Kuporomoka kwa ccm kutakuwa na mshido utakao potea ghafura. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuporomoka kwa ccm kutakuwa na mshido utakao potea ghafura.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gudlucky, Apr 15, 2011.

 1. Gudlucky

  Gudlucky Member

  #1
  Apr 15, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu watanzania waaminifu wenye kupenda kuona maendeleo ya nchi yao na ustawi wake kwa ujumla, Salam sana....

  Jamani, siku zote mfa maji hakosi kutapatapa, na mara nyingi mtu akaribiapo kukata roho hutupa miguu na mikono huku na kule akigeuza shingo yake mara huku mara kule, uso wake na hali ya muonekano wake ukiwa umejawa hofu na woga wa mauti. Hatimaye muda kitambo utaona kimya kilicho ambatana na utulivu kimetanda. Hii ndiyo inatokea sasa kwa CCM. Ni dhahiri kabisa chama hiki kimeanza kutapatapa kutokana na kule kufunuliwa kwa uovu wao na kuwa watupu mbele ya watanzania. Hali hii iliyopelekea wananchi kupoteza imani yao na CCM imewafanya CCM kuanza kupoteza muelekeo sahihi na kujikuta wakienda sehemu nyingine tofauti.

  Ndugu watanzania, mtakubaliana nami kuwa CCM sasa imepoteza dira, haina jipya kabisaa. Kitu kikubwa wanacho nishangaza ni hiki; Kutokana na makosa (mistakes) waliyoyafanya kupoteza imani ya wananchi kwa chama hicho wameanza kusingizia vyama, vikundi na vyombo vya habari mbalimbali kuwa wanawachafulia jina, mara wanavunja amani n.k badala ya kukaa chini na kutafuta ufumbuzi wa migogoro na matatizo waliyolisababishia taifa na watanzania kwa ujumla. Hawa wananikumbusha mithali isemayo, 'Mbaazi ikikosa maji ikakauka husingizia jua' ooh! Wanashangaza sana.

  Naomba nieleweke, sisemi hivi kwa sababu eti naichukia CCM, bali kwa sababu ya tabia na vitendo wanavyoonesha sasa. Ikumbukwe kuwa, Jana katika taarifa ya habari TBC1 Pius Msekwa alisikika akiishutumu JF kuwa ni chanzo cha CCM kuchukiwa eti kwa sababu inaichafua CCM kwa umma wa Tanzania. Sasa kweli tujiulize, Ni kweli JF inaichafua CCM, au ni watanzania wanatoa sauti zao zilizojawa na ukweli mtupu?

  Mioyo ya watanzania yenye kiu (desire) ya kutaka kuona mabadiriki kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na hata kisiasa inataka kufika mahala ambapo itatuliza kiu hiyo au kuimaliza kabisa. Kwa sababu hiyo wanatafuta watu halali, waaminifu, jasiri, wakweli na wenye nguvu ya kuwafikisha wanapotaka kufika na si watu wanaowarudisha nyuma na kuzidisha kiu yao. Si kama zamani miaka ile, sasa mioyo ya watanzania haina imani na Chama hiki, na kwa sababu hiyo ni lazima waseme. Watasemea wapi sasa, ikiwa baadhi ya vyombo vya habari mmevifumba vinywa na kuzizuia sauti za watanzania zisikike? JF ni chombo cha jamii, kitasema kweli siku zote kupitia sauti ya Watanzania. Kiacheni, kipeni uhuru jamani!

  Jamani, nimalizie kwa kusema, Hayawi hayawi huwa, siku zinakwenda mbele hazirudi nyuma na Imani ya wananchi kwa CCM inatoweka mithili ya kipande cha mshumaa moto uwakapo juu ya tambi nyembamba iliyoshikwa na mshumaa huo. Punde si punde mshumaa uisha na hauwezi kuutengeneza (restore) tena, ndivyo ilivyo CCM. Time will tell.
   
 2. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  ccm ni kama jeshi ambalo liko vitani lakini halimjui adui yake, yeyote akitokea kuwakosoa au kutaka kuwaonyesha njia huyo ndo anashambuliwa utawasikia mara Cdm na misaada toka nje, magazeti, sijui wasomi, mara malecturer,ooh wanafunzi wa vyuo vikuu, mara wastaafu yaani vuruvuru hawaeleweki. Yaani kama wanajeshi waache wamalize risasi na nguvu nyingi kupigana na hewa afu wakiwa empty ndo adui wao wa ukweli ambaye yuko katikati yao ndo atakapojitokeza watakuwa hawana nguvu wala silaha bali watashindwa kilaini na hapo kuna mawili kujisalimisha au kubisha wachakazwe mbaya kabisa !! CCM siku ya kiama kwenu haiko mbali tubuni na kuziacha dhambi zenu la sivyo mtaingia ktk vitabu vya historia na kuongeza mifano kama KANU
   
Loading...