Kupotea kwa Ben Saanane: Hoja za wananchi, kinachoendelea na maoni ya Waziri Mwigulu

Mwigulu Nchemba

Verified Member
Feb 25, 2012
414
1,000
WanaJF,

Nimeamua (kama member wa JF) kuandika kwa masikitiko makubwa sana kufuatia uzi wa technically:

Mwigulu Nchemba ndiye suspect namba moja kupotea kwa Ben Saanane?

Vijana wenzangu, tuwe tunatafakari kwanza kabla ya kuaondika mambo makubwa yasiyo na utani bila kujiridhisha na tunachokiandika. Sio kitu kizuri kuandika jambo kubwa hivi kwa taarifa za kuungaunga na ufahamu wa kuungaunga.

1) Moja anasema watu wamezikwa bila kutambuliwa: Ni kweli watu hao miili ilishaharibika na hatua iliyokuwa inasitahili ilikuwa kuzikwa. Hata hivyo tumechukua sampuli kwa kila mwili nawe ukitaka kuitambua unaruhusiwa. Mpaka sasa haijulikani sana uhakika kuwa hao ni nani, lakini sisi tulisema kuna uhusiano mkubwa wa watu hao na wahamiaji haramu ambao waliokotwa 81 wakiwa mahututi eneo hilohilo na wiki hiyo hiyo.

Hatujasema kuwa ni kwa asilimia 100 ni wahamiaji haramu, tunasema huenda wakawa ni wao maana kama hao 81walikuwa hoi wiki hiyo hiyo huenda kati yao kukawa na baadhi yao ambao walishapoteza maisha na tukasema tuendelee na kutafuta undani zaidi, lakini wewe unasema tumezika bila kutambuliwa, hivi ni nani angewatambua? This is not fair.

Wapo wakadiriki hata kusema watu hao waliuwawa na Polisi, la hasha hata wakiwa wahamiaji haramu hawaruhusi kuuawa ndio maana Polisi ilipowaokota wale mahututi wakiwa hwawezi kuongea wala kusema iliwapikia uji na wengine kuwapeleka hosipitali.

Tunaongelea miili iliyookotwa, kumekuwa na kawaida ya wasafirisha watu kutupa miili hovyo, sishangai huenda hata wakawa walikuwa zaidi ya 81 wameokotwa saba, huenda wengine wakawa wamepelekwa baharini, ndio maana tunaendelea kutafuta undani.

2) Pili unasema kifo cha Mbagala kahusika Mwigulu, Eti alifika wa kwanza.

Si kweli, sikufika wa Kwanza. Angalia, kwanza tukio lilifanyika saa moja kwenda saa mbili hivi, akaenda OCD saa moja hivi, saa tatu akaenda RPC, saa nne akaenda Siro na IGP. Mimi nilienda Saa sita usiku na nimemkuta RPC na Kamanda Siro na video zipo. Niliwakuta na ndio walikuwa wananielekeza tukio lilipo. Unasema niliwatangulia polisi? Jitafakari. Yaani yote hayo ni kutaka kuhalalisha fikra potofu na kuchafua taswira ya mtu, kwanini unaandika kwa uhakika wakati ni vitu vya kusikia?

3) Tatu unasema swala la Lwakatare. Kwa sasa Lwakatare ni mbunge na ni rafiki yangu na anajua ukweli wa yote yale yaliotokea na tunaongea mara kwa mara. Nitakupa namba yangu, hebu tafuta siku tukakae na Lwakatare mimi nawe akisema nilimsingizia nitaacha ubunge na uwaziri.

Jana tu, tar 20/12/2016 ilikuwa kesi hiyo hiyo wewe unasema kesi ilienda mpaka ikaisha! Uwe unapata ukweli kabla ya kuandika. Jambo hili halijaisha jana ilikuwa kesi, lakini Lwakatare anajua hili jambo, tunaongea mara kwa mara nadhani ungeacha tu jambo hili liishe liliko kwenye mkono wa sheria, usilichokonoe hata Lwaka hangependa ulichokonoe kama unavyofanya kwani yeye anajua ukweli, namba yangu ni 0714008888

4) Unasema nilisema nitatoa ushahidi wa mauaji ya SOWETO. Ndugu, kapitie upya kumbukumbu zako. Nenda kaongee na Lema hata sasa kulekule alipo, muulizie maana naye mwanzo alikuwa na mtazamo kama wa kwako.

