Kuporomoka kwa elimu yetu ni mpango mkakati wa ccm!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuporomoka kwa elimu yetu ni mpango mkakati wa ccm!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Miwatamu, Oct 11, 2012.

 1. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Ndugu wana JF nimelazimika kuleta thread hii mbele yenu ili tuweze kuijadili kwa pamoja kutokana na anguko la mara kwa mara la elimu katika taifa letu hili. Kwa wote wapenda maendeleo na wanaoamini kuwa msingi wa maendeleo ni elimu bora, watakubaliana na mimi kuwa kuporomoka kwa elimu yetu si kwa bahati mbaya. La, hasha! bali ni mpango mkakati wa kutaka kuendeleza kikundi kidogo kujitwalia mamlaka ya kiutawala hadi siku za dahali.

  Nathubutu kusema hivyo kutokana na vile viongozi wetu walivyo mstari wa mbele kuwakimbiza watoto wao kusoma nje ya nchi wakati huo huo sisi walala hoi tukiendelea kuona wanetu wakikaa vumbini, kuandikia kwenye magoti huku magogo ya miti yetu yakivunwa na kusafirishwa nje ya nchi usiku na mchana bila huruma! Kibaya zaidi walimu wetu wakilipwa kiduchu ili kuwapunguzia morali ya kazi na kuwafanya watoto wetu kuendelea kuwa mbumbumbu siku hadi siku.Thread yangu hii inathibitishwa na matokeo ya utitiri wa watoto wa vigogo walioko madarakani walivyochomoza ghafla ndani ya ulingo wa siasa huku wengi wao wakiwa hawana background ya kuwa wanasiasa. Hebu angalia hawa! Watoto wa vigogo waliochomoza ghafla ndani ya NEC na UVCCM ngazi ya Taifa:Ridhiwani Kikwete, Ashura Hussein Mwinyi, Dickson Membe,Fredy Lowasa, Beny Samwel Sita, Deborah Mwandosya, Iren Pinda, Felster Ndugai, Christopher Ndejembi, Sharifer Bilal,Hawa Kigoda, Judith Mkama na Jarome Msekwa.

  Tafakari! Kwanza kabisa kitu ninachotaka kuuliza, Je, hiki ndicho kile kikosi cha ushindi 2015 kilichosifiwa na Babu wa Bumbuli, Makamba? Nchi hii imekwisha! Inatia hasira. Mbona kuna vijana wengi tena wenye weredi wa kisiasa ambao wamekuwepo miaka mingi lakini hawapewi nafasi hata zile za ngazi za chini?

  Kwa matokeo haya ndiyo maana nasema kuwa kuporomoka kwa elimu yetu hapa nchini, ni mpango maalum kutoka kwa watawala wetu kutaka kuendeleza himaya zao na kuwafanya akina yakhe kuenedelea kuwa madaraja huku tukiwapigia makofi na kuwaita waheshimiwa hata kama hawastahili.Kwa picha hii watanzania sasa wanatakiwa kufungua macho ili kuiokoa Tanzania hii isiwe kampuni ya familia au kikundi fulani, badala yake iwe ni nchi ambayo inastahili kuongozwa na yeyote mwenye uwezo na upeo wa kuleta mabadiliko yenye tija kwa wote bila kuangalia itikadi zao na uwezo wao kiuchumi.
   
 2. SHIEKA

  SHIEKA JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 8,131
  Likes Received: 943
  Trophy Points: 280
  Asante kwa mada ya kusisimua. Hebu nieleweshe zaidi kuhusu hao watoto wa vigogo uliowataja. Kila uliyemtaja anashika wadhifa gani na kwenye kitengo gani?
   
 3. a

  adolay JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,567
  Likes Received: 3,026
  Trophy Points: 280
  Hujakosea, ni ukweli uliowazi. Kikwete anafaham vizuri ndio sababu anawapuuza walimu ili kufikia malengo.
   
 4. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Mbona ni lahisi tu mkuu wangu! Ingia kwenye wavuti wa ccm utapata kila kitu hapo.
   
Loading...