Kupinduana, kupo sana...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupinduana, kupo sana...!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 26, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 26, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Unapoishi nyumbani na ndugu yako, jamaa yako au hata mtumishi wa kike, ni vizuri ukajitahidi kulinda ndoa yako. Kumbuka kwamba, wanaume hawajali hisia, hujali zaidi mwili. Kama ukimwachia ndugu yako, jamaa au rafiki yako kumzoea sana mumeo, jua tu kwamba, inawezekana unajitengenezea maumivu makubwa sana hapo baadae.

  Tafiti zinathibitisha sana kwamba, mwanaume anapohisi kuwa mwanamke fulani anamwonesha kwamba, yeye ni mwanaume kweli kweli, anapoonesha kwamba, anatambua uwepo wake na mchango wake katika familia, mwanaume huanza kumpenda, bila kujali sura au hadhi.

  Kama ndugu yako ni mjuaji wa mambo haya, anaweza kumwonesha mumeo kwamba, anaamini kuwa ni mwanaume kwelikweli. Hii hufanyika kwa kumsifu, kutopingana naye, kumpongeza mara kwa mara na kumwonesha kwamba anaamini katika yeye.

  Hata wale watumishi wa ndani, wanaochukuliwa na wanaume za watu hawafanyi hivyo kwa sababu, ati hao watumishi ni wazuri sana wa sura au wanajua sana mapenzi, hapana.

  Wanaume huwachukua kwa sababu, wake au wapenzi wa wanaume hao wameshindwa wajibu wao, wameshindwa kujua kwamba wanaume hutazama uhusiano kwa jicho tofauti.

  Lakini, iwe ndugu au jamaa zenu na hata watumishi majumbani mwenu, bado na wao ni binadamu, wana udhaifu. Kwa udhaifu wao, pamoja na udhaifu wa wanaume au wapenzi wenu, wanaweza kuwasaliti. Kwa hiyo ni juu yenu kulinda ndoa zenu, ili udhaifu huo usiwe chanzo kwa kuvunjika kwa matumaini na matarajio yenu ya kujenga familia.

  Kuna mambo mawili makubwa hapa, kwanza inawezwekana mmejiachia wazi sana kama wanawake na kusahau kuwa wanaume huvutiwa na mambo gani.
  Kwa hali hiyo, mnawaacha wale walio karibu nao kuwafanyia yale wanayohitaji na kuchukua nafasi zenu.

  Lakini pili, ni udhaifu wa kibinadamu na zaidi kwa wanaume, linapokuja suala la mwili. Kwa udhaifu huo, inabidi muwasaidie kuwalinda wasishawishiwe kirahisi. Lakini, ndugu zenu wa kike au watumishi mnaoishi nao, inabidi muwakague vizuri na kuacha kuwamini kupita kiasi kwa waume au wapenzi wenu.

  Ni hatari sana kwa mwanamke kwa mfano, kumwambia au kumruhusu mumewe aende sehemu za starehe na rafiki yake wa kike au na ndugu yake wa kike, ati kwa sababu anamwamini rafiki huyo au mumewe. Kumbuka, suala hapa sio kuaminika au kutoaminika, bali ukweli wa kimaumbile pia. Mwanamke, chunga ndoa yako, ilinde sana, kwani sio dhambi.
   
 2. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Kama utakuwa humwamini mme wako kiasi hicho, yeye kwa nini akuamini? Mtaishi kwa kutoaminiana katika ndoa mpaka lini???
   
 3. Amateur

  Amateur Member

  #3
  Aug 26, 2011
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hii thread ni kwa ajili ya wanawake kwa ajili ya kuchunga waume zao? Not the other way around? Au the other way around hakunaga shida? Anyway, just passing!
   
 4. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Bullshit!
  Why is always a woman's responsibility kichunga ndoa? Why not man's, after all nani alimchumbia mwenzie, akabother kujipendekeza, kutoa mahali, kugharamia a very expensive wedding etc! Whose loss will be if ndoa ikivunjika? A man will have to incur the same shit allover again plus taking care of the children!
   
 5. Biohazard

  Biohazard JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 2,002
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  Trust nobody
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,568
  Likes Received: 18,313
  Trophy Points: 280
  Asante kwa hii post, nimeipenda nikaicut na kuipaste ili nimtumie wife, lakini nikasita nisije kumletea problem tx wetu, asante ujumbe umenifikia.
   
 7. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #7
  Aug 27, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Hio paragraph nilo bakisha ndio hua natoa basis kua mwanamke anaweza kabisa mbadilisha mwanaume aelekee ndani ya nyumba (thou not always) for at the end of the day waume zetu wanataka uwaoneshe na wajue una m-appreciate, unajali uwepo wake, unajali mahitaji yake na kwamba wamthamini... End result ni kua anaweza ndio asikupende.... lakini hatasikia neno lolote baya juu yako, au kutoa maamuzi yoyote mabaya juu yako maaana yule mwelewa anajua kabisa kua hio amani anapata hapo sio guranteed toka kwa wanawake wooote...
   
 8. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #8
  Aug 27, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hakuna kitu ambacho wanaume wengi kinawakera kama akiwa anajali na kutekeleza wajibu wake kama mume/bf lakini bado kunakuwa na lack of appreciation! Hapo mwanaume anavunjika sana moyo na inakuwa rahisi sana kuishia kwengine
   
 9. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu naona hapa hii story inafanana sana na ile drama ya governor Arnold Schazneggerkuishia kuwa na affair na kumzalisha yule house maid wake na ndoa kuvunjika
   
 10. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #10
  Aug 27, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Na vice versa Sherrif... hata wanawake tunajisikia hivo pia.. thou tunajikaza in most cases... Sema maamuzi ya mwisho ndio tumetofautiana... mwingine anaachia ngazi mapema.. wengine unashindwa for unaua dhahiri waweza ruka mkojo na ukakanyaga kinyesi.. you try your best... ikishindikana then unasepa... thou it is the worst option ever katika relationships...
   
 11. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #11
  Aug 27, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mapenzi ya dhati yameenda wapi siku hizi? Kama kweli unampenda mwenzio na yeye anakupenda, je ni kwa nini kuwe na lapses kama hizo eti oooh sijui mume katembea na house maid, ama mke kakumbushia old flame?
  Inasikitisha sana morals hakuna kabisa siku hizi hata kwa waliofunga pingu za maisha!
   
 12. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #12
  Aug 27, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  kweli kabisa Adi, mana tukishaona tunathaminiwa basi hata rungu linapunguza fujo, linakua linataka mtu maalum tu na kwa muda maalum.
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Aug 27, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  wanawake wa kizazi mbona mna wakati mgumu? Hata kuilinda ndoa ni jukumu lenu, siku c nyingi nyie ndo mtakua vichwa vya familia!
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Aug 27, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Sherrif, mapenzi ya dhati yapo, tena sana, lakini kuna wakati wanandoa au wapenzi hujisahau na kuwaachia watu wngine majukumu ambayo yalitakiwa yafanywe na wao, na si kwa wanawake tu hata wanaume pia. kunakuwa na kujisahau kwingi na ndio maana ndoa ikivunjika, husemwa kwamba wote mmechangia, ina maana kuna mmoja wa wandoa aliuona udhaifu kwa mwenzie na kuamua kuufumbia macho au kulalamika kwa ndugu, jamaa au marafki zake. hiyo haisaidii, sana sana inachangia kuipeleka ndoa shimoni.
   
 15. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #15
  Aug 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Life is not about finding the right person, but creating the right relationship, it's not how we care in the beginning, but how much we care till the very end.
   
 16. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #16
  Aug 27, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  umejitahidi kumpotray mwanaume ni kiumbe dhaifu,ukweli ni kwamba mwanaume ni mwenye nguvu zaidi na ana uwezo sana wa kucontrol hisia zake....we both men and women have equal rensponsibilities kufanya kila jitihada ndoa zetu zidumu sio jukumu la mwanamke pekee kama unavyotaka kutuaminisha hapa.
   
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  Aug 28, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ann Marie, Siwezi kukubishia kwa sababu huo ndio mtazamo wako.......lakini kama wewe ni msomaji mzuri wa mada za mahusiano zinazowekwa humu utagundua kuwa kuna malalamiko mengi ya wanawake juu ya kusalitiwa kwa ndoa au mahusiano yao. Nimezungumzia hisia kwa sababu hisia za wanawake na za wanaume katika swala zima la mapenzi zinatofautiana. Kama si mila na desturi zetu ambazo zinamsisitiza mwanamke kuwa yeye ndiye anayewajibika kulinda ndoa kwa kiasi kikubwa swala la kukithiri kwa talaka au kutengana lingekuwepo tangu kale. lakini wazazi wetu waliliona swala la talaka kama udhaifu kwa mwanamke na sio kwa mwanaume. muingiliano wa tamaduni umesababisha kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa swala zima la talaka. hiyo ni kutokana na mabadiliko ya kiuchumi. kile tulichokuwa tukiita mke ni mama wa nyumbani hakipo tena, mke ni lazima achangie pato la familia, na ndio maana kuna mahitaji ya kuwa na mfanyakazi wa nyumbani tunaita House Girl au ndugu wa kike ambaye anaweza kuchukuliwa kwa ajili ya kusaidia kazi za nyumbani... Tatizo huja wapi......? Rejea makala yangu ukisoma between line utanielewa.........
   
Loading...