Ushauri wangu: Kuandika hapa jamvini suala serious kama hili ni vyema ukafanya fact finding kidogo

Sasa kuhusu suala la Ben Saanane:

Kwanza tumwombee kwa Mungu awe salama mpaka sasa. Tafadhali usiandike kwa hisia zako.

Ben is my personal friend (Sio katika Siasa) tunakutana na kushirikiana mambo kila mara mpaka ya familia, namfahamu na anaifahamu familia yangu mpaka watoto wangu wanamfahamu. Nilimsaidia kura za maoni ndani ya chama chake, nimewasiliana naye mfululizo mpaka wiki hiyo hiyo. Unamwongelea rafiki yangu na ndugu yangu wa ndani, na sasa nafuatilia kama serikali na kama rafiki.

Tafadhali, tuna mambo ya kisera tunaweza kupigana madongo, lakini hapa tunaongelea maisha ya mtu, an innocent young brother. Usikusanye vitu vya kuungaunga na kuleta katika jambo kubwa ambalo bado lina giza na wengine ni ndugu yao wa damu na wengine ni close friend.

Naamini mimi Ben ni rafiki wa karibu kwangu kuliko kwako mtoa mada maana ungekuwa mtu wake wa karibu ungejua haya ninayokwambia. Fuatilia mawasiliano yangu na Ben tangu mwaka juzi ndio uone who are we. I still believe kuwa Mungu anamlinda Ben na nchi yetu haijafika huko

Mwigulu

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
24,905
2,000

Sasa kuhusu swala la Ben Saanane:

Kwanza tumwombee kwa Mungu awe salama mpaka sasa. Tafadhali usiandike kwa hisia zako.

Ben is my personal friend (Sio katika Siasa) tunakutana na kushirikisha mambo kila mara mpk ya familia, namfahamu na anaifahamu familia yangu mpaka watoto wangu wanamfahamu. Nilimsaidia kura za maoni ndani ya chama chake, nimewasiliana naye mfululizo mpaka wiki hiyo hiyo. Unamwongelea rafiki yangu na ndugu yangu wa ndani, na sasa nafuatilia kama serikali na kama rafiki.

Tafadhali, tuna mambo ya kisera tunaweza kupigana madongo, lakini hapa tunaongelea maisha ya mtu, an innocent young brother. Usikusanye vitu vya kuungaunga na kuleta katika jambo kubwa ambalo bado lina giza na wengine ni ndugu yao wa damu na wengine ni close friend.

Naamini mimi Ben ni rafiki wa karibu kwangu kuliko kwako mtoa mada maana ungekuwa mtu wake wa karibu ungejua haya ninayokwambia. Fuatilia mawasiliano yangu na Ben tangu mwaka juzi ndio uone who are we. I still believe kuwa Mungu anamlinda Ben na nchi yetu haijafika huko

Mwigulu
Mheshimiwa Mwigulu, wewe ni mtu mwenye dhamana. Kila mmoja anakuangalia na kwa umakini mkubwa wanasikiliza unaongea nini. Maelezo haya ungeliyatoa mwanzo nadhani "hali ya hwa" ingelikuwa tulivu!
All in all, tunakuombea kazi yako iwe na baraka katika uchunguzi wa Ben.
By the way: Mbona mnawaharass sana wapinzani?
 
rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,840
2,000
Labda unaweza kuwa suspect namba moja kwa sababu ni jukumu lako kuwaeleza wananchi what Is real going on,kama minister of police umeshindwa kuja na jibu LA kutosheleza basi ujue something wrong somewhere
Napenda nichukue nafasi hii kukueleza this nation belong to all of us,na kama nchi ni Mali yetu tuna haki ya kuhoji,kuuliza,kutoa maoni,kuwa na hasira nakadhalika
What is about to happen in our country you real going to pay for it!!!!!!
 
MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
8,947
2,000
Mkuu tumekusoma.

Tatizo ni kwamba hamtoi mrejesho (feedback) kwa haya matukio ndio maana watu wanakosa uvumilivu na wanakuja na arguments mbalimbali mbaya ambazo ndio zinawaibua kama wewe Mkuu ulivyoibuka.

