Kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani:Ukifungua kesi leo hii na mpaka kesi iishe,utakuwa ndani ya muda wa kufanya uchaguzi kisheria?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,887
143,983
Kwa nchi yetu hii,leo hii ukifungua kesi mahakama kuu kupinga matokeo ya ubunge au udiwanu ni wazi kesi hiyo inaweza kuchukua mwaka na hata zaidi ya mwaka kuisha mahakamani.


Wakati huo huo tunajua kuwa kwa mujibu wa Sheria, ikibaki miaka miwili kabla ya Bunge kuvunjwa na kufanyika kwa uchaguzi mkuu unaofuata,ndani ya kipindi hicho ikitokea Jimbo liko wazi kwasababu yoyote ile,kisheria hairuhusiwi kufanya uchaguzi mwingine wowote kujaza nafasi iliyowazi

Sasa najiuliza leo bado kuna muda wa kufungua kesi za uchaguzi na ambazo mkishinda zitatoa fursa ya kufanyika uchaguzi mwingine?

Je,si kweli muda umeisha na hata ukifungua kesi na kushinda haiwezi kukusaidia zaidi tu ya kumvua ubunge mbunge alieshindwa kesi?

Kama hali ndio hii,nani atahangaika kupoteza muda na gharama za kuendesha kesi katika mazingira haya?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom