Kupishana kauli: Tumuamini kamanda Sirro au Mkurugenzi wa elimu ya mlipa kodi TRA?

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,491
2,355
Katika tukio la wizi ukiotokea usiku wa kuamkia jana katika ofisi za TRA kumetoke kupishana kauli hali ambayo inatia mashaka kuhusu ukweli wa tukio lenyewe, ni kama vile kuna jambo linataka kufunikwa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema tayari jeshi hilo linawashikilia watu wanne kwa uchunguzi zaidi.
Sirro alitaja vitu vilivyoibwa katika ofisi hiyo kuwa ni kompyuta mbili, televisheni moja na king’amuzi.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA, Richard Kayombo alikanusha kutokea kwa wizi huo akisisitiza kwamba lilikuwa ni jaribio la wezi kutaka kuvunja ofisi hiyo.
Kayombo alisema hakuna wizi wowote uliotokea katika jaribio hilo kwa sababu hawakufanikiwa kuingia ndani. Alisema mali zote ziko salama na suala hilo tayari tukio hilo limeripotiwa polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Katika maelezo haya, tumuamini nani?
 
Back
Top Bottom