Kupokea Ndege kufanywa ni tukio la kitaifa ni ushamba, tunachoreshana..

Mtapata tabu sana, kwan kuna ubaya gani rais akienda kuipokea.
Mbona Mwenyekiti wa taifa na Cabinet yake walienda kuzika mbwa wa Nassari lakini Ukerewe hawakwenda?
Kupanga ni kuchagua kama unaona ni vibaya rais kupokea lala tu nyumban au fanya mambo yako.
Hivi ujasiri wa kuicompare Tanznia na Chadema huwa mnaupata wapi wa ndugu?-pili naomba unisaidie-wale waliofariki kwenye ile meli walikuwa watanzania au wanachadema?na kwa mtazamo wako na pole pole ulitaka Chadema waende kufanya nini?Hivi tunapata faida gani kuwekeza kwenye huu ujinga?
 
Tukiangalia tulipotoka na tulipo kwenye sekta ya anga, ni jambo la kupengeza kwa jitihada hizo zilizochukuliwa.
 
Kwa kweli mm sijajua slogan ya kubana matumizi yanatumika wapi maana kwenye maandalizi ya kupokea ndege lazima mamilioni ya hela yametumika ikiwemo:
Kuandaa ukumbi
Vikundi vya ngoma
Mafuta ya gari
Kukodi vyombo vya muziki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sio mpinga maendeleo. Ninasapoti kwa asilimia zote maamuzi chanya yenye lengo la kukuza uchumi wa taifa hili changa. Ukiwemo uamuzi huu wa kufufua Shirika la Ndege kwa kununua ndege 7. Kongole Serikali!

Hata hivyo, kuna mambo yanatutia aibu. Mojawapo ni hili la mapokezi ya hizi ndege kufanywa kuwa ni tukio special sana la kitaifa. Kwa lugha ya mtaani tunasema ni 'kuchoreshana'.

Kwa dunia ya sasa, hata kama tulikuwa hatuna, sio fahari kuitangazia dunia kwamba tunasubiri ndege airport, tena tukiongozwa na Rais!? Sijaona Kenya wakifanya, Ethiopia, South Africa, Nigeria, Rwanda na kokote kunakotuzunguka. Mambo gani haya?

Halafu mbaya zaidi, siku zote hizi za mapokezi ni lazima RAIS ahudhurie kama mgeni rasmi. Ni kuonesha kwamba it is our top priority for now as a nation. Really? Waziri na watu wachache wangetosha sana kutuwakilisha. Na hakuna ulazima wa kufanya live coverage kwenye redio na televisheni.

Huko baadae zitakuja treni za kisasa, tutafanya hivi pia?
Wengine tumesema haya hadi mate yamekauka.
Ethiopia wana madege zaidi ya 70. Wangehitaji siku ngapi kufanya mapokezi kama ya kwetu?
Kenya wanazo zaidi ya 40. Wangehitaji siku ngapi?
Tukio moja kama kielelezo ikikuwa inatosha sana.
 
Masahihisho,Ethiopia wana Ndege 100+ zikiwemo bombandia 17,Boeing 737-700 na boeing 737-800,wana Boeing 787-8 na Boeing 787-9 na Airbus 350
Kenya wana ndege kama 35 or less zikiwemo boeing 787-8 (Dreamliner 7) Embrarer E190 ndege 15 na boeing 737-800
 
Soma katika biblia shilingi iliyopotea, Luka 15: 9 "........Na akisha kuipata atawaita marafiki zake na majirani na kuwaambia, ‘Furahini pamoja nami; nimeipata ile shilingi yangu iliyopotea!’

Binafisi sioni huu ni ushamba hata kidogo, ni kufurahia tu manunuzi ya ndege. Happiness is an attitude, let them me happy!
 
Hili shirika lilikuwa limekufa kabisa. Leo lina ndege sita, ipo kila sababu ya rais kwenda kuzipokea. yeye ndio kaidhinisha manunuzi kuna ubaya gani akienda mwenyewe kutazama bidhaa aliyoinunua?.

Hawa wanasumbuliwa na kasumba, wanamuona Ngosha mshamba kumbe wao ndio washamba.
 
Ukifuatilia post za wasanii wengi na celebs wa bongo wamepost maneno ya kusifia ujio wa hii ndege na wote wamemtag msigwa, nahisi ndie aliedhamini hizo post

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukifuatilia post za wasanii wengi na celebs wa bongo wamepost maneno ya kusifia ujio wa hii ndege na wote wamemtag msigwa, nahisi ndie aliedhamini hizo post

Sent using Jamii Forums mobile app
JPM na serikali yake wana akili sana. Wamewapiga chenga, mwishowe mnawaza ushamba na kuchoreshana wakati wenzenu wako kwenye siasa, wakifanya kampeni ya kuongeza idadi ya kuungwa mkono. Subiri wakati wa uchaguzi ndiyo mtajua iliakuwa ushamba au la. Safari hii hawana haja ya kuiba kula tena....mark my words......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom