Kupitia Corona Serikali za Dunia inabidi zijifunze kwamba afya ndio mtaji wa nchi kujiendesha

Chibudee

JF-Expert Member
Dec 28, 2016
1,775
2,397
Kupitia Corona Serikali za Dunia inabidi zijifunze kwamba AFYA NDIO MTAJI WA NCHI KUJIENDESHA;

Ndio, yaani inabidi huduma za afya zitolewe bure na zigaramiwe na serikali.

Serikali za dunia mpaka sasa zimeshuhudia hasara kubwa sana kutokana na janga la CORONA, kwamba watawaliwa hawafanyi kazi, mfano shule zimefungwa na mikusanyiko ya hela hakuna n.k

Hii inamaana kwamba HAKUNA UZALISHAJI HUKU SERIKALI ZIKITEGEMEA KODI.

Sasa serikali zinaingia gharama za kununua madawa kwa bajeti isiyopangwa.

Maana yangu ni kwamba Serikali za dunia kama zitagaramia huduma zote za afya haswa matibabu ya KANSA, FIGO, UPASUAJI MBALI MBALI na magonjwa yote MAKUBWA KAMA MOYO, maana yake ingetengeneza mtaji afya wa walipa kodi wengi ambao wasingepoteza muda wao kuhangaika na matibabu badala yake wanapona wanaingia mtaani.


Mfano niliwahi kuisikia taasisi 1 ya moyo inasema 'KUTIBU MOYO HUANZIA MILIONI 15- 30'

Rafiki yangu mmoja alienda India akatibiwa figo kwa milioni 36 jumlisha nauli n.k

SERIKALI ZA DUNIA HASWA ZA AFRIKA ZITOE MATIBABU BURE KWA WANANCHI WAKE, NCHI KAMA TANZANIA INAWEZA KABISA KWA KUTUMIA RASILIMALI WALIZO NAZO.

(kuna wakati nikitumia sanitaza huwa naandika point)

FB_IMG_1584115686747.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumewekeza nguvu kubwa sana ya pesa na miundombinu kusomesha watu wetu. Tumetoa mamia ya "wanasayansi".

Mpaka muda huu sijasikia angalau mwanasayansi mmoja kutoka Tanzania akitupatia japo matumaini ya jitihada zao katika kutafuta kinga dhidi ya corona.

Wote wako kimya. Tunamsubiri mzungu.

Tanzania haijulikani mwanasayansi nani wala ngumbaru nani. Ni kama wote hatukwenda shule.

Wakemia wote hoi. Hakuna hata jitihada za kuchanganya madawa huko maabara wapate chochote cha kututia matumaini.

Hivi huwa wanashughulika na nini haswa hawa wanasayansi wetu!

Kwanza, hivi Tanzania tuna "wanasayansi" (just to begin with)?

Wana shughuli gani haswa hawa "wanasayansi" wa hii nchi?

Hata kufurukuta furukuta tu hakuna angalau tujue wanafanya kitu cha kututia moyo?

Wameshindwa japo tu kutambua kwamba klorokwini ina uwezo wa kufubaza corona?!
 
Huu ugonjwa umeporwa na wanasiasa,wanasayansi wametuliza Mpira chini.
Mrisho Gambo yupo anazunguka mitaani na msafara wa waandishi wa habari na ambulansi kutafuta wenye corona.
 
Hamana kitu, wote wakina ummi waziri wa afya, hamna kitu pale, ni sogezasogeza tuu, siku ziende!
 
Mara kumi wanasayansi kutoka vyuo mbali mbali Uganda wamejidhihirishia kwa kuchunguza popo 50+ kwamba virus vya corona vinapatikana kwenye nyama yao
 
Kwa mfano, watu wa nje wakigoma kutuuzia madawa au tukawekewa vikwazo kupata madawa na tiba dhidi ya magonjwa mbalimbali ya mlipuko au yakawaida, inamaana ndio tunakufa wote Tanzania, au manabii na waganga wakienyeji watapewa vibari vya kusimamia mambo ya afya.

mbona hamna ubunifu, miaka nenda rudi, wizara na vitengo vyake, tunakuwa tegemezi kwa nchi zilizo endelea, mnasema mnafanya research! za nini sasa?

