Kupingwa kwa hoja ya Magufuli, kulizingatia faida za kisiasa au manufaa kwa wananchi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupingwa kwa hoja ya Magufuli, kulizingatia faida za kisiasa au manufaa kwa wananchi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by analysti, Jul 16, 2010.

 1. analysti

  analysti JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 704
  Likes Received: 354
  Trophy Points: 80
  Mheshimiwa J.P.Magufuli, akisoma bajeti ya wizara ya Mifugo na Uvuvi 2010/2011, alitoa hoja ya kuundwa chombo kitakacho dhibiti idadi cha mifugo ambayo mfugaji anaweza kumiliki.

  Waheshimiwa wabunge, hasa wale wanaotoka kwenye jamii za wafugaji, waliipinga hoja hii kwa nguvu zao zote, na kuhakikisha kuwa inaondolewa.

  Swali ni Je!? kupingwa kwa hoja hii, kulizingatia maslahi ya kisiasa au maslahi ya wananchi na ustawi wa jamii kwa ujumla?

  Hoja hii ingepita ingewanufaisha vipi jamii ya wafugaji, au ingewaathiri vipi?
   
 2. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nadhani imepingwa kwa manufaa ya wabunge na si ya wananchi. Mimi ninatoka katika jamii za wafugaji, kusema kweli ufugaji holela umesababisha uhalibifu wa mazingira na umasikini mkubwa sana kwa jamii hizi.
  Kama kungelikuwa na chombo cha kisheria cha namna hii kingeweza kuweka kiwango cha mifugo kwa kila eneo kulingana na upatikanaji wa malisho na ardhi katika eneo husika na kungelikuwa na manufaa sana kwa wananchi hawa. Ungeliwawezesha kuwasomesha watoto wao na kuhakikisha mazingira hayaharibiwi.
   
 3. analysti

  analysti JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 704
  Likes Received: 354
  Trophy Points: 80
  Hilo ndo tatizo la wanasiasa wetu!. Nakumbuka kauli ya Ndg. JK alisema tuondokane na hali ya kuwa na Ng'ombe wenye afya mbona na mwenye ng'ombe ana afya mbovu!, Kwa hiyo hakuna mwenye manufaa kwa mwenzake!!!
  Nafikiri wanasiasa inabidi waliangalie vizuri swala hili!
   
 4. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  wangekubali kwanza ikaundwa ikatoa mapendekezo, hapo ndipo wangekubali au kukataa.
   
 5. M

  MJM JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Mimi naona hili suala kama halijakaa vizuri kwani pendekezo limekuja kwenye budget au mswada? Wabunge wa jamii ya wafugaji lazima watetee maana hiyo ndiyo kauli ya wapiga kura wao (wananchi) na wao ni wawakilishi hivyo hawawezi kuwatosa. Ukiwabana wafugaji wabane pia wavuvi idadi ya samaki wanatakiwa kuvua, wabane wakulima (japo na wafanyakazi na wanasiasa wako humu) idadi ya ekari za kulima, punguza mshahara na malupulupu ya wanasiasa, uza mashangingi yote ya serikali tuanze upya kujipanga.
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Inasikitisha kuona mtu anamiliki ng'ombe 20000 lakini watoto wake hawajui kusoma wala kuandika. Kuhusu hoja ya Dr Magufuli nadhani maslahi ya kisiasa yalizingatiwa zaidi kwani hakuna aliyeonekana kueleza ni jinsi gani wananchi wata athirika kama kutaundwa chombo cha kudhibiti idadi ya mifugo ambayo mfugaji anastahili kuwanayo.
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hiyo mifugo mingi na nomadic lifestyle with little efficacy in terms of nutri-economics should be discouraged, kwanza wanaharibu mazingira pili wanaharibu mazao ya watu na kusambaza magonjwa na pia kuleta migogoro na wakulima. Nchi ambazo leo zinatuuzia maziwa na nyama za kopo mboni hazina huo upuuzi??

  Kwanza majuzikati nimesoma article kwamba within few decades wataalam watakuwa able kutengeza 'nyama' maabara ambayo ni more eco-friendly kwa kuepuka utengezaji wa greenhouse gases. Wenzetu wachina wameshaanza kutengeza 'nyama' kwa kutumia uyoga na mazao mengine.

  The world is changing fast na ni vyema hao wabunge gullible wakaenda kubrush their knowledge na kuondoa vichwa vyao mchangani vipate mwanga wa jua(elimu dunia).
   
 8. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Muswada huo ni mzuri sana.kwani wafugaji hawanufaishwi na mifugo yao, wengi wanaishi maisha ya taabu sana,huishi kwa kuhamahama kama wanyama vile.hawana elimu.matibabu mazuri hakuna.taabu tu.

  Lakini pamoja na uzuri wa muswada huo,mim wasiwasi wangu ni namna ya utekelezaji wake,maana tumeshuhudia ubovu mkubwa ktk utekelezaji wake.
   
 9. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  SISI HUKU TUNALALAMIKA TUNAKULA WATER BULK[BULL] ambaye siye ngombe kumbe Duuu..WAMEFIKA KWINGINE
   
 10. analysti

  analysti JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 704
  Likes Received: 354
  Trophy Points: 80
  Ni bora mfugaji awena ng'ombe 20 watakao pata Tiba nzuri, kula vizuri na wakawa environ friendly, na wakawa na kilo 700 kila mmoja. Kuliko kuwa na ng'ombe 100 wanaorandaranda tu pasipo kushiba, wanaharibu mazingira na hawapati tiba ya kuridhisha hivyo kusambaza magonjwa, na kisha wakawa na kilo 150 kila mmoja.

  Kwa kweli Low stocking density ni very productive na environmentally friendly.
   
Loading...