Kupooza vidonda vya uchaguzi ninamshauri JK na CCM kumuenzi Dr. Slaa kwa uspika.....


Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
634,713
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 634,713 280
Huu ni ushauri wa bwerere ingawaje ninapaswa kuwatumia CCM na haswa JK bili ya ushauri huu wa kitaalamu ya kuwa namna pekee ya kuwapooza watanzania ni kuiachia Chadema imteue Dr. Slaa awe spika wa bunge na serikali ya CCM kuahidi kuandaa muswada wa kuifanya NEC iwe huru na ya haki kuwezesha chaguzi zijazo ziendeshwe kwa misingi ya kiutu...........

Na sifa za NEC huru ni hizi zifuatazo:-

a) Wawepo wajumbe tisa wa NEC na wachaguliwe kwa utaratibu wa kutoka kwenye maeneo haya:-

i) Chama cha Majaji na Mahakimu ziteue wajumbe wawili kwa kura za wajumbe wake ambazo ni za wazi kwa hakimu mmoja na jaji mmoja. Lazima nafasi moja iende kwa jinsia tofauti ili mwanaumme na mwanamke wapatikane.....

ii) Chama cha wanasheria nchini cha bara na Zanzibar kila kimoja kiteue mjumbe mmoja mmoja na hivyo kuwa na wajumbe wawili. Lazima nafasi moja iende kwa jinsia tofauti ili mwanaumme na mwanamke wapatikane.....

iii) Vyama visivyokuwa vya kiserikali yaani NGOs zote ziteue wajumbe wawili tu kwenye tume hiyo. Lazima nafasi moja iende kwa jinsia tofauti ili mwanaumme na mwanamke wapatikane.....

iv) Vyama vya siasa viteuwe nafasi tatu kulingana na idadi ya kura za uchaguzi wa wabunge zikijumlishwa na zile za Uraisi na hivyo nafasi hizi kupatikana kwa asilimia za majumuisho hayo.

v) Mwenyekiti wa NEC kuchaguliwa na wajumbe hao tisa badala ya kuteuliwa na Raisi.Tume hii ni lazima ithibitishwe na bunge na ajira yake hatma yake kuwa bungeni tu na wala siyo kwa watendaji serikalini

vi) Tume kuajili makamisaa wa majimbo wa kudumu ambao watawajibika moja kwa moja kwao badala ya utaratibu uliopo wa kuazimwa kutoka serikali za mitaa..ambako mgongano wa kimasilahi umejitokeza.......

vii) Tume iwe inatoa ajira za muda mfupi za wasimamizi wa vituo vyote vipato 52, 000 na kuondoa waalimu kununuliwa na serikali iliyopo madarakani kwa peremende za kuongezwa mishahara nyakati za uchaguzi........

viii) Tume ya uchaguzi iwe inatenga bajeti za kuwalipa mawakala wote wa vyama vya siasa ili kuondoa hisia ya kuwa vyama vya upinzani mawakala wake hurubuniwa na chama tawala kutokana na ukata walionao.....
Wajumbe wa NEC waruhusiwe vipindi viwili vya miaka mitano mitano tu na baada ya hapo wajumbe wengine wateuliwe.............
Haya ni mazingira ya uchaguzi wa huru na wa haki na damu kamwe haiwezi kumwagika.......
 

Forum statistics

Threads 1,237,971
Members 475,809
Posts 29,308,297