Kupita bila kupingwa - is this democracy too?

Ndugu zangu wana JF, naomba kuelemishwa ni nin hatima ya mbunge anayepita bila kupingwa hapa nchini. Nafahamu kuwa, kila chama kina mchakato wake wa kuteua mgombea wa ubunge wa jimbo, hii ikiwa ni pamoja na kuitisha kura za maoni, na baadaye kuchakachua matokeo na kumpitisha aliyeshinda au yule ambaye chama kiinampenda (si lazima awe mshindi). Sasa, pale inapotokea huyo mshindi wa chama kimoja anakuwa ndiye mgombea pekee, baada ya vyama vingine kupata mgombea au wagombea waliojitokeza na kupita kuamua kujitoa kwa njia yoyote ile, au wagombea kuwekewa pingamizi na kutolewa; ni nini hatima ya huyu mtarajiwa aliyepita bila kupingwa na hivyo hakuna uhakika kama anapendwa jimboni mwake:
(1) JAnaweza kuteuliwa kuwa waziri?
(2) Anaweza kuteuliwa kuwa waziri mkuu?
(3) Je anaweza kugombea Uspika?

Naomba nisilaumiwe, bali nielimishwe!! Huwezi jua, inawezekana tuko wengi tu tusioelewa suala hilli!! Nawasilisha.
soma hapa kwa kirefu
https://www.jamiiforums.com/uchaguz...-mwenyekiti-wa-tume-ya-taifa-ya-uchaguzi.html
 
Ma mdogo Shikamoo.

Umepeza sana kama mama Salma vile.

Kurudi kwenye mada.

Nadhani vyama kutoweka wagombea au wagombea kuamua kujitoa kabla ya uchaguzi hakumyimi mshindi nafasi ya kuteuliwa uwaziri, au kugombea uspika.

Na vilevile wao ambao hawana wapinzani wanahitaji kupata kura kiasi fulani, hapa wajuzi watatujuza.

Msalimie ba'mdogo.
 
Mie naona kama mgombea yuko peke yake jimboni ni vizuri akachaguliwa kwa asilimia fulani hapo jimboni.Sidhani kama watu wote wana mkubali na hapo ndio umuhimu wa wagombea binafsi inapoonekana.

Ccm wametunyima haki ya mgombea binafsi kwa manufaa yao.kama tungekuwa na wagombea binafsi sidhani kama jimbo lolote nchini lingekuwa na mgombea mmoja kupita bila kupingwa.


Mabadiriko makubwa yanahitajika nchi hii hiweze kusonga mbele,na sioni hayo kutokea kama tutaendelea kuongozwa na ccm.
 
Mbunge anayepita bila kupingwa - mmmmmmmmmmmmmm

Nadhani si halali hatimaye kumwita huyu mbunge wa kuchaguliwa. Yeye kapitishwa na chama chake tu. Hakuchaguliwa na watu. Ni vigumu hata kuelewa kwamba atawakilisha watu wa jimbo husika kwani hawakumpigia kura. Ni mbunge atakayewakilisha chama chake kilichomteua - sio wanajimbo. Naamini kuna kasoro kuwa na wabunge wa namna hii.
 
Sasa sijui kama Masha, Malima na yule wa Mafia wanasikitika kurudishwa kugombea au wanafurahia; maana ile ya "kupita bila kupingwa" ilikuwa inakuja na ujiko wa aina fulani hivi.
 
Mbunge anayepita bila kupingwa - mmmmmmmmmmmmmm

Nadhani si halali hatimaye kumwita huyu mbunge wa kuchaguliwa. Yeye kapitishwa na chama chake tu. Hakuchaguliwa na watu. Ni vigumu hata kuelewa kwamba atawakilisha watu wa jimbo husika kwani hawakumpigia kura. Ni mbunge atakayewakilisha chama chake kilichomteua - sio wanajimbo. Naamini kuna kasoro kuwa na wabunge wa namna hii.

labda sikuelewa kidogo...kama amepita bila kupingwa si inamaana na upinzani hawakumsimamisha mtu? si amekubalika na watu au..(even though si wote)
 
http://www.tz.undp.org/ESP/docs/Legal_Documents/Tanzania_Elections_Act 1985_(dated 30 June 2005).PDF

PART III FINAL NOMINATION OF CANDIDATES FOR PARLIAMENTARY ELECTIONS


44. Unopposed Candidates Act No. 6 of 1992 s 19 Act No. 8 of 1995 s 6.

Where only one candidate is nominated for an election in a constituency such candidate shall be deemed to be elected and the commission shall, by notice in the Gazette declare him to have been elected.

I am sorry, first off, achana mbali na mantiki ya sheria, kwanza Kiingereza chenyewe kibovu, halafu kimejaa mfumodume.

Ukinipeleka kwenye mantiki ya kimsingi, sheria hii inapokonya demokrasia kutoka kwa wananchi na inanuka siasa za chama kimoja. Inawezekana kabisa mtu ambaye wananchi hawampendi akafanya njama na kununua wapinzani wake wote akijua kwamba akiweza kuwa "mgombea pekee" wananchi watakuwa hawana njia ya kumkataa, na itabidi awe mbunge wao watake wasitake.

Sheria hii inatoa mwanya kwa ubunge kununuliwa na watu kuingia bungeni bila kuteuliwa na rais wala kupigiwa kura na wananchi. Hili ni jambo baya sana kwa demokrasia.

Tunataka kuona wabunge hawa wanaopita bila kupingwa wanapigiwa kura na wananchi, hata kama ni kura za "NDIYO" au "HAPANA". Hata tukijua tu wamepata "NDIYO" asilimia ngapi tutajua kukubalika kwao.

Narudia, mbona Nyerere na Mwinyi tumewapigia kura za "NDIYO" na "HAPANA" ingawa wao nao walikuwa wagombea pekee/ Hawa wabunge wana ujiko gani zaidi ya Nyerere na Mwinyi ?
 
Mzee Mwanakijiji,
Duh! nilikuwa sijakusoma mkuu wangu - Hii kitu kimekaa safi sana, nimekukubali mkuu.....
 
Kaka MMM, asante kwa barua yako iliyojaa taarifa zilizonipa ufahamu mkubwa kuhusu wale wagombea wanaosemekana wamepita bila "kupingwa". Asante Nd Macho Mdiliko kwa kunielekeza kwenye link hii ili nipate hii taarifa. Naamini JF ni kisima cha elimu na hekima. Asanteni
 
"deem to be elected" is not the same as "being elected". Neno "deem" lina maana kadhaa miongoni mwazo ni "to form or have an opinion; judge; think" na vile vile "to hold as an opinion; think; regard". Tunaambiwa maneno mbadala yake ni pamoja na "consider, hold, believe.". Kwa kiswahili neno zuri ni "kuchukulia" kwa maana ya kwamba atakuwa "atachukuliwa kuwa amechaguliwa". Lakini cha kuudhi zaidi ni kuwa kutoka kwenye ku"deem" tunaambiwa ati baada ya kutangazwa basi atakuwa "have been elected". Now.. je ibara ya 66 inatiiwa?
 
Mwanakijiji,

Until I actually read the law I thought this was either a mere precautionary measure or a case of misinterpretation on your part.

Then I went and read the 2005 law from the above given link, and it hit me with a BANG!

I am still hoping against hope that someone can correct us all with a more sensible update to this imbecilic law. Why isn't the press drumming this injustice up ?
 
Mwanakijiji,

Until I actually read the law I thought this was either a mere precautionary measure or a case of misinterpretation on your part.

Then I went and read the 2005 law from the above given link, and it hit me with a BANG!

I am still hoping against hope that someone can correct us all with a more sensible update to this imbecilic law. Why isn't the press drumming this injustice up ?

Kiranga.. wengi wetu tumekuwa tukikubali status quo bila hata ya kuhoji mantiki yake au hata kujaribu kufikiria kama kungeweza kuwa na njia bora zaidi. Utaona kuwa mabadiliko hayo ni ya 1995 kwa sababu sheria ya uchaguzi ya 1985 haikuwa na upuuzi (ashakum si matusi) huo. Kwa chaguzi tatu zilizopita tumekubali tu bila kuhoji kwa sababu somehow kuna watu walikuwa wananufaika sasa nani akate mkono utakaomlisha? Nadhani baada ya kuona miaka mitano iliyopita ilivyokuwa wengi tumeanza kuona kuwa the stakes are extremely high this time..