Lini mmewahi kuutangazia umma kwamba hiyo miili 7 mmeshaifukua na kuchukua sample ya kila mwili for a test???? Hamjawahi kusema. Leo ndio umesema hapa.

Watu wataacha vipi kuwatuhumu huku wakiwaza hakuna lolote linaloendelea isipokuwa kila siku ni habari kubwa kubwa za John Faru..!!??

Issue ya Ben.. hamjawahi kutoa fdback pia.. Mpo kimya.

Mpaka mtu awalipue hapa JF ndio mnaibuka.

Na hata hapa kwenye maelezo yako haujasema lolote kuhusiana na effort gani zimeshafanywa na serikali kwenye kumtafuta. Ben Saanane, mtu aliepotea karibu mwezi sasa.

Natoa mfano tu, let's say angekuwa amepotea labda Le Mutuz... Mngekaa kimya namna hii??

Acheni kubagua eti kwasababu Ben alikuwa CDM na ni msumbufu basi wacha apotee tu... NO.. Big NO.

Ben is a human being and he has all the rights of living and protection in his Country.
 
tamsana

JF-Expert Member
Jan 13, 2012
844
1,000
Nampongeza aliyeku-suspect maana angalau tumepata maelezo japo bajo hayajajitosheleza. Mhe. Mwingulu tambua tu ya kwamba umebeba dhamana kubwa sana na sisi wananchi tunapenda kusikia neno kutoka kwako ili tusiwe kwenye maswali ambayo hayana majibu. baba siku zote ndie mwenye dhamana kubwa ya kutatua au kutoa solution ya matatizo ya familia, vivyo hivyo wewe unayo nafasi kubwa sana ya kutoa maelezo juu ya sintofahamu hii. nakupongeza kwa kujitokeza Mhe. Waziri.
 
Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,830
2,000
WanaJF,

Nimeamua (kama member wa JF) kuandika kwa masikitiko makubwa sana kufuatia uzi wa technically:

Mwigulu Nchemba ndiye suspect namba moja kupotea kwa Ben Saanane?

Vijana wenzangu, tuwe tunatafakari kwanza kabla ya kuaondika mambo makubwa yasiyo na utani bila kujiridhisha na tunachokiandika. Sio kitu kizuri kuandika jambo kubwa hivi kwa taarifa za kuungaunga na ufahamu wa kuungaunga.

1) Moja anasema watu wamezikwa bila kutambuliwa: Ni kweli watu hao miili ilishaharibika na hatua iliyokuwa inasitahili ilikuwa kuzikwa. Hata hivyo tumechukua sampuli kwa kila mwili nawe ukitaka kuitambua unaruhusiwa. Mpaka sasa haijulikani sana uhakika kuwa hao ni nani, lakini sisi tulisema kuna uhusiano mkubwa wa watu hao na wahamiaji haramu ambao waliokotwa 81 wakiwa mahututi eneo hilohilo na wiki hiyo hiyo.

Hatujasema kuwa ni kwa asilimia 100 ni wahamiaji haramu, tunasema huenda wakawa ni wao maana kama hao 81walikuwa hoi wiki hiyo hiyo huenda kati yao kukawa na baadhi yao ambao walishapoteza maisha na tukasema tuendelee na kutafuta undani zaidi, lakini wewe unasema tumezika bila kutambuliwa, hivi ni nani angewatambua? This is not fair.

Wapo wakadiriki hata kusema watu hao waliuwawa na Polisi, la hasha hata wakiwa wahamiaji haramu hawaruhusi kuuawa ndio maana Polisi ilipowaokota wale mahututi wakiwa hwawezi kuongea wala kusema iliwapikia uji na wengine kuwapeleka hosipitali.

Tunaongelea miili iliyookotwa, kumekuwa na kawaida ya wasafirisha watu kutupa miili hovyo, sishangai huenda hata wakawa walikuwa zaidi ya 81 wameokotwa saba, huenda wengine wakawa wamepelekwa baharini, ndio maana tunaendelea kutafuta undani.

2) Pili unasema kifo cha Mbagala kahusika Mwigulu, Eti alifika wa kwanza.

