Kupinduliwa matokeo ya uchaguzi wa Rais huko Kongo, Kabila ajiingiza mtegoni.

KWADWO ABIMBOLA

JF-Expert Member
Jan 8, 2019
762
1,598
Huku dunia ikisubiri kwa tahadhari uamuzi wa mahakama ya kikatiba juu ya ni nani mshindi wa kura za urais huko Kongo, kumeibuka data zilizovujishwa kutoka ndani ya database ya tume ya uchaguzi inayohusisha asilimia 86 ya kura zote zilizopigwa. Data hizi ambazo zimechambuliwa na kuripotiwa na gazeti la financial times zinaonyesha kuwa mgombea Martin Fayulu alishinda uchaguzi wa December 2018 kwa asilimia 59.4 (59.4%), akifuatiwa kwa mbali na Felix Tshisekedi aliyepata asilimia 19 (19%)- Congo voting data reveal huge fraud in poll to replace Kabila. Pamoja na juhudi za Kabila kujaribu kuendesha uchaguzi kwa kuzuia usimamizi wa uchaguzi kwa vyombo kutoka nje, yaonekana wazi kuwa kuna wazalendo waliowezesha kukushanya hizo taarifa sahihi na kuzivujisha.

Taarifa hizi mpya, zinakaribiana sana na zile zilizotolewa na kanisa katoliki zilizokusanywa kwenye vituo zaidi ya elfu 40 zilizoonyesha kuwa Bw. Fayulu alishinda kura za urais kwa zaidi ya asilimia 60. Pamoja na hayo, waratibu wa kampeni ya Bw. Fayulu, wanadai kuweza kukusanya sampuli za matokeo yanayoonyesha ushindi wa zaidi ya asilimia 61. Takwimu hizi, zimeongeza hisia za watu wengi ndani na nje ya Kongo kuwa Kabila aliingia makubaliano ya kushirikiana madaraka na Bw. Tshisekedi, baada ya kudhihirisha kuwa asingeweza kumtangaza mgombea wa chama chake Bw. Shadari aliyeshindwa vibaya mno kwenye uchaguzi huo.

Kutokana na taarifa hizo, dunia imeanza kuimulika Kongo. Jumuiya ya SADC ambayo Kongo ni mwanachama, imeitisha kikao cha dharura kuijadilli huko Addis Ababa, Ethipia - SADC calls for emergency meeting over DRC poll. Pia SADC ambayo kupitia waangalizi wake kwenye huu uchaguzi katika hatua za awali ilitoa maoni kuwa ulienda vizuri na kasoro ndogondogo, imegeuka msimamo wake wa awali na kuitaka tume ya uchaguzi ya Kongo (CENI) ihesabu kura upya African nations call for recount in DRC election. Mataifa yenye ushawishi Kongo, mfano Ubelgiji, Ufaransa na Marekani, wote kuanzia awali waliyatilia shaka matokeo ya uchaguzi, wakisema yalipinduliwa.

Kwa hali ilipofikia sasa, Kabila ataweza kujinasua kwenye mtego alipojiingiza? Haki ya wakongo itaweza kupatikana kwa maamuzi ya watawala kujipangia wao watakavyo kwa kupindua matokeo ya uchaguzi?
Huku Tanzania tutaendelea kuziamini teknolojia zinazoweza kutumika kuvujisha matokeo halisi ya uchaguzi? Kongo wataweza kuvuka kwa mbinu kama za akina Jecha za kuufuta uchaguzi wa Zanzibar wa 2015?
 
Siti ya kwanza kabisa. Hivi haya mambo kwanini hayatokeagi Tanzania?

Sent using Jamii Forums mobile app
Watumishi wa Tanzania siyo risk taker, na ni waoga sana. Hata wakiona uozo unaendelea, wao huwa kimya kama makondoo. Mpaka Somalia tunaowadharau watatupita kwenye demokrasia na ujasiri wa wananchi kusimamia maamuzi yao kwenye kura.
 
Hicho ndicho kingetokea hapa kwetu Kama polisi wasingefanya ugaidi wa kuvamia vituo vya kuhesabia kura vya ukawa na ofisi ya mama Bisimba.
Nadhani kabila alijikwaa hapo kutokutumia mbinu za polisccm.
Ilimbidi avamie kituo Cha kuhesabia Cha kanisa katoliki na kusambaza propaganda kanisa linajihusisha na siasa
Then pia avamie kituo Cha kuhesabia kura Cha vijana wazalendo wa Congo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hicho ndicho kingetokea hapa kwetu Kama polisi wasingefanya ugaidi wa kuvamia vituo vya kuhesabia kura vya ukawa na ofisi ya mama Bisimba.
Nadhani kabila alijikwaa hapo kutokutumia mbinu za polisccm.
Ilimbidi avamie kituo Cha kuhesabia Cha kanisa katoliki na kusambaza propaganda kanisa linajihusisha na siasa
Then pia avamie kituo Cha kuhesabia kura Cha vijana wazalendo wa Congo


Sent using Jamii Forums mobile app
Ni aibu sana. Binadamu akizaliwa Afrika automatically anakuwa na mental problem. Kwanini tunawaza kuvamia vituo ili kuzuia maamuzi ya haki ya wananchi? Kwani ni nani kasema kuwa wananchi hawatakiwi kujua waliyemchagua kwa kupiga kura?
 
Nalisifu Kanisa Katoliki DRC kwa kusimamia kidete haki katika uchaguzi huu wa Kongo. It seems hawabahatishi na wanachokisema.
 
Back
Top Bottom