwako mtoa mada maana ungekuwa mtu wake wa karibu ungejua haya ninayokwambia. Fuatilia mawasiliano yangu na Ben tangu mwaka juzi ndio uone who are we. I still believe kuwa Mungu anamlinda Ben na nchi yetu haijafika huko

Mwigulu
Hii ndio aina ya ujengaji hoja unaotakiwa. Good Mwigulu.
 
Ben is my personal friend (Sio katika Siasa) tunakutana na kushirikiana mambo kila mara mpaka ya familia, namfahamu na anaifahamu familia yangu mpaka watoto wangu wanamfahamu. Nilimsaidia kura za maoni ndani ya chama chake, nimewasiliana naye mfululizo mpaka wiki hiyo hiyo. Unamwongelea rafiki yangu na ndugu yangu wa ndani, na sasa nafuatilia kama serikali na kama rafiki.
Mh, hapo mimi nimebaki gizani!?
 
Kwanza nikupongeze bwana Mwigulu Nchemba kwa kuweza kujitokeza leo hii kumjibu mwanajf mwenzetu. Kwa kweli una roho ngumu maana huku jukwaani zile lugha za kunyenyekewa kama kiongozi hazipo bali unapewa makavu live. Nadhani ndugu utakuwa umejifunza maana ya kutoa taarifa kwa umma mara moja pindi kunapokuwa na suala linalowagusa. Huenda hili suala la miili 7 mmelikalia kimya kwani kwa namna moja limekuja na la Ben Saanane ambaye ni mpinzani, na ni ukweli ulio dhahiri serekali hii inafanya kazi kiitikadi, ukubali ukatae hilo liko wazi. Nina mashaka sana kama suala hilo lingemkuta mwanaccm mngekaa kimya hivi nyie kama serekali bila kuonyesha jitihada. Hakuna namna yoyote sisi wananchi tungekaa kimya wakati ndio tuliowaweka madarakani tuone taarifa tunazopata toka serekalini ni za Faru kuliko binadamu bila kujali ni wa aina gani. Kumbuka hakuna faru anayetoa madaraka, bali ni nyara tu za serekali hata kama anaingiza kodi kubwa ila binadamu ni kipaombele chenu, labda kama haumfahamu au kuwa mpinzani ni kama mtoto wa kambo.

Wakati mwingine ni vyema mkajua wajibu wenu sio kukaa kimya pindi mnapokuwa kwenye ofisi za umma, hizi kelele unapigiwa kama waziri mwenye dhamana ya jambo hili na sio Mwigulu kama Mwigulu. Kwa mtazamo wangu hafifu mnadhani kuwa kwenye ofisi ya umma ni sehemu ya kuula, bila kujua kwamba ukiwa kwenye ofisi ya umma ni kama umebeba msalaba, na pindi linapotokea jambo tena linalohitaji ufafanuzi lazima uwajibike. Napenda nikupongeze tena wangalau kwa kuonyesha kuguswa na hili jambo, japo mmechelewa kutoa taarifa kwa umma kwa wakati mpaka watu kukosa uvumilivu na kujikuta post kama hizi zinakufukua huko ofisini.
 
Back
Top Bottom