Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 10,233
- 17,457
Haya matukio yanaonyesha kuporomoka kwa hadhi ya Ki-diplomasia kwa Tanzania.
1. Tanzania imekaa bila Balozi kamili wa USA kuanzia Oktoba 2016 alipoondoka Mark Bradley hadi Novemba 2019 alipoteuliwa Dr Don Wright. Kwa miaka 3 tulikuwa unafanya kazi na Inmi Patterson ambaye kicheo ni Charge D'affaire.
2. EU ilimuita nyumbani Mkurugenzi wake wa Tanzania Roeland van De Geer mnamo Novemba 2018, ilikuwa mwaka mzima hadi ilipomteua Manfredo Fanti kujaza nafasi hiyo.
3. Waziri wa Mambo ya Nje (Secret of State) wa USA Mike Pompeo amekwishaanza kutoa majina ya watu wasioruhusiwa kwenda USA. Ameanza na Paul Makonda kutokana na rekodi yake mbaya kwenye kunyang'anya haki ya kuishi ya Watanzania wengine, kudhibiti upinzani, kukandamiza uhuru wa kujieleza nk
4. Donald Trump ameitaja Tanzania pamoja na Kirgystan, Eritrea, Nigeria na Sudan kati ya nchi ambazo wananchi wake hawatoshiriki green card lottery na watadhibitiwa wanapoingia USA
5. Taasisi zisizo za Kiserikali za Amnesty International, Transparency International na Human Rights Watch zimeiorodhesha Tanzania kama nchi ambayo imeporomoka katika usimamiaji wa haki za Binadamu na Ufisadi. Kwa mfano Transparency International inaiorodhesha Tanzania kama nchi ya 99 katika nchi 180 kwenye corruption Index
6. Mashirika ya misaada ya kimataifa kama WB, EU, USAID, SIDA wamekuwa yakisita au yakipunguza msaada ya Maendeleo kwa Tanzania
Hayo sita ni machache kati ya mengi ambayo yanaifanya nchi yetu ambayo ilikuwa ni Tegemeo kwa amani na utulivu wa eneo la maziwa makuu ionekane nchi ya kawaida tu kama Burundi au Malawi. Toka tupate Uhuru mwaka 1961 Tanzania iliheshimika sana katika duru za diplomasia ya kimataifa kutokana na juhudi za Baba wa Taifa Mwl Nyerere na Marais wote 3 waliomfuata. Hali ilivyo kwa kipindi cha JPM siyo nzuri kabisa na siyo jambo la kuacha lipite hivi hivi.
*SULUHISHO*
Tufanye mabadiliko uchaguzi wa 2020, twende na Bernard Camilius Membe iwe ndani ya CCM au Upinzani.