Si kweli, sikufika wa Kwanza. Angalia, kwanza tukio lilifanyika saa moja kwenda saa mbili hivi, akaenda OCD saa moja hivi, saa tatu akaenda RPC, saa nne akaenda Siro na IGP. Mimi nilienda Saa sita usiku na nimemkuta RPC na Kamanda Siro na video zipo. Niliwakuta na ndio walikuwa wananielekeza tukio lilipo. Unasema niliwatangulia polisi? Jitafakari. Yaani yote hayo ni kutaka kuhalalisha fikra potofu na kuchafua taswira ya mtu, kwanini unaandika kwa uhakika wakati ni vitu vya kusikia?

3) Tatu unasema swala la Lwakatare. Kwa sasa Lwakatare ni mbunge na ni rafiki yangu na anajua ukweli wa yote yale yaliotokea na tunaongea mara kwa mara. Nitakupa namba yangu, hebu tafuta siku tukakae na Lwakatare mimi nawe akisema nilimsingizia nitaacha ubunge na uwaziri.

Jana tu, tar 20/12/2016 ilikuwa kesi hiyo hiyo wewe unasema kesi ilienda mpaka ikaisha! Uwe unapata ukweli kabla ya kuandika. Jambo hili halijaisha jana ilikuwa kesi, lakini Lwakatare anajua hili jambo, tunaongea mara kwa mara nadhani ungeacha tu jambo hili liishe liliko kwenye mkono wa sheria, usilichokonoe hata Lwaka hangependa ulichokonoe kama unavyofanya kwani yeye anajua ukweli, namba yangu ni 0714008888

4) Unasema nilisema nitatoa ushahidi wa mauaji ya SOWETO. Ndugu, kapitie upya kumbukumbu zako. Nenda kaongee na Lema hata sasa kulekule alipo, muulizie maana naye mwanzo alikuwa na mtazamo kama wa kwako.

Ushauri wangu: Kuandika hapa jamvini suala serious kama hili ni vyema ukafanya fact finding kidogo

Sasa kuhusu suala la Ben Saanane:

Kwanza tumwombee kwa Mungu awe salama mpaka sasa. Tafadhali usiandike kwa hisia zako.

Ben is my personal friend (Sio katika Siasa) tunakutana na kushirikiana mambo kila mara mpaka ya familia, namfahamu na anaifahamu familia yangu mpaka watoto wangu wanamfahamu. Nilimsaidia kura za maoni ndani ya chama chake, nimewasiliana naye mfululizo mpaka wiki hiyo hiyo. Unamwongelea rafiki yangu na ndugu yangu wa ndani, na sasa nafuatilia kama serikali na kama rafiki.

Tafadhali, tuna mambo ya kisera tunaweza kupigana madongo, lakini hapa tunaongelea maisha ya mtu, an innocent young brother. Usikusanye vitu vya kuungaunga na kuleta katika jambo kubwa ambalo bado lina giza na wengine ni ndugu yao wa damu na wengine ni close friend.

Naamini mimi Ben ni rafiki wa karibu kwangu kuliko kwako mtoa mada maana ungekuwa mtu wake wa karibu ungejua haya ninayokwambia. Fuatilia mawasiliano yangu na Ben tangu mwaka juzi ndio uone who are we. I still believe kuwa Mungu anamlinda Ben na nchi yetu haijafika huko

Mwigulu
Nadhani ni muhimu pia ukaliweka sawa suala hili katika muktadha wa Uzi wako mwingine humu JF mwaka 2013 ukiwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (bara). Uzi huo unapatikana hapo chini

Red Brigade: Kikundi cha mauaji, watekaji, wamwagia sumu na "nchi kutotawalika"
 
mshunami

JF-Expert Member
Feb 27, 2013
3,976
2,000
Si vema kupiga ramli chonganishi! Ujumbe umefika kwa Mwigulu kama Waziri mwenye dhamana ya ulinzi wa raia na mali zao, kwamba angalao watu wanapenda kusikia kuwa vyombo vya usalama vinafanya nini katika hilo na vimefikia hatua gani. Taarifa tu toka kwao itazua ramli hizi!!
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
76,366
2,000
Sijaridhishwa na ufafanuzi wako kuhusu Lwakatare , lakini nina hoja kuhusu Ben , hivi kama wewe ni Waziri mwenye dhamana ya Usalama wa raia na mali zao kwanini usijiuzulu baada ya kushindwa kumpata Ben , ili upishe wengine wenye weledi kukushinda , ambaye unaonekana unafaa zaidi kwenye fitina za chama cha Mapinduzi kuliko uongozi wa serikali ?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom