X-PASTER
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 11,610
- 1,809
- Thread starter
- #21
Mkuu, kwa habari za kuaminika ni kwamba hao mashoga siku ile ya tamasha walialikwa rasmi na TGNP, na si kualikwa tu, walilipwa mpaka posho za maudhurio.Nakupinga jambo moja la TGNP kusupport mashoga sio kweli. Mi nilikuwepo kwenye matukio yote ya gender festival ambayo yanatumika kama platform ya watu kuongea kuhusiana na theme zinazowekwa. Na TGNP walijibu kuwa wao wanatambua jinsia mbili tu ya mwanamke na mwanaume...na sio mashoga au wasagaji.
Na kuhusu maadili ni kweli yanamong'onyoka kwa sababu ya utandawazi. Media inapositive na negative side...na negative side ndo hiyo so serikali inabidi iwe makini na media
Hii hapa chini ni mmoja wa waandishi Dada Gloria Tesha. Mwandishi wa habari kutoka gazeti la habari leo
Na hii ndio sehemu ya ripoti yake.
Gloria Tesha said:SIKUWEZA kujizuia kutokwa machozi pale nilipomuona mtoto wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 14 hadi 16 akitembea kwa kutingisha makalio, na kuzungumza huku akicheka kama mtoto wa kike katika Tamasha la 10 la Jinsia jijini Dar es Salaam lililofanyika wiki iliyopita.
Hata hivyo niligundua kuwa hayupo peke yake baada ya kuona kundi la vijana kama yeye wanaojulikana kama mashoga likipitia huku na kule katika tamasha hilo na wakati mwingine kujitambulisha kama wanawake.
Nilianza kuwaonea huruma wazazi wao na pia kuwalaumu lakini pia nikailaumu jamii na hata serikali kwa kuwa nilijua nguvu za taasisi hizo zingeweza kuwanusuru watoto na vijana hao kuwa mashoga kwa kuwa niliamini kibaiolojia zipo tiba na kisaikolojia pia.
Kilichonisukuma kuandika wazo hili pamoja na uchungu kwa hali ya vijana wale na pia baada ya kuona wanaharakati wakigawanyika kutokana na ushiriki wa mashoga hao katika Tamasha hilo huku wengi wakiilaumu TGNP kuwaalika mashoga hao katika tamasha hilo wakidai tabia na mambo wanayoyafanya vijana na wanaume hao si maadili ya Kitanzania na inahamasisha jamii iamini kuwa ni kitu cha kawaida.
Pamoja na malalamiko hayo, TGNP haikuwa wazi kueleza kuwa imewaalika au la baada ya kudai kuwa tamasha ni huru kwa kila mtu, halikubagua mtu kwa jinsia, kabila, dini au rangi.
Hata hivyo baadaye ilifahamika kuwa waliwaalika kwa kuwa waliwalipa posho ya ushiriki wao. Nami kwa sehemu nakubaliana na wanaharakati hao kuwa tamasha lilikuwa huru kwa kila mtu.
Hakuna aliyekasirika ushiriki wa yeyote, lakini kwa mashoga hawa, lawama zilikuwa nyingi kutokana na namna walivyojitambulisha kuwa ni wanawake wakati ni wazi ni wanaume na kutaka Katiba Mpya iwatambue huku baadhi ya wanaharakati wakionekana kuwatetea kuhusu suala hilo la Katiba.
Binafsi naona huu si utetezi wa haki za binadamu bali ni ukatili wa jinsia, najua nitawaudhi wengi katika hili, lakini nani asiyefahamu kuwa nchi hii inaongozwa na sheria na kanuni na iko wazi kuwa kumuingilia mtu kinyume cha maumbile ni kosa la jinai?
source: HabariLeo