commonmwananchi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2011
- 3,377
- 1,952
Inakuuma nini, wewe si rais wako ni mbowe.Mimi sio mpinga maendeleo. Ninasapoti kwa asilimia zote maamuzi chanya yenye lengo la kukuza uchumi wa taifa hili changa. Ukiwemo uamuzi huu wa kufufua Shirika la Ndege kwa kununua ndege 7. Kongole Serikali!
Hata hivyo, kuna mambo yanatutia aibu. Mojawapo ni hili la mapokezi ya hizi ndege kufanywa kuwa ni tukio special sana la kitaifa. Kwa lugha ya mtaani tunasema ni 'kuchoreshana'.
Kwa dunia ya sasa, hata kama tulikuwa hatuna, sio fahari kuitangazia dunia kwamba tunasubiri ndege airport, tena tukiongozwa na Rais!? Sijaona Kenya wakifanya, Ethiopia, South Africa, Nigeria, Rwanda na kokote kunakotuzunguka. Mambo gani haya?
Halafu mbaya zaidi, siku zote hizi za mapokezi ni lazima RAIS ahudhurie kama mgeni rasmi. Ni kuonesha kwamba it is our top priority for now as a nation. Really? Waziri na watu wachache wangetosha sana kutuwakilisha. Na hakuna ulazima wa kufanya live coverage kwenye redio na televisheni.
Huko baadae zitakuja treni za kisasa, tutafanya hivi pia?
Sasa huyu anakuhusu nini si mumuache aboronge ili mumuangushe mumuweke membe wenu au?
Kazi ya chadema imeporomoka toka chama cha upinzani, hadi genge la wambea watoa matusi mitandaoni loh!
Sent using Jamii Forums mobile app