Kupooza kwa uso upande mmoja huenda kusipone ukichelewa kupata matibau bell`s palsy

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
KUPOOZA KWA USO UPANDE MMOJA HUENDA KUSIPONE UKICHELEWA KUPATA MATIBABU

SUMMARY​

Mshipa wa fahamu, facial unaposhindwa kufanya kazi vizuri matokeo yake ni misuli ya uso inayoratibiwa nao kutotekeleza majukumu yake kwa ufanisi hivyo kusababisha uso kupooza. Kwa wengi, hali hii hutokea upande mmoja wa uso; kulia au kushoto ingawa huweza kuwa uso mzima yaani pande zote mbili.

Yapo maradhi mengi yanayoweza kuushambulia uso, kupooza kwa uso ni kati ya hayo. Hili ni tatizo la kushindwa kufanya kazi upande mmoja au uso mzima kutokana na mshipa wa fahamu unaoitwa facial kushindwa kufanya kazi ipasavyo.

Mshipa wa fahamu, facial unaposhindwa kufanya kazi vizuri matokeo yake ni misuli ya uso inayoratibiwa nao kutotekeleza majukumu yake kwa ufanisi hivyo kusababisha uso kupooza. Kwa wengi, hali hii hutokea upande mmoja wa uso; kulia au kushoto ingawa huweza kuwa uso mzima yaani pande zote mbili.

Sababu
Kupooza kwa uso husababishwa na mambo mbalimbali na tatizo linaweza likaanza ghafla au likachukua muda mrefu kabla ya kuonekana. Sababu hizo ni zifuatazo:

Kiharusi
Sababu ya kupooza kwa uso ni kiharusi ambacho kinapotokea huweza kuathiri eneo la ubongo lenye mshipa wa fahamu wa facial hivyo misuli ya uso kupooza.

Kiharusi husababisha chembe hai za ubongo kufa kutokana na ukosefu wa hewa safi na virutubisho au shinikizo litokanalo na mkusanyiko wa damu iliyovuja kutoka kwenye mishipa ya damu iliyopasuka. Kiharusi husababisha chembe hai kufa haraka sana. Watu wanaopooza uso kutokana na kiharusi hupoteza uwezo wa kutambua watu, wakati au maeneo, huonekana kama wamechanganyikiwa na mara kadhaa hupata kizunguzungu.

Vilevile, wapo wanaopoteza fahamu, kupata kifafa au kushindwa kuona vizuri. Baadhi hushindwa kufanya shughuli za kawaida na wachache hupooza upande wa mikono au miguu.

Bell`s palsy
Bell`s palsy ni maradhi mengine yanayosababisha mshipa wa fahamu wa facial uvimbe na kushindwa kuratibu vizuri ufanyaji kazi wa misuli ya uso. Tatizo hili mara nyingi huathiri mshipa wa upande mmoja na madhara yake huko.

Hii ni sababu kubwa ya kupooza kwa uso kwa watu wengi duniani. Bado haifahamiki kwa uhakika bell`s palsy husababishwa na nini lakini imedhihirika kuna uhusiano na maambukizi ya virusi.

Dalili za bell`s palsy ni pamoja na kupooza upande mmoja wa uso, ni mara chache husababisha kupooza kwa uso mzima, na kushindwa kufunga au kufungua jicho moja la upande ulioathirika.

Nyingine ni kukosekana machozi kwenye jicho la upande uliopooza, kushindwa kuhisi ladha ya chakula, kinywa kupooza kwenye upande ulioathirika na kushindwa kutamka vizuri kiasi cha kueleweka.

Wapo wanaoshindwa kuzuia mate yasitoke upande wa kinywa uliopooza bila kuwa na uwezo wa kuyazuia, kuhisi maumivu kwenye sikio la upande ulioathirika na sikio la upande ulioathirika kusikia sauti kubwa zaidi kuliko hali halisi au kupata ugumu kula au kunywa kitu chochote ikiwamo maji.

Watu wengi wenye bell`s palsy hupona baada ya matibabu yanayochukua takribani miezi sita. Tofauti kati ya watu waliopooza kutokana na kiharusi na wale waliopooza kutokana na bell`s palsy ni kuwa waliotokana na kiharusi huwa na uwezo wa kuchezesha ngozi ya upande wa uso ambao haujaathirika. Vilevile huwa wana uwezo wa kufunga na kufungua jicho la upande ambao haukuathirika.

Watu waliopooza kutokana na bell`s palsy hushindwa kufanya lolote kwenye upande wa uso ambao haukupata tatizo. Sababu nyingine za kupooza kwa uso ni maradhi ya sikio hasa yanayoshambulia eneo la kati, hitilafu ya mfumo wa ulinzi wa mwili kwa mfano multiple sclerosis au ajali iliyoathiri kichwa au uso.

Nyingine ni maradhi ya lyme ambayo husambazwa na kupe ingawa hayapo kwa wingi nchini, uvimbe kichwani, shingoni au kwenye ubongo au kupooza wakati wa kujifungua huweza kusababisha tatizo kwa mtoto kama mshipa wake wa facial utajeruhiwa wakati wa kuzaliwa. Wapo pia wanaopooza kutokana na maradhi ya kuzaliwa nayo kama vile mobius.

Matibabu
Baada ya kupata dalili nilizoorodhesha awali mgonjwa hutakiwa kwenda hospitali ambako ataonana na daktari atakayesikiliza historia ya tatizo na kufanya vipimo muhimu. Baada ya kufanya vipimo daktari atatoa matibabu kadri inavyostahili.

Watu waliopooza kutokana na bell`s palsy hupona bila matibabu yoyote ingawa dawa yaweza kutolewa ili kuharakisha kupona. Mazoezi ya misuli nayo husaidia kurejesha hali ya kawaida ya uso na kuzuia ulemavu wa uso.

Kwa waliopata tatizo kutokana na kiharusi matibabu huhusisha dawa za kuzuia madhara zaidi kwenye ubongo. Mafanikio ya matibabu ya kiharusi hutegemea ilichukua muda gani tangu tatizo lilipotokea mpaka matibabu hayo yalipotolewa.

Matibabu ya kiharusi pia huhusisha mazoezi maalumu ya viungo na misuli iliyoathirika kutokana na kiharusi. Mazoezi hayo huwa na lengo la kurejesha hali ya kawaida au kuendelea kutumia misuli hiyo na viungo vilivyoathirika.

Kwa wale waliopata tatizo kutokana na sababu nyingine matibabu hutegemea chanzo cha tatizo. Kama ni maradhi yenye tiba basi mgonjwa hupatiwa tiba hiyo ili kuondokana nayo. Kwa wale ambao sababu ya kupooza huko haina tiba huwa wanafanyiwa mazoezi ya kuwawezesha kuishi na hali hiyo.

Madhara
Wagonjwa wengi kati ya wanaopooza kutokana na bell`s palsy hupona kabisa baada ya miezi sita mpaka mwaka mmoja. Tatizo kubwa kwa watu wanaopooza kutokana na bell`s palsy huwa ni kupoteza uwezo wa kufunga au kufungua kabisa jicho la upande ulioathirika.

Hii huathiri maji maji yanayokuwapo hivyo mara nyingi jicho huwa kavu hali ambayo huathiri uwezo wa jicho hilo kuona kwa kiasi fulani.
Kwa waliopata tatizo kutokana na kiharusi matokeo ya matibabu hutegemea ilichukua muda gani tangu tatizo lilipotokea mpaka matibabu yalipopatikana. Hii maana yake, kuna umuhimu mkubwa wa matibabu ya haraka kupatikana mara tu baada ya mtu kupata kiharusi.

Wagonjwa hufaidika na mazoezi maalumu ya misuli iliyopooza. Mazoezi hayo husaidia kupunguza ukubwa wa tatizo na kuboresha muonekano wa uso.

Tatizo la kupooza uso kwa watu wengi huwa halitibiki na kuwezesha hali ya uso kurudi kama awali. Hii ina maanisha watu wengi huishi maisha yao yaliyobaki wakiwa na athari za kupooza kwa uso.

Ni vyema waathirika wakawahi kufika hospitali kwa ajili ya matibabu na kuonana na wataalamu wa saikolojia ili waweze kupatiwa matibabu ya kisaikolojia yatakayowawezesha kuishi wakiwa na mabadiliko mapya ya muonekano wao.

Ikishindikana kupona Hospitalini maradhi yako ya kupooza uso upande mmoja nitafute mimi Kwa wakati wako ili niweze kukutibia maradhi yako

mouth-stroke.jpg
 
Huu ugonjwa sitakaa niusahau uliwahi kunipata 2015 ila nashukuru M/Mungu nilipona baada ya mwezi mmoja tu nikarejea katika hali ya kawaida.
 
Ulipona kwa tiba gani mzee baba

Nilienda hospitali mzee nikafanyishwa mazoezi ya misuli.
Walikuwa wananiwekea kipande cha taulo kwenye upande uliopoza then kuna kifaa kama pasi hivi walikuwa wanakichomeka kikipata moto wananiwekea juu ya ile taulo kwenye uso wanapasha misuli iliyopooza na bada ya hapo wananifanyia massage ya uso( 3 times per wek).

Baada ya mwezi mmoja nikapona vizuri wala hakuna dawa nyingine walionipa zaidi ya hayo.
 
Nilienda hospitali mzee nikafanyishwa mazoezi ya misuli.
Walikuwa wananiwekea kipande cha taulo kwenye upande uliopoza then kuna kifaa kama pasi hivi walikuwa wanakichomeka kikipata moto wananiwekea juu ya ile taulo kwenye uso wanapasha misuli iliyopooza na bada ya hapo wananifanyia massage ya uso( 3 times per wek).

Baada ya mwezi mmoja nikapona vizuri wala hakuna dawa nyingine walionipa zaidi ya hayo.
Aisee haya maradhi nadhani yanaponeka ila hatujataka kufanya tafiti zaidi.

Kuna moja ya kufanya massage kwa kutumia silicone cups zile za kufanyia hijama.

Kuna vikijombe viduchu special kwa ajili ya massage ya uso tu,nilijsribu kuzitafuta nikaona kuna baadhi ya articles zinasema ziko effective kutibu hizo facial paralysis
 
Ilikuwaje mkuu.

Na je ulikupata ukiwa na umri gani
Mwaka 2017 mkuu nikiwa na umri wa miaka 22 ulianza kwa kucheza mdomo wa juu kabla ya kuweka kama kishimo na ulimi ulikiwa kama mtu aliengua na chai hivi yaani kifupi dalili zote hapo nilipitia na ni kweli..!!

Ilinichukuwa kama miezi miwili ya tiba hatimae nikakaaa sawa namshukulu mungu hadi sasa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom