Kupita bila kupingwa - is this democracy too?

Mkjj,

Unaona vipi kama miongozo ya uchaguzi ibadilishwe kidogo kuhusiana na hili hili swala... Ya kwamba, pale ambapo vyama vingine vinaposhindwa kusimamisha mgombea mwenza, basi chama ambacho kimepata mgombea pekee katika jimbo husika kiruhusu mgombea aliyekuwa wa pili katika kura za maoni za kupitisha wagombea wa chama hicho aruhusiwe kugombea ubunge kama mpinzani aliyepita kwa kura zaidi (au baada ya kuteuliwa), japokuwa ni ndani ya chama kile kile.

Steve Dii
 
hilo nalo ni wazo zuri.. unajua tunaweza kuwka mechanisms zozote tunazoona zinafa alimradi wabunge hao wachaguliwe na wasipitishwe bila ya kuchaguliwa.
 
Ahsante Mzee Mwanakijji. Hapa sasa ndipo anatakiwa mtu kama Mtikilla, kufungua kesi mahakamani, hawa watu wasiingie bungeni mpaka wachaguliwe, huku kwetu watu wamechukia sana huyu mbunge wetu ambaye kwa njama tu ametangazwa kupita bila kupingwa na matokeo yake mabango ya Chagua Kikwete yamechanwa chanwa, na hii inaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Mtikila! Mbuzi wa shughuli? Inanikumbusha jeshini kuna wale askari wa "rack" ambao hutangulizwa kama chambo. Mtikila wa watu atazeekea mahakamani bila kuacha mrithi.

On a serious note though, MMKJJ asante kwa ufafanuzi, changamoto na elimu kubwa uliyoweka hapa kwa manufaa ya wengi wakiwemo watendaji kwenye vyombo husika.

Mara nyingi mambo yanapita hata kama hayako sawa kwa vile watz hatuna kawaida ya kuhoji.Hatuhoji kwa vile hatujui, hatujui kwa vile hatujishughulishi kujua, hatujishughulishi kujua kwa vile tu wavivu kufikiri, tu wavivu kufikiri kwa sababu............... hebu nivute pumzi kidogo ndio niendelee.
 
Mwanakijiji sikuoni tena ktk Mwanahalisi siku hizi.
Nashauri barua hii uiweke as makala pia ktk toleo lijalo la mwanahalisi shekhe wangu.
Imetulia na ina hoja
 
Jamani tusiwasahau pia Hawa wenzetu waliochangia huu uchaguzi wetu. Cha ajabu ni kwamba haya mambo kwao hayawezi kukubariwa ila hapa wanakuja kutoa pesa ili haya mambo ya kiuni yafanyike. Hawa donor njisi wanavyojikomba kwa serikali uwezi amini ndiyo unarudi kwenye msemo ule ule kuwa misaada yao si kwa ajiri ya kutuletea mae deleo bali nikwa ajiri ya malengo yao fulani. wachangiaji wa uchaguzi wetu ni wafuatawo
1) UK 9M USD
2) SWEEDEN 5.2M USD
3) EC 3.9M USD
4) FINLAND 1.9M USD
5) NETHERLAND 1.3M USD
6) NORWAY 1.M USD
7) SWITZERLAND 1. M USD
8) UNDP 1M USD
9) GOT ZA KUZUGIA SIJUI KAMA KWELI WANATOA

Tena kwa khali ilivyo kuwa tete kwa wahisani nyumbani kwao kwa sasa sizani kama watapenda raia wao wajue kuwa fedha zao zinatumika kuminya demokrasia kiasi hiki hii barua ya mwanakijiji itapokelewa kwa mikono miwili na magazeti kwa mafano ya uingeleza kama, http://www.telegraph.co.uk ambayo yamekuwa yakifuatilia matumizi ya fedha za uingereza kwa karibu
 
Mwanakijiji,

Action point ya hii mada ni nini mkuu?

wananchi wa Nyamagana, Bumbuli na majimbo mengine ambako kuna watu "wamepita bila kupingwa" waweke pingamizi kwamba wanaoenda Bungeni hawakuchaguliwa na wananchi.
 
Say word?

Unataka kuniambia candidates "waliopita bila kupingwa" hawapigiwi kura?

Hata Ally Mwinyi na Nyerere tuliwapigia kura za "NDIYO" au "HAPANA".
 
Say word?

Unataka kuniambia candidates "waliopita bila kupingwa" hawapigiwi kura?

Hata Ally Mwinyi na Nyerere tuliwapigia kura za "NDIYO" au "HAPANA".

That is how it is buddy! Hukuona jinsi walivyokuwa na furaha?
 
mzee.. si ndo maana wanaitwa "wamepita bila kupingwa"? LOL

Wamepita bila kupingwa huko kwenye party politics, hawajapita bila kupingwa kwa wananchi, ni lazima wapigiwe kura.

Hata kama mgombea ni mmoja tu watu wapate nafasi hata ya kupiga kura ya "NDIYO" au "HAPANA". Ama sivyo tutaanza kuona electioneering mpya ambapo wagombea wananunuliwa, wagombea wengine "wanapita bila kupingwa" na wananchi wanaachwa solemba.

Siamini kwamba wagombea "waliopita bila kupingwa" wataingia bungeni kama wabunge bila kupigiwa kura na wananchi, where do you get this idea Mwanakijiji ? This is a genuine question, not a rhetoric one, I would like to know where this nonsense is steming from.

Au unatoa a precautionary note in the style of "tahadhari kabla ya hatari" ?
 
well.. wameshapita bila kupingwa wanasubiri kuapishwa tu. Hiyo ndiyo sheria yetu. Madiwani na Wabunge.. sijui kwa rais ikoje kwani kwa rais inaonesha bado rais atapigiwa kura.
 
Nakupongeza sana Mzee MwanaKijiji,
Wewe ni mtu muhimu sana katika kuwafungua watanzania macho.Hatuna wanasheria wasomi hapa Tanzania wanaoweza kutafsiri Sheria zetu na kama wapo basi wanaogopa kwa sababu wako serekalini.Huu ndo ukweli.
Thanks again Mzee.
 
well.. wameshapita bila kupingwa wanasubiri kuapishwa tu. Hiyo ndiyo sheria yetu. Madiwani na Wabunge.. sijui kwa rais ikoje kwani kwa rais inaonesha bado rais atapigiwa kura.

Honestly sikuwa na wazo kuwa Masha, J.Makamba na wengineo wa staili ya "kupita bila kupingwa" wanasubiri kuapishwa!!! Was this the same in 2005? Wakuu tukumbushane...
 
Habari ndivyo ilivyo; ati sheria inasema kuwa atakayekosa mpinzani kwenye ubunge au udiwani "atakuwa" amechaguliwa.. (Will seem to have been elected)... najaribu kuyatafuta hayo mabadiliko ya sheria..ya 1985
 
Ndugu zangu wana JF, naomba kuelemishwa ni nin hatima ya mbunge anayepita bila kupingwa hapa nchini.

Nafahamu kuwa, kila chama kina mchakato wake wa kuteua mgombea wa ubunge wa jimbo, hii ikiwa ni pamoja na kuitisha kura za maoni, na baadaye kuchakachua matokeo na kumpitisha aliyeshinda au yule ambaye chama kiinampenda (si lazima awe mshindi).

Sasa, pale inapotokea huyo mshindi wa chama kimoja anakuwa ndiye mgombea pekee, baada ya vyama vingine kupata mgombea au wagombea waliojitokeza na kupita kuamua kujitoa kwa njia yoyote ile, au wagombea kuwekewa pingamizi na kutolewa; ni nini hatima ya huyu mtarajiwa aliyepita bila kupingwa na hivyo hakuna uhakika kama anapendwa jimboni mwake:
(1) Anaweza kuteuliwa kuwa waziri?
(2) Anaweza kuteuliwa kuwa waziri mkuu?
(3) Je anaweza kugombea Uspika?

Naomba nisilaumiwe, bali nielimishwe!! Huwezi jua, inawezekana tuko wengi tu tusioelewa suala hilli!! Nawasilisha.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom