Kupindisha historia ni kujidanganya-ni tanganyika siyo tanzania inatimiza miaka 50 disemba 09 2011!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupindisha historia ni kujidanganya-ni tanganyika siyo tanzania inatimiza miaka 50 disemba 09 2011!!

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Mtu wa Mungu, Dec 8, 2011.

 1. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kujaribu kuwafanya watanzania waamini kwamba Disemba 09, 2011 tunasherehekea miaka 50 tangu kupata uhuru ni kupindisha historia kwa maslahi ya nani????????? Ni nani tunajaribu kumdanganya kama si sisi wenyewe??????????
  Mimi ninayeandika thread hii nilikuwepo usiku wa 09.12.1961 wakati bendera ya mkoloni inashuka na ya Tanganyika kupanda, na tukaimba Mungu ibariki Tanganyika........ .Wanaotaka kupindisha historia wangoje wote tuliokuwepo siku hiyo tuwe tumekufa; hapo itakuwa rahisi kudanganya.
  Tanzania ilizaliwa mwaka 1964. Hivyo Tanzania itatimiza miaka 50 mwaka 2014. Kadhalika Tanzania bara ilizaliwa mwaka 1964, na siyo 1961 kama inavyopigiwa parapanda na hawa wapotosha historia ya nchi hii.
  Pole Tanzania!!!!!!!!! Kweli mvunja nchi ni mwananchi/mwenyenchi!!!!!!!!!!!!!!
   
 2. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Japo ni jina lake halisi hata leo ila ungeonekana wa zamani kama ungesema 'UNION JACK FLAG', Mzee yeyote wa zamani hata asiyekuwa na shule ukimtajia jina hilo anajua kuwa ni nini.
   
 3. Bushloiaz

  Bushloiaz JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Nyie wazee ndio mtusaidie kutuwekea historia vizuri,vijana tukiongea tunaonekana wakorofi,swali linalosumbua wengi kwa nini historia yetu imefanywa hivi???
   
 4. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tatizo ni ninyi vijana mnaowaacha mafisadi kwa kutumia UWT na FFU kuliangamiza taifa hili kwa kulitawala KIHUNI mchana mchana. Vijana wa Kenya walipogundua hili wao walitumia visu kuwachinja raia wasio na hatia. Sijui ninyi vijana wa Tanzania, mnaomwangalia tu mkulu anayelindwa na majini ya the late sheikh akiharibu chama na serikali yake, mtatumia ndumba au nini? Sisi wengine, tuliokuwepo wakati bendera ya mkoloni inashuka, wakati huo tutakuwa hatupo wakati huo; tutakuwa mbinguni!!!!!!!!!!!!!Poleni vijana wa Tz!!!!!!!!!!!
   
Loading...