Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,859
Hatuna haja ya kumtafuta mchawi kutoka nje ya mfumo wenyewe wa elimu Tanzania. Hakuna haja ya kusema kuwa wanafunzi wanafelishwa tu na 'betting' au kuporomoka kwa maadili kwa wanafunzi hao. Pia, si kwamba wanafunzi wanafeli kwa kutofundishwa vizuri na kuongozwa vyema.
Pamoja na kuwa hizo na sababu nyingine huchangia kwa kiasi kikubwa katika kufelisha wanafunzi katika ngazi ya sekondari, kipo kiini cha tatizo. Kiini ni uwepo wa mitihani ya kuchagua tu wakati wa darasa la saba. Izingatiwe kuwa mitihani ya Taifa ya darasa la saba ndiyo inayopeleka wanafunzi kwenye shule za sekondari za Serikali.
Kama 'ku-bet', wanafunzi wanafundishwa kufanya hivyo wakati wanapofanya mitihani yao ya kumaliza darasa la saba. Haipendezi wala kuvutia kuona mitihani ya kumaliza darasa la saba ikiwa ya kuchagua tu. Hata mtihani wa Hisabati mwanafunzi haangaiki kukokotoa. Na kwa mitihani mingine, mwanafunzi hafikiri bali anaotea tu.
Matokeo ya mitihani ya kuchagua darasa la saba ni mabaya. Wanafunzi wengi wanaojiunga sekondari-tena wengine Shule za Vipaji Maalum wanakuwa wa uwezo wa chini mno. Wengine hawajui hata kuandika na kusoma vizuri. Lakini, mitihani ya kuchagua imewapa nafasi na kufaulu kwa kishindo.
Umefika wakati wa kuirejesha elimu yetu kwenye enzi yake ya kutukuka. Mitihani ya kuchagua ifutwe. Irejeshwe mitihani ya kupima uelewa badala ya hii ya kupima umahiri wa kuotea.Hata kama wanafunzi wataofaulu kwenda kidato cha kwanza watakuwa wachache,elimu yetu itakuwa bora. Hakuna haja ya kufaulisha maelfu darasa la saba halafu hakuna lolote la kuvutia kwa wanafunzi hao.
Ilipoanza tu mitihani hii ya kuchagua, kama mdau wa elimu Tanzania na mtanzania huru, niliandika makala kwenye gazeti la Raia Mwema nikiweka bayana kuwa mitihani ya aina hiyo huzalisha mbumbumbu. Matokeo ya kidato cha nne yanadhihirisha hayo. Makala yangu nyingine kuhusu jambo hilo, waweza kuisoma hapa:Serikali haiyaamini matokeo darasa la saba? – Raia Mwema.
Elimu yetu lazima ilindwe.