So.. jibu ambalo nimelipata kutoka kwa baadhi ya watu ni nukuu hiyo ya sheria kuwa sheria ndiyo hivyo ilivyo kwamba hao jamaa watakuwa "deem to be elected"! without even a single vote! sasa msingi wa huku kudeem ni nini? kwamba kwa vile alikosa mpinzani hivyo amechaguliwa?
 
Sasa angalia wanavyojivuruga wenyewe kwenye ibara ya 34 ya hiyo sheria na utajiuliza kwanini wasitumie mtindo huo huo?
 
Mzee Mwanakijiji, asante kwa hili. Hii ni hoja ya nguvu iliyobeba nguvu ya hoja ambayo kisheria, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, haina mahali pa kuipangulia.
Ila kila sheria huwa inatungiwa regulations za utekelezaji wa sheria husika, sijabahatika kuziona regulations za mwaka huu, ila kwa mwaka 2005, kwenye regulations, zilimpa mamlaka msimamizi wa uchaguzi (RO) kumtangaza mgombea aliyepita bila kupingwa kuwa tayari ni mbunge/diwani mtarajiwa. Kitu ambacho bado sijakijua, hiyo regulation ili derive wapi mamlaka hayo ya kiimla!.

Regulation hiyo ilisema iwapo hakuna upinzani kwenye nafasi ya urais, mgombea aliyejitokeza, atapigiwa kura za ndiyo au hapana, kama enzi ya chama kimoja, kuweka sura na kivuli., sijui kwa nini utaratibu huu, usitumike, kwa hao wanaodaiwa kupita bila kupingwa.

Kwa kawaida kabla ya uchaguzi, document ya regulations ndio hutoka kwanza, na vyama vyote lazima visaini hizo rules of the game,ndipo kipenga kipulizwe, kwa vile kipenga kimeshapulizwa, na wakuu wa vyama vyote wameshasaini kanuni za mchezo, nadhani, there is nothing that can be done to rectify this serious anomality ili ni hoja muhimu ya kuishikia bango, katika madai ya tume huru ya uchaguzi.

Asante tena.

Pasco.

Mzee Mwanakijiji, asante sana kwa kuliona hili kwanza. Hili ni bomu jingine kwa NEC. Lakini hapo kwenye nyekundu, pamoja na kwamba vyama vilisaini regulation, haki ya msingi ya watanzania ilichakachuliwa. Vyama si wapiga kura na wala wanaogombea uongozi si wawakilishi wa vyama vyao tu ni wawakilishi wa wananchi wote ambao ndiyo wapiga kura. kuna wapiga kura ambao ni wanachama wa vyama mbalimbali na wengine ambao siyo wanachama wa chama chochote. Kama matakwa wanachama wa vyama yaliwakilishwa na viongozi wao mbona hawa wasio wanachama wananyang'anywa haki yao?! MGOMBEA ASIYE NA MPINZANI BADO ANATAKIWA APIGIWE KURA ZA NDIYO AU HAPANA ILI IJILIKANE KAMA ANAKUBALIKA NA WAWAKILISHWA (WANANCHI), kwa sababu atawakilisha wananchi wote siyo chama chake tu. Tofauti na hivyo yatatokea mabo kama ya Musoma vijijini ya wagombea wengine kununuliwa na mafisadi ili wajitoe au wasirudishe fomu kukimbilia kusikojulikana.
 
Ndilo la msingi "even though si wote"

Mgombea wa jinsi hii angebidi kuhalalishwa au kukataliwa kwa kupigiwa kura za ndio au hapana. Hapo kweli akipita atakuwa anawakilisha wanajimbo.
 
Ndugu zangu wana JF, naomba kuelemishwa ni nin hatima ya mbunge anayepita bila kupingwa hapa nchini. Nafahamu kuwa, kila chama kina mchakato wake wa kuteua mgombea wa ubunge wa jimbo, hii ikiwa ni pamoja na kuitisha kura za maoni, na baadaye kuchakachua matokeo na kumpitisha aliyeshinda au yule ambaye chama kiinampenda (si lazima awe mshindi). Sasa, pale inapotokea huyo mshindi wa chama kimoja anakuwa ndiye mgombea pekee, baada ya vyama vingine kupata mgombea au wagombea waliojitokeza na kupita kuamua kujitoa kwa njia yoyote ile, au wagombea kuwekewa pingamizi na kutolewa; ni nini hatima ya huyu mtarajiwa aliyepita bila kupingwa na hivyo hakuna uhakika kama anapendwa jimboni mwake:
(1) JAnaweza kuteuliwa kuwa waziri?
(2) Anaweza kuteuliwa kuwa waziri mkuu?
(3) Je anaweza kugombea Uspika?
Naomba nisilaumiwe, bali nielimishwe!! Huwezi jua, inawezekana tuko wengi tu tusioelewa suala hilli!! Nawasilisha.
Katiba ya Tanzania ya 1977 ipo wazi kwamba mbunge ni wa kuchaguliwa na hakuna mbunge wa kupita bila kupingwa.
 