Tangu uhuru, hakuna hata official madawa tumegundua, mfumo mbovu wa elimu na afya mko kisiasa zaidi.

Tutakuja letewa kirusi kingine kikali zaidi ya corona, alafu wakatunyima madawa au tukubali kufuata haki za binadamu wanazo zijua wao manake ukiwa tegemezi kubari kupangiwa masharti.

ni hayo tuu.
 
goldcall,
Tofauti na malalamiko, we we ushabuni nini?. Hakuna nchi inayojitosheleza wala kujitegemea kwa kila kitu, hata Marekani na China pamoja na maendeleo yao, bado ni tegemezi kwa nchi zingine katika baadhi ya mambo.

Ndomaana Marekani pamoja na ubabe wake, hutafuta suruhu kwa Korea, Iran, China na Urusi.
Umeshakuwa MTU mzima sasa, acha malalamiko, saidia nchi yako, Mjenga nchi ni Mwananchi
 
Tofauti na malalamiko, we we ushabuni nini?. Hakuna nchi inayojitosheleza wala kujitegemea kwa kila kitu, hata Marekani na China pamoja na maendeleo yao, bado ni tegemezi kwa nchi zingine katika baadhi ya mambo.
Ndomaana Marekani pamoja na ubabe wake, hutafuta suruhu kwa Korea, Iran, China na Urusi.
Umeshakuwa MTU mzima sasa, acha malalamiko, saidia nchi yako, Mjenga nchi ni Mwananchi
Tuache siasa, sisi bado sana.
Mtoa mada ndicho kamaanisha.
Japo tunazidi kuwa bora zaidi ya tulivokuwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wataalamu tupo tatizo ni selekali kutokutenga budget kwa ajili ya research lab ya dawa na magonjwa,
Kwa mfano mim nimesoma jinsi ya kutengebeza chanjo kwa kutumia purified virus rakin hakuna sehemu ya kuiapplay

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasayansi bongo?

Wapo kutishiana vyeti tu na kusubiri wenye akili wabuni wao waje kukosoa.

Nimegundua kukosoa ndiyo Kazi rahisi kuliko zote.Mfano ukiwa mtazamaji wa mpira, unakuwa unaujua kuliko wachezaji.
Mtu akigundua kitu,swali lao la kwanza,ana alimu gani!,kama huna hizo shada zao ndo basi tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni wakati sasa serikali kujitathimini kwenye sekta ya afya, ni desturi watu wakubwa wakiwemo viongozi wa serikali na wale matajiri wanapo umwa kukimbilia kutibiwa nje, but now kutokana na janga la Covid-19 nchi karibia zote duniani zimefunga mipaka yao kama ni kutibina kila mtu apambane na hali yake nchini kwake.

Laiti kama ugonjwa huu utakua seriouz hapa africa kama kwa wenzetu huko Ulaya, basi tutegemee wote mwenye nacho na asiekua nacho kurundikana hapa hapa nchini kwenye hospitali zetu hizihizi ambazo watu tajwa wamekua wakiziona hazijakidhi viwango.

Hivyo basi ni wakati muafaka wa kuamuka usingizini na kuacha kutekeleza yale yasiokua na umuhimu kwa taifa bali nguvu sasa zielekezwe kwenye sektor ya afya. Maana haitoshi tu kutusomea takwimu za idadi ya vituo vya afya na zahanati zilizojengwa kwa kipindi cha miaka 4 bali pia serikali sasa ihakikishe vifaa tiba vinapatikana kwa wingi, wahudumu wa kutosha wanaajiriwa.

Ni aibu mpaka sasa eti sample za vimelea hivi mpaka vipelekwe kwenye hospitali ya taifa pekee kuthibitishwa,hiyo inaonyesha wazi kua hosipitali za rufaa za mikoa mingine hazina aidha uwezo wa kutosha, zina vifaa haba, watalaam haba n.k kukabiliana na magonjwa ya mlipuko japokua ni gonjwa linaloihangaisha dunia kwa sasa.
 
Back
Top Bottom