Kuporomoka kwa kasi:Je CCM inaelekea mwisho wa kutawala Tanzania?

Malata Junior

JF-Expert Member
Nov 29, 2011
3,104
2,549
Heshima mbele wakuu.
Chama cha Mapinduzi (CCM) ni miongoni mwa vyama vichache vikongwe vilivyosalia vikitawala baadhi ya nchi za Afrika.Hata hivyo mwenendo wa chama hiki katika chaguzi mbalimbali unatia shaka kama CCM itaendelea kutawala Tanzania hasa katika uchaguzi ujao wa 2020.CCM mbali na kuporomoka kwa kura za urais kutoka 80% wakati uchaguzi wa vyama vingi ulipoanza hadi kufikia 58% kwenye uchaguzi mkuu uliopita wa 2015,CCM pia imepoteza viti vingi vya ubunge na madiwani ikiwemo kwenye maeneo ambayo yanasemekana ni 'ngome' yake.Kwa mara ya kwanza upinzani umeweza kuongoza Halmashauri zipatazo 30 tofauti na chaguzi zilizopita ambao upinzani uliongoza Halmashauri zisizozidi 5. Hali hii ni hatari sana kwa uhai wa CCM kwani ukiangalia grafu ya CCM tangu kuanza kwa vyama vingi inazidi kudidimia tofauti na vyama vya upinzani hasa CHADEMA ambayo kila uchaguzi inaongeza kura za urais, viti vya ubunge, udiwani na Halmashauri inazoziongoza.Wachambuzi na wataalamu wa mambo ya siasa wanasema sababu za kuporomoka vibaya kwa CCM mbali na ufisadi, wizi na ubadhirifu wa Mali ya umma pia kunachangiwa na sina ya makada wake wanaotumiwa kwenye kampeni za uchaguzi ambao hawatoi sera badala yake ni mipasho,matusi na kejeli dhidi ya wapinzani! Makada hao Livingston Lusinde,Joseph Msukuma,Christopher Ole Sendeka,Abdalah Bulembo na Maji marefu elimu ndiyo tatizo kwao lakini pia kuna makada waliosoma kama Nape Naye.Mwigulu Nchemba na Jamuari Makamba pamoja na kwamba wamesoma lakini wanafanya siasa za hovyo kuliko hata wale wasiosoma yote haya ni kujipendekeza ili wapate vyeo! CCM kama itaendelea kuwaamini watu hawa waendeshe chama hakuna chama hili kinakwenda kufa 2020. Haikushangaza wengi Magufuli alipojitenga na CCM aliposema chagua Magufuli,serikali ya Magufuli bila kujihusisha na CCM! Tusubiri tuone.
 
Back
Top Bottom