Wakuu, nimesoma makala ya Mwanakijiji katika gazeti la MwanaHalisi toleo Na 204 yenye kichwa cha habari "Wabunge waliobebwa ni batili"

Makala hii pengine imeibua mjadala miongo mwa wasomaji wengi wa gazeti hili. Nami kama wasomaji wengine (wa gazeti hili) nilipata fulsa ya kulisoma, kutafakari na kujiuliza na hata kushilikisha wengine!

Swali ni kwamba je, kama nafasi ya Urais itakuwa na mgombea mmoja, aliyepitishwa na chama chake kihalali iwe ni chama kinachotetea nafasi yake (kama ingekuwa ni katika soka tungekiita Mabingwa watetezi) au chama cha upinzani na chama kilichounda serikali ya mhula unaopita, atapita bila kupingwa kwa maana ya kutokuwa na ballots papers za nafasi ya rais?

Je, wananchi watapewa nafasi ya kupiga kura ya ndio au hapana kama ilivyokuwa kwa Mwl JK na Mzee Ruksa? Ili kukidhi matakwa ya katiba ya kupata viongozi kwa njia ya kupigiwa kura au kuteuliwa.

Source. MwanaHalisi
 
Hongera sana MKJJ kwa hili nilikuwa sijaisoma barua yako lakini ime hit kwenye point yenyewe, bila shaka Mwenyekiti wa Tume ameshaisoma na natumaini atayazingatia yote. Nakumbuka jana nilimsikia Kinana akisema kuna marekebisho fulani yamefanywa na NEC ya kuruhusu kujazwa kwa wagombea ambao wataondolewa kwa pingamizi kitu ambacho ni kipya kwa sheria zetu labda ndio mwendelezo wa kukubaliana na barua yako.
 
Huko nyuma enzi za mfumo wa chama kimoja tulipata uzoefu wa kumpigia Raisi kura ya "Ndiyo" au "Hapana" ingawaje mgombea hakuwa na ushindani wo wote.

Hivi sasa mawaziri na wabunge wa CCM werevu wamegundua njia ya kuwapiga chenga ya mwili wapigakura kwa kuwawekea mapingamizi wapinzani wao au kuwanunua wajitoe au kuwashinikiza wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo yao yaani wakurugenzi wa Halmashauri au Manispaa kuwang'oa wapinzani wao.

Baada ya kufanikisha mustakabali huo, wapigakura hunyang'anywa haki yao ya kimsingi na ya kikatiba ya kuchagua viongozi wao wanaowataka wawaongoze na huu ni ukiukwaji wa katiba ya nchi ambayo imetamka bayana ya kuwa wagombea nafasi zote kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi. Sasa inapotokea wananchi wanazuiwa kupiga kura kwa sababu za kiufundi tu huo ni kuwanyima wapigakura haki yao ya kimsingi ya kupigakura.

Hii yaamanisha ya kuwa hata akiwa mgombea mmoja bado NEC walipaswa kuhakikisha anapigiwa kura ya "Ndiyo" au "Hapana".

Kama atashindwa kuvuka asilimia hamsini basi uchaguzi huo urudiwe kwa sababu alikuwa yuko pekee yake.

Kwa kutofanya hivyo, NEC inaendesha uchaguzi kibabe kwa kuzingatia masilahi ya CCM na wala siyo vinginevyo.................
 
Kitendo cha masha kuangushwa kimeonyesha kuwa kun ahaina mpya ya upokaji demokrasia hapa nchini.
katiba inabidi iangaliwe upya ktk kipengele hiki na cha mgombea binafsi. kama Masha alipita bila kupingwa sasa huko wapi? Tujifunze kuwa kuna watu wamekabidhiwa ofisi na kuzifanya zao wakati ni za Umma.
hguwezi kuzuia nguvu ya umma ewe mtawala dhalimu
 
Back
Top Bottom