Kupokea Ndege kufanywa ni tukio la kitaifa ni ushamba, tunachoreshana..

Tukiwa tunasubiri ndege yetu ya airbus ya pili kuwasili, heko na shamra shamra za kuipokea zikiwa zinapamba moto, kuna baadhi watasema huo ni ushamba.

Lakini, ni kweli sherehe za kupokea ndege na kupiga picha ni ushamba?

Je sherehe zote zile ni kwa ajili ya ndege au kuna ziada?

Baadhi wanaweza hoji kuwa kinacho sheherekewa ni ushindi dhidi ya watu walioliuwa shirika letu la ndege. kwa hiyo kila ndege mpya inapokuja lazima kuwe na kumbukumbu ya kuwachoma wale waliotaka kulimaliza shirika letu.

Mwingine anaweza kusema kila ndege inapouja kuna "shujaa" anaye ambatanishwa na shughuli. Mfano mhadisi aliyeshiriki kuitengeneza Dreamliner au kapteni aliyeitorosha ndege toka Kenya. Hawa walionesha kuwa watanzania wanauthubutu wa kufanya mambo makubwa, na hivyo kwa kutumia sherehe hiyo tunakumbushwa kuwa tunaweza.

Pia sherehe zinaweza kuwa ni kwa ajili ya kuonesha watanzania jinsi kodi zao zinavyotumika. Ni vigumu kuwapa moyo walipakodi kama hawaoni matunda ya kodi zao. Sasa wakiona dude linatua, wanapata fahari ya kuona jinsi walivyoshiriki katika ujenzi wa Taifa lao.

Mwisho, Kunaweza kuwa na tafsiri nyingine nyingi tu za nini hasa maana ya sherehe hizi kubwa za kupokea ndege.

Je unafikiri sherehe hizi ni ushamba?

Mashirika mengine ya ndege huwa yanatangaza ujio wa ndege zake mpya kwenye mass media, magazeti, radio, luninga, na billboards. Sisi tumeamua kutangaza uwepo wa ndege mpya kwa kupitia mapokezi..... its OK
 
Tukiwa tunasubiri ndege yetu ya airbus ya pili kuwasili, heko na shamra shamra za kuipokea zikiwa zinapamba moto, kuna baadhi watasema huo ni ushamba.

Lakini, ni kweli sherehe za kupokea ndege na kupiga picha ni ushamba?

Je sherehe zote zile ni kwa ajili ya ndege au kuna ziada?

Baadhi wanaweza hoji kuwa kinacho sheherekewa ni ushindi dhidi ya watu walioliuwa shirika letu la ndege. kwa hiyo kila ndege mpya inapokuja lazima kuwe na kumbukumbu ya kuwachoma wale waliotaka kulimaliza shirika letu.

Mwingine anaweza kusema kila ndege inapouja kuna "shujaa" anaye ambatanishwa na shughuli. Mfano mhadisi aliyeshiriki kuitengeneza Dreamliner au kapteni aliyeitorosha ndege toka Kenya. Hawa walionesha kuwa watanzania wanauthubutu wa kufanya mambo makubwa, na hivyo kwa kutumia sherehe hiyo tunakumbushwa kuwa tunaweza.

Pia sherehe zinaweza kuwa ni kwa ajili ya kuonesha watanzania jinsi kodi zao zinavyotumika. Ni vigumu kuwapa moyo walipakodi kama hawaoni matunda ya kodi zao. Sasa wakiona dude linatua, wanapata fahari ya kuona jinsi walivyoshiriki katika ujenzi wa Taifa lao.

Mwisho, Kunaweza kuwa na tafsiri nyingine nyingi tu za nini hasa maana ya sherehe hizi kubwa za kupokea ndege.

Je unafikiri sherehe hizi ni ushamba?
Tena ni ushamba uliopitiliza
 
Hakuna hata mmoja humu duniani ambaye hakupitia stage ya ushamba,kabla ya kujua/kukifahamu kitu chohote ni lazima upitie kwanza kwenye ushamba then unakuwa mjuaji,kwahiyo wacha tu tupitie huu ushamba kama kuna watakaoita kupokea ndege ni ushamba,baada ya muda tutakuwa tumezoea na maisha yatasonga..
 
Haiwez ikawa ushamba mana naona ni njia moja yapo ya mkuu wa nchi kuwaambia wananchi wake mafanikio anayowaletea ndo mana unaona hotuba ya rais huwa anaongea mengi hata nje ya TUKIO lenyew kuwambia hiki ni kidogo vingi nafanya

Sent using Jamii Forums mobile app
ni nchi gani nyingine iliyonunua ndege ukaona inasherehekea kishamba namna kama mnayosherehekea nyinyi ?
 
Nafikiri kinachofanyika sio ushamba ni aina fulani ya kutoa taarifa nje na ndani ya nchi kuwa Tanzania ile ambayo ilikuwa na ndege moja au shirika lake lilikuwa linalegalega sasa imefufuka na kupata ndege mpya. Hivyo nguvu kubwa ni kuitangazia dunia kuwa sasa Tanzania inasonga mbele kwenye mambo ya usafirishaji wa anga hivyo watalii na wafanyabiashara wasibabaike kwenye eneo hilo hivyo kwa hali tuliyokuwa nayo sio ushamba tunajitangaza.
 
Mimi nipo jirani na tv nasubiria muda ufike Ndege yeetu....ile...paaale....ndege...yeeetu...ile..paale

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani kuna maana Zaidi ya kushangilia. Kama ni mali yako utashangilia. Kama si yako hutafanya hivyo. Hebu fikiria umeagiza gari toka Japan kupitia kampuni ya Be forward, na mara unaambiwa njoo gari yako imefika bandari ya Dar es Salaam. Utanuna? Basi kupokea ndege kwa mbwembwe ambayo hatujaikodi wala kuazimwa si ushamba.
 
Upo sahihi, tunaonekana washamba sana, waziri alikuwa anatosha, Rais alipopokea dreamliner ilitosha kabisa. Sasa kila ndege tunapokea nama coverage kibao. Duh!!
Acha mwanaume ajinafasi kwa ahadi za kweli alizotuahidi wapiga kura wake hutaki kuangalia tune hata wasafi TV uangalie ule wimbo unaoupenda WA Mwanza nyegezi....
 
Ni aibu kweli. Hata enzi za Nyerere tukiwa 'machokoraa' haikuwahi kufanyika hii.
Mambo yanayofanywa na awamu ya tano in tofauti kabisa nayaliyo wahi kufanywa na awamu nyingine! Hivyo muyazoee. Ni awamu gani walifanya maendeleo makubwa wakitumia hela yao ya ndani? Rais kutosafiri nje ovyo ovyo, nk. Msilinganishe in tofauti na nchi nyingine pia.
 
Back
Top Bottom