KUPIMA V.V.U kabla ya harusi ni lazima? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KUPIMA V.V.U kabla ya harusi ni lazima?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by chrispin2008, Jan 7, 2009.

 1. c

  chrispin2008 Member

  #1
  Jan 7, 2009
  Joined: Dec 12, 2008
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani mi nashindwa kufaham, mkitaka kuoana mnaambiwa eti lazima mpime,sasa nauliza je kupima ni hiari au cyo hiari?
   
 2. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kupima v.v.u kabla ya ndoa si lazima,ingawa inategemea na makubaliano yenu.Kama kupima ilikuwa ni sehemu ya makubaliano,hapo hauna jinsi ya kukwepa na hapo ndipo ulizima wenyewe unapoanzia.Na kama yupo anaekulazimisheni mkapime kwanza kabla ya kuoana,basi nina imani huyo mtu anawapenda sana kwani kuna humuhimu wa kujua afya yako kabla ya kuingia katika ndoa.Ila kama mlikuwa mnashake before use,kupima au kuto kupima itakuwa ni juu yenu.
   
 3. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2009
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mkuu,
  Katika suala la ndoa kupima sio hiari. Ila pia kabla ya kupima utapewa ushauri nasaha ili uweze kuwa tayari kupokea na kuyakubali majibu ya vipimo.
  Sidhani kama kuna mtu aliye timamu angependa kumuambukiza mwenzi wake virusi kwa makusudi na ndio maana imekuwa ni kama utaratibu pindi wawili wapendanao wanapotaka kuingia katika ndoa hupimwa ili kujua kama wako salama kuoana au wanahitaji kupewa ushauri wa jinsi ya kuishi pamoja iwapo mmojawapo ameambukizwa. Pamoja na kuepusha kuendelea kuishi gizani pia mtoto atakayezaliwa ni bora awe salama. Kwa hiyo suala la kupima kabla ya ndoa ni vema likabakia kuwa lazima.
   
 4. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Yaani wewe sijui unaishi dunia ipi ikiwa u are serious about your question... kupima sio hiari bali ni lazima, hebu take a simple example wewe chrispin, umejitunza kabisa.. utakubali mtu akuambukize kweli??? kama unajipenda wewe mwenyewe na kumjali mwenzako pamoja na watoto mtakao barikiwa nao.. basi u should not be asking this question.
   
 5. S

  Stephano Member

  #5
  Jan 7, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 27
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  inategemea kaka mi nadhani ni muhimu kupima kabla ya kujaribi au kuonja maana wengi wetu siku hz ndoa huwa ni hatua ya mwisho baada ya kuonjaaaaaaaaa ndo wanaamua kuhalalisha, hivyo muda muhimu na muafaka kupima ni kabla hamjaonja. kama mtaonja baada ya ndoa sawa kama kabla basi iwe kabla pia
   
 6. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,923
  Likes Received: 2,071
  Trophy Points: 280
  Nadhani kinachofanya watu waoane siyo kutokuwa na VVU bali ni upendo walio nao kati yao na nia ya kutaka kuishi pamoja kama mke na mume.

  Kisheria (kwa sasa) hakuna mtu aneyeweza kukulazimisha kupima VVU kabla ya ndoa. Wafungishaji ndoa hawana haki ya kujua HIV status ya wafungaji ndoa isipokuwa kwa ridhaa ya wanandoa wenyewe. Nafahamu kuna baadhi ya makanisa ambayo (kwa makosa) wanalazimisha kupima VVU. Lakini hawajui pia kwamba ndoa nyingi sasa hivi zinafungwa wakati wahusika tayari wana mahusiano ya kimapenzi (in most cases yasiyo salama!) kwa muda mrefu tu.

  Watu wenye VVU wana haki ya kuoa na kuolewa kama mtu mwengine yoyote yule mzima au mwenye kasoro au magonjwa mengine (kansa, kisukari, ukoma,bp etc).

  Hata hivyo mwenza wako (na si mtu mwengine!) anayo haki ya kukutaka 'mkapime' (sio'ukapime'!) VVU kama mojawapo ya masharti kabla ya kuoana. Kama ataamua kutofunga ndoa na wewe kwa sababu una VVU hilo ni suala jingine!
   
  Last edited: Jan 7, 2009
 7. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  Dhana ya Kupima kabla ya Ndoa haina maana kwa kuwa kuna-elemant za kulazimishwa, pili hakuna usiri na kwa kuwa wengi wanakuwa wanasubiri matokeo (wachungaji,wanandugu na marafiki n.k) na hata hivyo haisaidii hata kidogo, kwa kuwa maambukizi mengi hutokea baada ya kuoana, watu wanawavalia bango wachumba wapime kabla ya ndoa na baadhi ya madhehebu imekuwa ni kama sheria, je baada ya kufunga pingu za maisha nani anawavalia kidedea wanadoa kupima? wakati huo huwa ndyo muhimu sana kwa wanandoa kuelewa status yao ya maambukizi na hasa kabla ya kuamua kutengeneza watoto, hivyo kupima iwe ni utashi wa mtu mwenyewe kabla na baada ya kufunga ndoa.
   
 8. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #8
  Jan 7, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  kama kweli wewe uko serious na umejitunza kwanini usubiri wakati wa kwenda kanisani ndio mpimane? tena kwa kuwekewa sheria na kanisa? mpaka mnapendana mnatoleana mahali mpaka siku ya kufunga pingu? nina mashaka na aina hiyo ya useriousness.

  wakati wa uchumba wenu hamkujigi jigi,
  1. condom haizuii kwa asilimia zote
   
 9. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...pia UKIMWI waweza kuupata kwa kudungwa sindano au kuongezewa damu yenye virusi...si ngono pekee.
   
 10. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kupima kabla ya kuoa ni lazima. Hiyo itasaidia kutokuambukizana kama mmoja wenu anao. Na kama mtaamua kuoana wakati mmoja anao, mtafuata ushauri wa wataalamu jinsi ya kuepuka kuambukizana. Nakumbuka kusikia jamaa mmoja akieleza alivyompenda binti, na binti alikuwa kaathirika lakini wakaoana, hiyo ilikuwa BBC.
   
 11. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2009
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280
  I think kwa hali ya sasa hivi labda ni mwendawazimu au mwenye mtindio wa ubongo ndiye pekee hafahamu umuhimu, maana na mantiki ya kupima kama una mpango wa kucheza pekupeku- maana watoto hutawapata ukitumia kondom!!!! au kama lbda mtu anataka ku-commit slow suicidal basi hapo haina haja ya kupima. wheather ni kuoana, ama ni long term relationship basi hakikishianneni kuwa hakuna mwenye upupu!! Tatizo la binadamu hasa mweusi ni dharau ya kujikinga na kujudge watu kwa macho. i.e binti wa kibantu wowo hilo la kumwaga basi kijana anaamini huyo ni salama. Au binti ama kijana kasoma sana si kihiyo basi huyo hana, ama ana mdaraka makubwa sana katika kampuni ama serikalini huyo hana, ama katoka juzi tu Majuu huyo hana.Ama ninamfahamu tangu utoto wetu tena tunasali/tunaswali wote huyo hana, ama ameokoka, huyo hana, ama ni mswalihina huyo hana nakadhalika nkadhalika. hizo myths ndiyo zinapumbaza watu. Please wake up na tuwaalimishe wengine. HAKUNA PEKUPEKU BILA KUPIMA. Just treat everyone as a victim. usifunikwe na upendo. Sasa ngoma baada ya ndoa. hata hapo still inashauriwa kufanya regular medical check up. ingawa kwa mmatumbi ni ndoto mpaka dalili za macho zridhie ndiyo ajikongoje just to prove sio kucheck!!
   
 12. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  SMU
  Mkulu you have said it all.Let us be down to earth,huwezi kuinsist watu wapime kabla ya ndoa wakati watu walishaonjana miezi kama si miaka mingi.
   
 13. B

  Baba Mkubwa JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 770
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kama watu walishaonjana/walishafanya mapenzi; hapa si muhimu kupima.
  However; Kwakuwa lengo mojawapo la ndoa, katika ndoa nyingi, ni kuwa na familia a.k.a watoto basi kuna ULAZIMA wa kupima kabla ya ndoa, lengo ni kujuwa kama affected then prevent affection to a child. Ulazima wa kupima unalenga kutokumuambukiza mwenza, kama mmoja anao, au kutokumuambukiza mtoto, kama wote mnao endapo ndoa itafungwa.
   
 14. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #14
  Jan 9, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,923
  Likes Received: 2,071
  Trophy Points: 280
  Sina hakika kama ULAZIMA na UMUHIMU ni synonymous. Lakini nadhani kuna UMUHIMU wa kupima afya (sio VVU pekee) mara kwa mara whether or not unatarajia kuoa. Kitu ambacho nadhani mtoa mada (pamoja na mie) anaelekea kupata ukakasi ni KULAZIMISHWA (na mtu baki ambaye si mtarajiwa/mwenza) kupima VVU kabla ya ndoa. Anayekulazimisha kupima VVU hayo mamlaka (authority) anayatoa wapi? Nadhani mtu pekee mwenye haki angalau ya 'kukushurutisha' kupima ni mtarajiwa wako kwa sababu anayo haki ya kuweka huo upimaji kama sharti la nyie kuoana. Hata yeye hawezi 'kukulazimisha' kwa sababu kama unaona haupo tayari kutimiza hilo sharti la kupima unaweza pia ukaamua kuachana na huo mpango wa kuoana nae!

  Ni vizuri watu wakaelimishwa umuhimu wa kupima afya zao mara kwa mara na si tu wakati wakitaka kuoana. Hili litapunguza matatizo mengi katika ndoa yanayotokana na matatizo ya kiafya (ikiwemo VVU, infertility nk) kati ya wanandoa.
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Jan 9, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Watu mmependana mambo ya kupima yanatoka wapi?
  Incase ikigundulika mmoja ano so itabidi muachane?
  Sasa concept ya kupendana ktk shida na raha inakuwa haipo hapo jamani.
  Kama mmependana funga ndoa mengine mbele kwa mbele.
  Alafu kama mepima wote mko -ve alafu baada ya mda mmoja akaukwaa itakuwaje?
   
 16. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #16
  Jan 24, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Siku hizi kupima ukimwi kabla ya kufungashwa ni lazima ,wanaofungisha ndoa kwanza wanataka kuona shahada ya upimwaji ila shahada kwa Tz unaweza kuzipata kimipango bila ya hata wewe kumuona daktari ni kuzungumza tu.
   
 17. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #17
  Jan 24, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...utasikia 1st date wanatumia "salama", baada ya several dates wanakuwa weshanogewa hawatumii tena "salama",

  ...kabla ya kuoana wanapima VVU, kama wako salama wanaoana.

  Baada ya several days together, wanarudi kwa nyumba ndogo na Serengeti boys wao, kwani waliwaacha salama.

  Ipatikane tu Dawa ya UKIMWI, ugonjwa umeingia pabaya.
   
 18. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #18
  Jan 24, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  KUWA LAZIMA AU SI LAZIMA KUTATEGEMEA VITU VIFUATAVYO.

  1) KAMA KUNA SHERIA, - BASI NI LAZIMA.

  2) KAMA MWENZAKO ANATAKA IWE LAZIMA, - BASI NILAZIMA KAMA
  UNAMHITAJI KWELI.

  3) KAMA WEWE UKO RADHI KUTOKAMILISHA KUOANA KULIKO KULIKO UPIME
  BASI SI LAZIMA KWAKO.

  SWALI LA KUJIULIZA NI HILI: KWANI KUNA SHIDA GANI KUPIMA?

  Exaud J. Makyao
  +255784347001
   
 19. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  na hapo ndio kwenye tatizo la mapambano ya huu ugonjwa. watu wanaogopa
  kujulikana status yao kwa kuogopa kunyanyapaliwa na kupachikwa title ya uzinzi. utasikia watu wakisema "...alikuwa akijifanya mwemaaa na hafanyi ona
  ukimwi umemuumbua...jamaa alikuwa silencer tu..."

  tukirudi kwenye mada kupima ni suala la wahusika wawili na sio ndugu
  jamaa na marafiki kuwa wanasubiri matokea ya vipimo vya wanandoa watarajiwa. ni vyema kwenda kupima status yenu kabla hamjatangaza azma yenu ya kuoana.
   
 20. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #20
  Jan 25, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hili swali limekaa mkao ...wa kwenda hospitali mpaka uumwe...Medical check-up ni msamiati kwetu...Haya kanyaga twende...
   
Loading...